Kwangu mie wife material ni mwanamke mwenye vision alie na tabia za mke au mama, anaeweza kuishi ndani ya uwezo wa kidume bila kumsumbua, asiye wakwa na tamaa wala makuu yani anaeweza kumpenda mtu kama alivyo. Mara nyingi huwaga naspot ni wale wanawake wanaoonekana washamba flani hivi mbele ya wenzao ila wapo real na life. Wife material anaweza ishi maisha yoyote yale yanayowajia na atastick na wewe na kukupa mawazo ya kukujenga na atakutia moyo ilimradi mtoboe kimaisha hata kama mna hali ya chini sana.
Anauwezo wa kukufanya ujisikie bhakressa ijapokuwa wewe ni kapuku tu na ikitokea ana uwezo kiuchumi zaidi yako atakulindia heshima yako kama mume always na kujitahidi kuficha mapungufu yako mbele ya jamii. She will never reduce you or make you feel inferior because she's a ride or die kind of woman.
Uzuri ni variable tu anaweza kuwa mzuri sana ama kiasi alimradi akonge nafsi yako tu ila mara nyingi naonaga mvuto wa wife materials wengi huwaga ni wastani compared na wanawake wenye mvuto sana ambao wengi ndio waigizaji maisha ama slay queens.