Why Mlimani Tv, not ITV, TBC?


Kaka naomba niwe na fikra tofauti na zako.

Taasisi nyingi za kiserikali na zisizo za kiserikali zina sera ya mavazi (Dress Code) hivyo kusema kwamba unaweza kuvaa anyhow kwa kisingizio cha utandawazi huo ni uongo. Vaa kaptula basi kesho uendapo kazini kama boss wako atakuacha.
Kwa mfano civil servant (ke) haruhusiwi kuvaa Jeans (ref. circular ya Mh.Hawa Ghasia).

Hivi kama kweli dada zetu wa kiislam wanapenda kuvaa hijab mbona hatuwaoni mtaani/maofisini wamevaa ingawa hawazuiliwi?? Naomba kufanya assumption kuwa 60% ya watanzania ni wanawake na nusu ya hao wanawake ni waislam. Hapa utakuwa unaongelea kama wanawake milioni 12. Hata bila kufanya sensa wanaovaa hijab Tanzania hawafiki hata 10% ya hao.

Waislam wa Ufaransa nao waliwahi kuandamana kwa ajili ya hijab baada ya sheria inayozuia mavazi hayo kutungwa. Lakini hata kabla sheria kutungwa bado mabinti wa kiislam hawakuwa wakivaa ukiondoa wamama watu wazima tena waliohamia tu Ufaransa.

Kama itv, star tv na TBCcm hawaruhusu kuvaa hijab bado ni sawa coz watazamaji hawana interest na dini yako. Lakini pia being a TV presenter has a lot to do with your appearance.

Wakati mwingine sisi wanaume tunaongozwa zaidi na WIVU juu ya wanawake wanaotuhusu na si kwa sababu tunapenda sana dini na mafundisho yake.
Wanaume tuna hofu na mafataki endapo wake/dada/binti zetu wataonekana bila mabaibui na hijab!!
 
petty things like these ndizo zinaturudisha nyuma

cant we just get along?




thread kama hii ipo kwenye habari mchanganyiko na hakuna hata mtu aliyeijibu.... potezea na ondoa habari zako za uchochezi wa kidini

Can't we discuss more productive issues to our country other than this.

na wewe kiherehere cha nini...pia hapa si jukwaa lake...tafuteni jukwaa la kuchangia hiyo mmayoita mila na kumbe ni dini

mods.. hii ni justification ya thread hii kuwa ya udini...

please discard this thread ASAP

Bado hamjajibu hoja, naona mnapiga kelele na kuleta mdahalo wa kuhamisha mada.


Kwa taarifa yako tu hao unaowasema sio waislam wa kweli, ni wanafiki tu. Waumini wa kweli wa kiislam wanaofuata mafundisho ya uislam, wanaoamini kuwepo kwa siku ya mwisho, huwa hawavai vile. Usilete hadithi ya samaki mmoja akioza basi wote wameoza!!!
 
Muhogomchungu...kwani hijab ina mchango upi katika usomwaji wa habari.....
Na je kwanini baadhi ya mashirika ya kimaifa zikiwepo nchi nyingi za kiislam hawaruhusu hata kuzifaa katika media broadcasting?
Mimi sioni kama hili lina mantiki bali unaturudisha nyuma na mambo ya dini.....
 
So na wanaume wakatangaze na kanzu!!!!!!, au kanzu sio haki ya wanaume mana naona unatetea upande mmoja tu.
 

Usinchekeshe ewe muhogomchungu, unakuwa kama mgeni na nchi hii!!! Wenye makampuni/viwanda/mashirika na taasisi ambao sio waislam (waumini wa kweli) ndio wako hivyo, wametawaliwa na mfumo kristo.
Mimi binafsi nilishanyimwa kazi sababu ya kuuliza iwapo nitaweza kwenda kuswali swala ya ijumaa, ilikuwa wakti wa interview; kazi ilikuwa ni 12 hours shift 6 days in a week.


 
Muhogomchungu....kama una-consume what you grow (refer your avatar) then uko sahihi kuleta hoja za aina hii!!!
 
wa tz bana...ndo maana hatuendelei, badala ya kuongelea mambo ya kuleta maendeleo, tumekazana mara na mahakama ya kadhi, uvaaji wa hijabu...ndo maana jamii za kiafrika hususan za kiislam ziko duni sana ktk nyanja za maendeleo...wame komaa na madrassa, mwisho wa siku wanalia kuw wanaonewa.....!
 
Originally Posted by muhogomchungu

Mlimani TV inayomilikiwa na wasomi utakuona akina dada wetu ambao ni watangazaji wakiruhusiwa kuvaa hijab na huku wakiwa Live wanatangaza. hii nimeona ktk taarifa ya habari au hata katika habari nyengine lkn baadhi ya tv hawaruhusiwi. na hii kutoruhsu uvaaji wa vazi la lazima kwa akina dada wetu wa kiiislam kunaifanya baadhi ya akdada wenye imani ya kweli na dini yao wanashindwa kujiunga na tv hizo huku wakiwa na sifa zao za utangazaji . kwa mfano niliwahi kusoma ktk moja ya gazeti kwamba Sakina dotto alikata kujiunga na Itv baada ya kukuataliwa kuvaa hijab akiwa Online.na wapo wengi tu ambao kwao hijab ni lazima lakina wanasifa zote za kutangaza.
Huku tukiwa tunapigania haki za wanawake Tanzania, yaani wawe huru bila ya kuvunja sheria, vyombo vya habri vikiwa mbele kutetea uhuru wa wanawake,yaani uhuru wa wanawake na kutowanyanyaswa .
Mbona mlimani tv inawezekana na huku Itv, star tv,Tbc haiwezekani? au mlimani tv ni ya waislam?
​
HIVI VYOMBO VYA HABARI VYETU HAVIONI UMUHIMU HUU HASA TUKIZINGATIA KWAMBA HUU NI WAKATI WA UTANDAWAZI?


Wakati naiona hii thread niliharakisha kweli kutaka kuchangia maana NILIHISI ITAZUNGUMZIA KITU FULANI ambacho kinawafanya Mlimani TV kuwa tegemeo sasa...but...kuifungua ghosh...nway ikabidi nifikirie kama inahitaji mchango wangu, nimeamua kuchangia baada ya kuona dalili za upotoshaji wa ama makusudi au bahati mbaya.

Mfano mchokoza maada anasema; "hii nimeona ktk taarifa ya habari au hata katika habari nyengine lkn baadhi ya tv hawaruhusiwi..." where does s/he get inferences to draw such a conclusive argument, it may end up being an invalid argument. Unless athibitishe kuwa katika tv zote zingine alizozitaja anao uhakika kuwa wapo wasomaji wa habari wenye imani ya kiislam na wamezuiwa kuvaa kinyume na imani au utashi wao.

Nitatoa mfano. Unapomsikia mtu anaitwa Fatuma Nyangasa au Chiku pale ITV si lazima atakuwa mwislam eti kwa sababu tu jina lake...lakini pia hata kama ni mwislamu anaweza yeye mwenyewe akawa hataki kuvaa vazi hilo kama ambavyo wengine hawapendi huku mtaani au huko bungeni.

Kuna wakati ni ngumu sana ku-draw a big line/ margin between TBC na Mlimani Tv, coz mwisho wa siku zote ni offshoots za serikali (umma?) kwa namna moja ama nyinngine, hivyo sidhani kama kuna hoja kusema TBC wamewazuia bila kuweka uthibitisho wa hoja hiyo.

Mfano wa Sakina Dattoo nao pia hauna mashiko coz hauna concrete references, mtoa hoja asijifiche nyuma ya 'gazeti fulani'. Ukitumia mfano hafifu, hata kama ulikuwa na hoja madhubuti, haiwezi kuwa sawa tena.

Mwisho kabisa, mtoa hoja alitaka kutuaminisha kuwa hijab ni suala la imani (kitu ambacho ni nusu kweli na nusu si kweli) lakini baadae kumbe akajifunua zaidi aliposema "HIVI VYOMBO VYA HABARI VYETU HAVIONI UMUHIMU HUU HASA TUKIZINGATIA KWAMBA HUU NI WAKATI WA UTANDAWAZI?...my question sasa tv hizo anazozishutumu bila uhakika, ziwakubalie/ziruhusu hijab bcoz of religious belief au utandawazi??
 
EE Bwana Muhogomchungu wee....
hata mimi nimeshangaa nimetuma maoni yangu kuhusu mada ya huyo jamaa alielezea suala la OIC na Mahakama ya kadhi inajaribu kujibu hoja tu na ufafanuzi pale mwanzo ilichapishwa na nikaisoma lakini punde tu iomeondolewa sijui ni kwa makosa au makusudi nahisi harufu si nzuri hapa. tuwe huru kweli kweli kutoa maoni . nakupongeza.
 
WATU WANACHANGIA KUTETEA DINI ZAO HUSIKA,, ! CHANGIA ILI KUMUELEWESHA MTOA MADA, SIO KWA JAZBA,!
KUELIMISHANA NA KUFAHAMISHANA NDIO MSINGI WA JUKAA HILI.
Mdada mi ninamuajiri kilingana na uwezo wake wakaz sio iman yake. .
Suala liliopo hapa NI MSiwazuie kufanya kaz wakina dada wanaovaa hijabu kisa Udini,, HIJABU ni Vazi tu. Sio kwamba ni Udini,, Anaweza kuvaa Hijab na akawa bado jambazi tu.., Napia anaweza asivae Hijabu na akawa yupo fresh tu.
Pia Kila offic inataratibu zake.
 
Nadhani ni chombo husika huwa kina na dress code yao kwa hiyo tusilazimishe vyombo vingine viige Mlimani TV wao wameamua hivyo lakini hata Aljazeera huoni watu wamevaa hijab pamoja na ukweli kwamba wapo sana katika kutetea maslahi ya waislamu,ukipanda Qatar au emirates huoni mtu yeyote kavaa baibui mule jamani na dhani dhana nzima ya imani iko ndani ya moyo wa mtu lakini sio mavazi
 
Nadhani wengi wanabisha kiushabiki, lakini kiukweli vazi la hijabu linawapendeza akina dada/mama zetu. Hayo ndo mavazi toka enzi za mitume. Mfano hata masister wa kanisa katoliki huvaa na kupendeza licha ya kuwazuia waumini wao. Vichwa wazi na vimini makanisani ni mila za kuiga kwa wazungu na ndio wanatubomolea maadili yetu.
 
sasa ukivaa ushungi usoni halafu unatutangazia, tutakuonaje? na zaidi sana ni ubaguzi wa kidini na kijamii huo, kwasababu kama mimi siwapendi waislam, nikona ushungi tu, unakuwa umeshajibagua mwenyewe, kama station ndo nabadilisha kabisa hadi uondoke, kwasababu naona kama umevaa kidini fulani hivi...peleka dini yako huko kwenu kwa familia yako, pale uwe secular tu kwasababu unawatangazia watu wa dini zote, huwatangazii waislam tu, ...sasa kwanini utokee kwenye dressing stature ya waislam? wakati unawatangazia waislam pamoja na wakristo na wasio na dini? .....kwa kifupi, na kwa ushauri..hata mnapoomba kazi, muwe mnaangalia, ukija kwenye usaili na unavaa liushungi lako, mtu anakua hakuamini, anaona wewe kama ni mbaguzi wa dini vile, hivyo ili upite hakikisha kuwa wale wanaokuintervew wote ni waislam..inaweza kukuweka pabaya....kama hauamini, nenda kuomba visa US embassy na ushungi....
 
So na wanaume wakatangaze na kanzu!!!!!!, au kanzu sio haki ya wanaume mana naona unatetea upande mmoja tu.

........ kukata kuelewa kitu hiyo ni hiyari yako ! mwanamke aliyefunika kifua chake na yule aliye kiwacha wazi katika public ni yupi aliye aliejisitiri ? .............. utapendelea mkeo abane makalio mpaka ramani zionekana kisha ajipitishe kwa jamaa zako/ rafiki?:shock::shock::shock:
 

Ukimwona jamaa kavaa kanzu, kkibarkhshee na kitambaa bongo haraka haraka utasema ni mswalihina na mtakatifu lakini ukiwa saudia ni tofauti kwa kuwa hilo vazi halihusiani na utakatifu wala kumcha Mungu bali ni vazi kama mmasai avaavyo shuka yake na kuendelea kuchunga ng'ombe au kulinda geti la mpemba pale Bungoni Ilala ha ha ha. Whether mtu kavaa hijabu au laa haiwezi kuwa agenda ya nchi
 
.......... sio kweli ! huyo dada ni Mkorea/msingapore ! pia si Muislaam, hivyo ana hiyari

Nani kakwambia kuwa wakorea wote ni wakristo? Au mwislam lazima awe mwarabu? Uwezo wako ni mdogo sana. Wahi madrasa kaka muda umepita ha ha ha
 
hawa watu wanaodai hijabu ktk tv si waanzishe tv zao? hijabu bila matendo mema ni sawa na bure,Mungu anajua usafi wa mtu moyoni mwake si kwa mavazi yake.anaweza kuonekana kavaa hijabu kwenye tv kumbe ni nyumba ndogo ya mtu au kahaba fulani.Mbona aljazeera inamilikiwa na waarabu amabao ni waislamu swafi lkn je hao watangazaji wake wanavaa hijabu? sasa wasilazimishe na sie ambao si sehemu ya hijab tulazimike kuangalia hijab. tuseme na masista nao waingie studio na vilemba vyao asome habari? hii haingii akilini.
 
nini uchochezi kwa wewe, yaani kuutetea uislam ingalikuwa nimeuzungumzia ukiristo ungalipiga thanks.
TANZANIA KWANZA

Hapo kwenye red mawazo yako yanapingana na kile ulichokiandika nakusahihisha sema hivi UISLAM KWANZA nadhani umenipata vizuri

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…