Wife wangu ananiibia, ushauri unahitajika

Duh!Aisee pole sana mkuu
 

Dah jamani Tanzania tumekua maskini sana hiki ni chakula tu familia na ndoa inavunjika, Hakuna upendo hata chembe
 
mkuu kuna mfumo wa maisha unaitwa "hand to mouth" yani unatakiwa usipeleke chakula mdomoni mpaka uwe umechakimeza unachokula.....Achana na mpango wa kununu stock....Kama nyuma yako ni kubwa na in store room...fungia kila kitu kwa ufungu...na asubuhi wape stock ambayo wanahitaji kwa siku iyo...ila khofu yangu huyu mwanamke hana huruma na wewe ukifanya hivi anaweza kupanga kitu chengine cha hatari zaidi na ndugu zake...kwa uwoni wangu ndugu zake ni muhimu zaidi kuliko hata watoto ambao amewazaa wenyewe...kwa io kukufanyia kitu mbaya wewe kwao sio issue...

Mkuu tunaoa kwa sababu kuu 4:
1.Ukimuangalia mkeo unavutiwa na umbile lake na unapta kupumzika.
2.Anakusaidia wewe kuweza kupatana na jamaa zako na jamaa zake.
3.Anakusaidia wewe katika kumuamudu muumba wako.
4.Anakusaidi wewe katika machumo yako na kuweza kukufanyia wepesi wa matumizi ya nyumbani na uwezo kujikimu..

Kwa hiyo Kazi ni kwako...
 
Mkuu tatizo sio chakula...tatizo ni kwamba watu wengine wanakuwa wavivu au wabahili na kuona raha kula nguvu za wenzao bila ya huruma..Mimi ni Muislamu sisi kwenye dini yetu jambo hili pia ni kharamu..na mtu ukichoka nalo si vibaya kumwacha mke....
 
Acha akili za utegemezi mtoto wa kiume,...angalia ucje...
Acha kuandika maneno nusu nusu mtoto wa kiume usije fumuliwa marinda........soma nilichokiandika kwa mara ya pili.....Unakua kama mbuzi aliyekosa majani akala chanuo
 
Mkuu nosspass fanya yote lakini la kumuacha shem, daaah, naomba pepesa macho kaka!
 
Last edited by a moderator:
Hili jipu hili..... Katika familia lazima mfanye vitu kwa makubaliano moja akiwa anafanya yake chini ya meza hapo hakuna namna ni kutumbua jipu tuuuu
 
Dah jamani Tanzania tumekua maskini sana hiki ni chakula tu familia na ndoa inavunjika, Hakuna upendo hata chembe
Kabla hujahukumu, angalia anachofanya huyo mwanamama kama ni sahihi kwa mustakabali wa familia yake. Mume kasema hajui mshahara wa mkewe unafanya kazi gani, kwa sababu huwa kila kitu anatoa mume ndani ya nyumba, mke hachangii chochote. Sasa kwa nini mke asingetumia mshahara wake kulea wadogo zake badala ya kumtwisha furushi mumewe?
 
Kwanza unaonekana unafatilia sana mambo ya jikoni!Una moyo mgumu sana duu Mimi nisingeweza kumuweka ndani shemeji Yangu tena sababu ya chakulaaaa ....hapo tatizo ni njaaa .mmh we kweli jasusi!
Ni wazi unatatizo kubwa na mkeo.

Unacho takiwa kufanya ni kukaa na mkeo chini na kumueleza ukweli kuwa na yeye aanze kuchangia na swala la kuwasaidia ndugu zake mnaweza kukaa chini na kuangalia jinsi ya kuwasaidia bila kuingia kwenye mikwaruzano.

Kama ndugu zake hawana kazi basi jitahidi muwatafutie kibarua na ni vyema mka kaa na mkeo mkajua jinsi ya kufanya!

Halafu ni wazi hili swala umeligeuza kama uadui ndio maana mkeo anafanya hivyo bila kukushirikisha!

Hebu jaribu kukaa na mkeo muongee kuhusu hili swala na uchukulie kama huo ni mzigo wako pia

True words, nadhani hii kesi isingetakiwa isifike mbAli kote mpaka polisi ni ya kifamilia sana,. Na ni kweli inabd hao ndgu watafutiwe hata vibarua wafanye kumlea mtu sio kazi ndogo umpe kila kitu chakula, kodi, mavazi, ndo mana wife anachukua vyakula kupunguza garama flani anafidia.. Ila usingewapeleka polisi jamani umewakomesha sana lol
 
Jitahid ujue pale anapofichaga kisha nawe umuibie, eeeh ndio!! Kwa kuwa hakuna namna nyingine
 
Nina mashaka na akili yako, mti mzima mwenye familia unadirikije kuja kutaja mambo yako ya kifamilia humu, tena bila soni wala haya unaomba ushaur! Mpumbavu mmoja wewe, Kweli wanaume tunazid kuadimika dunian
 
Mimi naona kuna hali ya ubinafsi kwenye ndoa yenu, hivi inakuwaje wanandoa mpaka mnafikishana polisi/mahakamani kwa issue ndogo km hizo? mchukuliane kwa kila hali jamani.
 
Tatizo huyo ni mwivi TANGU kitambo, pia anaubinafsi.
 
Pole bwashe! Wamarangu wana tabia hizo. Umeafanya sahihi. Diplomasia inatakiwa ifuate baada ya kutibua upupo.
 
Ningependa kujua huyu mleta Uzi ni Kabila gani ,? Jamaaa mchoyo hadi kapitiliza . Hili jitu sijui la wapi
 
Utelezi wa Mlenda Haumuangushi mtu mzima mkuu!

Ukiona Mbwa Anadokoa Nyumbani bhas Chukua Tahadhari..!
 
Kuna kitu kinaitwa dhamiri; kama dhamiri yako sio safi huwez kuhukumiwa ndan kuwa ukifanyacho sio kizuri. Na kuna tabia za asili inatokea majina fulan wanayo or mikoa fulan wanayo or koo fulani wanazo. Mtu akitaka awe na dhamiri safi ambayo itamuhukumu kwa kibaya afanyacho lazima awe amesimama na Mungu hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Na tabia za asili mtu anakua nazo sema hawez jua pia au anaweza jua na zinaweza kuwa hazimkeri yeye anajiona yupo sawa tu kumbe hayupo sawa. Mpka ajione ana hizo tabia pia lazima neema ya Mungu aipate au lazima amjue Mungu ili aweze kupambana na hiyo hali ndani yake kwa kuikataa na kuomba Mungu amchange. Hapo tunakuja kuona mtu kama dhamiri safi hana hata kumuomba mtu msamaha hawez sababu anajiona yupo sawa. Dhamiri( nafsi) haimshuhudii kuwa kakosea. Sitaki kukaa upande wa kwako or mkewe bt ninachojua kila mtu ana shida hapo sema kila mtu anataka kujiona yeye anastahili kuliko mwngne. Kujishusha sio lazima mdogo tu hata mkubwa waweza jishusha. Kama umemkosa mwanao waweza sema samahan bt watu hii ni ngumu bt ukiwa na Mungu ndani yako trust me kuna shida katika ndoa lakin neema ya Mungu itawabeba na mtasolve na maisha yanarud kama mwanzo. By da way pole if unajua kusali sali and muombee mkeo pia na jiombee mwenyewe Mungu atafanya njia pasipo na njia. Bwana Yesu asifiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…