Wifi kazidi dharau

Julieth Ms

Senior Member
Nov 29, 2011
102
37
Jamani huyu wifi yangu amezidi dharau sana kaka angu anaumwa amelazwa Regency majirani zangu wamenisindikiza na wamemnunulia mgonjwa juice ya Azam box kubwa wifi yangu alivyo fika nakuona ile juice akauliza "nani ameleta uchafu huu yaani mnamletea mme wangu juice chafu hii mnataka ahalishe" heee si tukabaki tumeduwaa akabeba ile juice na kwenda kutupa kwenye dust bin imeniuma sana majirani zangu wameona aibu kwa kweli yaani inasikitisha ukurugenzi wake ndo unafanya adharau mpaka mali zinazo zalishwa hapa nchini? Mi nimempa jibu moja tu wifi si ungemsafirisha kaka akatibiwe ulaya avute hewa nzuri na anywe maji na juice nzuri? akanifyonya
 
Kaka angu anaumwa kwenda kumwona ndo haya sasa huu sio ubinadamu
Kesho ukienda tena mtengenezee juice fresh ili akinywa asiharishe....

Jiangalie sana na huyo wifi yako lazima kuna zaidi ya juice sio bure, manake hata kama hakutaka mumewe atumie hiyo juice angesubiri mlioleta muondoke then ndio aitupe.. Hakutumia busara ila jiulize 'KWA NINI'
 
Unajua kibaya zaidi juice yenyewe wamenunua majirani zangu na sijanunua mimi maana aliuliza huu uchafu nani kaleta akaonyeshwa wale majirani zangu yaani ubinadamu kazi jamani
 
ndio yeye hata simuelewi bidada kazi yote anajipa ya nini kifaa amechagua kaka yake yeye kutwa na njia kwenye himaya ya wifi kulikoni!
Hahahaha! Atakonda kwa mambo ya watu huyu, angepata wifi kama mimi afu anifwate mkiani hivi angejuta kunifaham.....inabidi ajiangalie mara mbili, mbili kulikoni yeye na wifie.
 
Unajua kibaya zaidi juice yenyewe wamenunua majirani zangu na sijanunua mimi maana aliuliza huu uchafu nani kaleta akaonyeshwa wale majirani zangu yaani ubinadamu kazi jamani
Am sure ameipupa vile wameleta majirani zako wewe, sasa hebu tuambie kulikoni wewe na huyo wifi ako manake sio bure!.
 
Am sure ameipupa vile wameleta majirani zako wewe, sasa hebu tuambie kulikoni wewe na huyo wifi ako manake sio bure!.

Maisha yamebadilika pindi alipo pata ukurugenzi basi amekuwa juu dharau ndo kabisaaa siku akiukwaa uwaziri au ukatibu mkuu sijui itakuwaje
 
Hahahaha! Atakonda kwa mambo ya watu huyu, angepata wifi kama mimi afu anifwate mkiani hivi angejuta kunifaham.....inabidi ajiangalie mara mbili, mbili kulikoni yeye na wifie.

Mi simfuati fuati kama unavyo fikiria wewe huyu wifi ameanza dharau baada ya kuupata ukurugenzi.
Kwa vile umeukwaa ukurugenzi ndo hutaki hata majirani zako na wifi yako waje kumwangalia kaka yao mpendwa?
 
Ww nawe hata humjulii wifi yako! Hapo ungewaambia kabisa jirani zako mgonjwa haruhusiwi kula chochote nje ya hosp, mkaenda kama wazungu. Afu inakua mtindo humnunulii chochote,kakako akitaka kitu atakuambia. Usimjibu,akikuboa cheka tu afu upone atakavyoboeka kama kichaa,lol!
 
Pole mwaya, uwe unaenda kumuona kaka yako tu vitu vingine kuhusiana na wifi yako jaribu kumpotezea maana ana dharau sana. Naona hizo hela/cheo zinampa dharau sana. Ila zina mwisho wake!!!!!!
Duniani sisi tunapita tu na hizo hela tutaziacha hapahapa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom