Wiki 2 za kupigania Uhai wangu dhidi ya Covid-19

Wiki 2 za kupigania Uhai wangu dhidi ya Covid-19

msani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Posts
1,800
Reaction score
1,195
COVID-19 IPO!!
Haya ni maelezo ya Rafiki yangu na tukio hilo ni kuanzia takribani 20 Juni 2020.
Kwa ruhusa yake nimeweza kuweka uzi huu hapa ambapo maelezo yake binafsi. Corona ipo!!!!

Wakuu hbr zenu
Ni kama wiki imepita niliomba dawa ya flue, na nashukuru mlinipa options.

Toka siku ile sikuweza kuingia tena humu hadi siku ya leo

In short nilikua tait sana kupigania uhai, baada ya kuzunguka hospital 4 ikaonekana nina dalili zote za covid

Nashukuru Mungu kuniwezeaha angalau kuwa hai, huu ugonjwa unaua kwa kweli.

Siku ya J2 yote sikuweza kuongea neno hata moja nikiwa na madrip nikizungukwa na ndugu na jamaa Nlikua nimeshakata tamaa na umauti ulinikaribia.

Bila kujua kuwa naumwa na nini, hospitali niliyokuwepo wakaja na kudeclare wameshindwa hivyo wananipa refferal kwenda SekoToure kisha Bmc kama itafaa.

Sikua naongea lkn niliwaskia wakiongea...niliingiwa na wsws sana. Imagine hiyo ni hospital ya 3 nahama na wao wanasema walipoishia wanaona hawana option ingine..drip bado liko mkononi tukisubiria liishe ndipo niondolewe.

Drip lilipoisha basi nlilibebwa na staff wenzangu huku wakibishana, SekoT kubaya jamaa ataenda kufa huyu..eh basi mm siwezi hata kuchangia point.

Hatimaye nikapelekwa Kamanga Hosp ni kampuni kubwa private.

Tulisafiri kama dk25 hv kuna umbali, nikafika pale wakanibeba kwa wheeelchair hadi wordini.

Nilikua nakohoa jmn, mpk mbavu zinatoa mlio.

Nikapigwa sindano ya matakoni ili nikae sawa.
Angalau baada ya nusu saa ndipo nikaweza kuongea na Dr.
Nikaelezaaaa akasema sasa mbona krb kila
Kitu umepimwa, nikusaidieje.
Nakumbuka kusema, naogopa kurudi nyumbani naomba nikae tu hapa hapa.
Nilikua nimekata tamaa kbs.
Nikaanza kupimwa upya tena.
Yani nimetobolewa hii mwili jamani.

Wakaanza kupima, mara fully blood picture, mara sijui serum eeh
Mimi nawaza tu hapa siondoki..kufika sa5 hv wakaja na majibu.
Huna ugonjwa wowte ila kapimzike nyumbani🙆🏿‍♂️🙆🏿‍♂️
Nilihisi kuwa sasa ni wkt wa kuaga ndg na jamaa.
Nilikua natoa machozi kama mtoto..nikajipa moyo nikasema sawa.

Nikaomba jamaa angu afate gari akanifata, around sa6 nikafika home...nawaza tu jmn hv naeza kufa.

To make the story short, siku ilofata nlitembelewa na watu wengi home..mmojawapp ni mtu aliyekua ameugua kama mm. So aliponiona akasema ‘tyr huyu’

Walioondoka wengine akaniambia, ‘bro unajua una covid19’.

Nikasema whaaaaat?

Akampigia Dr wake akamwelelzea nilivyokua jana yake na juzi..akanipa pia nikaongea nae.

Dr akasema bro acha story fata covid kit.

Kwa kweli nikaanza kutumia hiyo kit.

Angalau nimepata afadhali..
Saivi angalau nina matumain ya kuishi.

Nimeamua kuandika angalau itawasaidia.
Mimi sio daktari lakini naweka picha za baadhi ya dawa.
 
Muoga tu huyo, Covid-19 ukiiogopa inakupeleka, ichukulie ugonjwa wa kawaida japo kweli cha moto utakiona lakini unapona vizuri tu.
 
Covid kit,ikoje mkuu .inakuwa na diagnostic tools zote pamoja na dawa za kutibu ungonjwa incase unao?.pole sanaa kwa kuumwa corona atleast tunapata shuhuda za uhakika kwan watu tushajisahau kabsaa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
IMG-20200702-WA0015.jpg
IMG-20200702-WA0014.jpg
IMG-20200702-WA0013.jpg
 
Naskia wenye vitambi kama wewe, mnapata shida sana kupumua.
Refer walio angushwa na covid kule mjengoni.
 
Wewe acha roho mbaya weka wazi ili nawengeni wanufaike.
 
Wewe acha roho mbaya weka wazi ili nawengeni wanufaike.
Mkuu sio uchoyo, hii taarifa nimemuomba mhusika kuileta humu ningekuwa mchoyo wala nisingehangaika. Rafiki zangu wawili wamekumbwa na hili. Mmoja ilimchukua wiki 4 kutoka hospital. Kwahiyo tatizo lipo mkuu.
 
Mkuu sio uchoyo, hii taarifa nimemuomba mhusika kuileta humu ningekuwa mchoyo wala nisingehangaika. Rafiki zangu wawili wamekumbwa na hili. Mmoja ilimchukua wiki 4 kutoka hospital. Kwahiyo tatizo lipo mkuu.
Hongera na shukrani kwa juhudi zako!
 
Muoga tu huyo, Covid-19 ukiiogopa inakupeleka, ichukulie ugonjwa wa kawaida japo kweli cha moto utakiona lakini unapona vizuri tu.

Kwamba wanaokufa wanaogopa Covid-19?

Hukuwasikia wale maaskofu waliokufa na Corona hali walisema wala haiwezi kuwapata?

Kuna ujasiri zaidi ya huo?
 
Ungetumia vitu vya asili usingeteseka hvo nimepitia same situation na sikwenda hospital nikupambana na Hali yangu, na kutumia vtu asilia Leo nadunda zangu, hapo ungejifukiza, uchemshe tangawizi, limao na asali kifua kingeachia, shukuru Mungu upo hai aisee.
 
Mkuu sio uchoyo, hii taarifa nimemuomba mhusika kuileta humu ningekuwa mchoyo wala nisingehangaika. Rafiki zangu wawili wamekumbwa na hili. Mmoja ilimchukua wiki 4 kutoka hospital. Kwahiyo tatizo lipo mkuu.
Sidhani kama huyo mgonjwa, naye amesajiriwa kwenye kitabu cha Ummy Mwalimu!
 
Back
Top Bottom