Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

in Short Board ya TTCL wengi wana Mgao toka mobile Networks kama sio wana hisa,the same na ATC shirika letu la ndege thus why linaujumiwa mchana kweupe
 
Reactions: aye
Baadhi ya sababu ni hizi..
1. Site yao moja ikizima, itachukuwa muda mrefu sana kuirudisha hewani na hii inatoka na yafuatayo
Engineers hawana magari....ni kwamba gari analo dereva, mafuta anasaini bosi, hivyo dereva akishapatikana anatakiwa aanze kukimbizana na sahihi za kupata mafuta, na baada ya hapo amtafute Engineer aliko ndipo waende site. Huo mlolongo unamaana down ni ndefu sana. Hawa TTCL walikuwa wanapata sana hela toka other mobile operators, lakini sababu hiyo hapo juu imewafanya hawa jamaa wajenge minara yao kwa ajili BACKBONE FROM ONE REGION TO THE OTHER.
2. Kutokwenda na wakati......TTCL walikuwa wanatumia SDMA kwenye mobile network yao, wakati mida hii watu wapo kwenye GSM ndani ya 3G
3. Urasimu.........Hebu niambie ilikuwa inachukuwa muda gani tangu kuomba kufungiwa simu hadi kuipata..??? Utapanga foleni utafikiri unahitaji kulazwa hospitali.
4. TTCL ina wazee wengi............ Unajuwa kuna teknolojia zinahitaji damu changa............ Mambo ya kuficha manual ili washindwe ili nawe uonyeshe umaarufu yamepitwa na wakati. Umaarufu unapatikana kwa kuchapa kazi na si kuficha informations..

Hayo ni machache...............
 

Jibu moja tu hakuna nia ya dhati ya kuendesha hilo shirika. Ni ufisadi tu mi nina share coy X niendeleze la uma ni zengwe la kuliu tu maana linakuwa lina leta kauizibe.
 
Wakati Acting management ya TTCL sasa hivi inajitahidi kuhakikisha kampuni haifilisiwi na mpaka sasa inavutia watu wengi Bunge letu la jamhuri pamoja na ushauri mzuri wa kamati ya miundo mbinu na upinzani kuwa ttcl iwezeshwe.Lakini serikali imekataa na kutoa majibu kuwa sasa hivi TTCL inasubiri kutafutiwa mwekezaji mwingine.(Airtel imeondoka??????)


Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewasahau tena Waheshimiwa Wabunge wengine

wawili na naomba niwataje, Mheshimiwa Betty Machangu na Mheshimiwa Desderius J.

Mipata. Hawa wamechangia kwa maandishi.

MWENYEKITI: Huyo ni Betty Machangu, siyo Mchangu.

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Betty

Machangu, ahsante sana. Naona maandishi sikuyafahamu vizuri, naomba mnisamehe.

Mheshimiwa Mbunge, naomba samahani kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya sita ilikuwa changamoto zinazoikabili Wizara

kutoshughulikiwa ipasavyo. Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine imeandaa

mikakati ya kushughulikia changamoto mbalimbali inazokabiliana nazo. Mathalan

kutafuta vyanzo vingine vya fedha, kushirikisha sekta binafsi katika miradi ya

maendeleo, pamoja na kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi zaidi.

158

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya saba, Serikali ikamilishe mapema Mradi wa

Anuani za Makazi na Posta. Jibu la hoja hii ni kama ifuatavyo: Mradi huu umewekwa

katika mpango wa kazi wa Wizara katika mwaka 2011/2012. Aidha, Wizara kwa

kushirikiana na wadau wengine ambao ni Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) na Wizara

ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inaendelea kubaini vyanzo vingine vya fedha kwa ajili ya

kuutekeleza mradi huu. Mazungumzo yameanza na Jamhuri ya Korea Kusini na Benki ya

Dunia, vilevile juhudi zinafanywa ili kuanza kutekeleza mradi huu Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya nane ilikuwa ni kwamba, Serikali iwezeshe

Shirika la Posta kimtaji ili liweze kutoa huduma bora zaidi na kuhimili ushindani. Majibu

ya hoja hiyo ni kama ifuatavyo: Serikali inaendelea kurekebisha mizania ya Shirika la

Posta na kufanya tathmini ya mahitaji ya mitaji kwa ajili ya shirika hilo kwa nia ya

kuboresha mtaji na kuweka mazingira mazuri ya kuliwezesha kupata mikopo kutoka

taasisi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja namba tisa iliyotolewa na Kamati ya Bunge

ilisema, Serikali ifanye juhudi za makusudi kuikwamua Kampuni ya Simu Tanzania

(TTCL) kifedha na kiutendaji ikiwa ni pamoja na taasisi za Serikali kulipa madeni yote ya

shilingi bilioni 6.3. Jibu la hoja hiyo ni kama ifutavyo: Katika jitihada za Serikali

kuikwamua TTCL kifedha na kiutendaji, yafuatayo yamefanyika:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tathmini imefanyika ili kuwezesha Serikali

kutoa dhamana ili TTCL iweze kukopeshwa fedha inazohitaji kutoka kwenye mabenki

yaliyoonesha utayari kuikopesha kupitia rasilimali zilizopo za TTCL.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, utaratibu unaandaliwa ili TTCL iweze kupata mbia

na mwekezaji mpya baada ya mbia aliyepo sasa hivi kuondoka kwenye shirika hilo.

Kuhusu deni la shilingi bilioni 6.3 ambalo Serikali inadaiwa na TTCL, Serikali itaendelea

kulipa deni hilo kupitia tengo la fedha za bajeti kwa kila Taasisi na Wizara zinazodaiwa

na Kampuni ya Simu Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kumi ilihusu Serikali isifikirie kubinafsisha

TTCL, badala yake ipewe mtaji wa kutosha ili isimamiwe na kuendeshwa na Watanzania.

Serikali tumeipokea hoja hii na jibu lake ni kama ifuatavyo: Katika jitihada za Serikali

kuiwezesha TTCL kujiendesha yenyewe yafuatayo yamefanyika:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tathmini ya kuwezesha Serikali kutoa

dhamana ili TTCL iweze kukopeshwa fedha inazozihitaji kutoka kwenye mabenki

yalioonesha utayari kuikopesha kupitia rasilimali zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, utaratibu unaandaliwa ili TTCL iweze kupata mbia

na mwekezaji mpya ili iendelee kujijenga kibiashara.



For more information visit:

http://www.bunge.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-4-25-2011.pdf
 
Haya mashirika makongwe kama TTCL,POSTA ATC nk yanahujumiwa na serikali hii. Ukiona Taasisi inatafutiwa mbia au mwekezaji jua ndo kwisha yake. Hata suala la mafuta kukosekana ni hujuma tu ili ianzishwe kampuni nyingine ipewe mtaji na serikali. UTANIAMBIA.
 
Tatizo siku zote huwa kwenye uongozi na sio kitu kungine. Cha muhimu ni kubadili uongozi wa wala rushwa uliopo na kuweka watu wenye akili zao wanaoweza kurudisha kampuni kwenye chati yake ya zamani
 

huu ni utamaduni wa walio juu ya ofisi za umma, either serikalini au katika mashirika na makampuni yenyewe, mbaya zaidi uongozi wa juu hauzingatii sana taaluma, sjui kuhusu TTCL. Mtu wa sanaa anapewa kampuni ya umeme, mabadiliko yatakayoonekana ni sanaa zaidi. Asante kwa hoja!!
 
 
Ngogo pls rekebisha post yako. Hatuna serikali. Serikali hazifanyi upuuzi wa type hii. Tanzania kwa sasa haina serikali. Anayefuatilia mambo atakubaliana nami!
 
Wanajamii tutake tusitake wageni wamekuja kuchuma tu.sisi ndio tunaweza kuleta mafanikio nchini.ubinafsishaji ulioshinikizwa na imf na benki ya dunia ulikuwa na madhumuni ya kuchota rasimali zetu na kupata masoko ya bidhaa zao huko walipotoka.ukiangalia ttcl imeweza kupona misukosuko yote hii kutokana na kuwa na wazalendo waliosoma na wenye kujua mambo kuliko hao wawekezaji.basi tusihubiri mambo ya wazungu tuache siasa tujipange pamoja kujenga nchi yetu kwa kujitoa zaidi na kutengeneza ajira na kuwatenga mafisadi ambao wanajali matumbo yao tu.pesa ambazo ttcl ilianzisha celtel hazikurudi hivyo ilidhoofisha uwezo wa kifedha wa kampuni wa kuwekeza kwenye technologia ya kisasa.
 
Ukifuatilia sana ufisadi ndani ya serikali, unaweza kufa kwa presha. Nchi inahitaji maamuzi kama ya China na Korea Kaskazini ambapo washenzi wa sampuli tuliyonayo wanafutwa kwenye uso wa ardhi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
thatha njoo na huku!

Mijadala km hii ndo imetufanya wengine kuwa wanachama wa JF cz Mtu anaandika kitu kwa kumaanisha Sasa nawewe unamuita huyo Ataanza kucfia chama chake Manake hao ndo wamefanya Jukwaa la Siasa tunakosa Mijadala ya Watu wanojitambua Wengine inatuuma sana,,,!!!
 
Last edited by a moderator:
MKAPA kainajisi sana hii nchi maana karibu mikataba mibovu na mambo machafu yote pamoja na hili la TTCL yametokea ndani ya uongozi wake,inaniuma sana yaani sisi tunaishi kwa shida halafu kuna watu wanaishi kama peponi,na huyu bwana mkubwa wa msoga ndio anajiwahia kumaliziamalizia
 
dhambi iliyofanywa kwenye uuzwaji wa nyumba za ttcl na familia ya mama Mkapa haitapotea bure..walifukuzwa wafanyakazi wa ttcl kama mbwa wameuziwa watu wa ukoo mmoja pamoja na baadhi ya maofisa wa serikali!! akiwemo Marten Lumbanga na wenzie waliokuwa ikulu wakati huo. pamoja nao ni mashemeji, mashoga na hata nyumba ndogo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!ZITARUDI TU MAANA ZOTE ZINAJULIKANA.
 

safi sana umeeleza vizuri na hakuna cha kuongeza hapo labda nikukumbushe wakati TTCL ikiwa iko sambamba na zain waliweka alama ya mfanao wa nike chini ya neno TTCL kuonyesha sasa inaenda kufa ila baada ya kujitenga ttcl walirudisha ile logo yao ya kale na ndo inayotumika mpaka sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…