Wiki mbili zitanitosha kujua gari?

Mmmh!!

Ya kweli hayo?
kweli kabisa hata mm siku ya kwanza kuendesha gar mume wangu alikuwa anaumwa ....mm nilikuwa namwona tu akiendesha kila mara nikasema nitaenda kujifunza sikuwa naenda ...ila hyo siku sitakaa niisahau nilimwendesha mpka hosp....baada ya kupona hapo hapo nilienda huo wiki 2 mana nilikuwa nikitoka narud nachukua gar naenda uwanjan najipangia mawe mwenyew
 
sasa hiv unaongeza na boda boda wa kushoto na kulia ..mwendesha bajaj na mwendesha baiskel hapo jumlisha na mtembea kwa miguu....bila kusahau na trafic anayekutegea kwenye mstar mweupe wa mwenda kwa miguu...kazi ipo
ni kweli kabsa maana hawa boda boda wa sasa hv wanajfanya wana haraka bila ya kujua sheria wala hawajali uwepo wa vyombo vngne.
 
Habari zenu ndugu zangu. Ninataka kujifunza kuendesha gari, haya magari madogo ya familia. Je, wiki mbili zitanitosha kujua kuendesha manual na automatic?
"Jiangalie kichwa chako kama kiko sawa sawa!"
 
zinatosha kabisa hasa ukipata mwalimu mzuri kama mimi nitafute nikufundishe pia ukiwa na kichwa chepesi kwa ajili ya kujua sheria za barabarani
dereva bora ni yule anayejua sheria za barabarani na kujua kumuendesha dereva aliye nyuma yake
Mkuu unafundisha kwenye driving school? Nikutafute?
 
Habari zenu ndugu zangu.

Ninataka kujifunza kuendesha gari, haya magari madogo ya familia.

Je, wiki mbili zitanitosha kujua kuendesha manual na automatic?
Kujua gari hizi auto siku 3 tu. Tatizo kujua sheria na alama za barabarani utakuchukua muda mrefu
 
Week mbili zinatosha kbsaa..mm nilijifunza kwa week mbili Lumumba driving school tena gari manual. Chamsingi ni kufanya mazoez na kuzijua sheria za barabara
Naomba mawasiliano yao mkuu nijue garama... Kuna mdogo wangu anahitaji huduma hii
 
Mimi nlisoma manual kma saa moja hivi nikaingia barabarani bas ndo ntolee....sheria nazo nlisoma
 
Gari inategemea na kichwa chako tu, wengine tulijua siku moja tu ila shida ni sheria za barabarani ndio inatake time kuzifahamu zote, kila unapoendelea kutumia barabara ndio unafahamu mengi.
 
Back
Top Bottom