Why do we repeat generational cycles, from time to time!

Mkuu ngoja niweke sawa kitu hapa.
Siyo kweli kwamba njia pekee ya kuua cycle ni kutokuzalisha. Kuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba baadhi ya experiences za wazazi zinaweza kuacha athari zinazoweza kuonekana kwa vizazi vinavyofuata, lakini hiyo haimaanishi kwamba kila pattern haiwezi kuvunjwa.

Kuna experiment maarufu iliyofanywa na Brian G. Dias na Kerry J. Ressler kuhusu kurithishwa kwa sensitivity ya hofu kati ya vizazi. Walichukua panya na kuwafundisha kuhusisha harufu ya acetophenone, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kama inayofanana na cherry blossom, na shoti kidogo ya umeme "mild electric shock", Kila walipokuwa wanawanusisha hiyo harufu waliwapiga shoti hiyo ya umeme ambayo ilikuwa inaumiza kiasi, Baadaye watoto wao, na hata wajukuu wao, walionyesha kuongezeka kwa sensitivity na fear response kwa harufu hiyo, ingawa hawakuwa wamepitia shoti ile ile,Kwa hiyo ni kwamba “watoto waliogopa viashiria vile bila kuwahi kuona shock” , lakini kisayansi zaidi ilikuwa increased sensitivity/fear to that odor cue, si lazima sawa na kuwa walijua tukio lote la shock... si kwamba watoto “walikumbuka tukio” moja kwa moja kama kumbukumbu kamili, ila vinasaba vyao vilikuwa na Kumbukumbu au information ambayo wao hawajawahi kukutana nayo ila iliwaambia wakinusa watapata tukio fulani.

Sasa point ya muhimu hapa ni hii, si kwamba watoto walirithi kumbukumbu kamili ya tukio lile, bali walionyesha increased sensitivity ya ile harufu kadri kizazi kinavyoenda. Utafiti ule ulipendekeza kuwa kulikuwa na mabadiliko ya epigenetic yaliyohusishwa na sperm ya wazazi, kwa hiyo si “memory” ya tukio lote moja kwa moja, bali ni aina ya biological information iliyoongeza uwezekano wa response fulani.

Kwa hiyo inaonyesha kwamba wakati mwingine unaweza ukawa upo ndani ya pattern inayokutisha au inayokuendesha bila hata kujua imeanzia wapi. Inaweza kuwa fear, trauma, tabia za uharibifu, au mazingira ya kifamilia yaliyokaa kwa muda mrefu sana. Lakini ukweli wa pili muhimu ni kwamba pattern haimaanishi sasa kwamba iko milele.

Kikubwa ni kuitambua hiyo pattern na kuanza kuivunja. Iwe ni pattern ya uzinzi uliopitiliza, ulevi, umaskini, violence, neglect, au hata mambo ambayo watu huyaita uchawi wa kifamilia, point ni kwamba ukishaijua una nafasi ya kuibadilisha. Kuvunja pattern hakumaanishi unafuta history yote ghafla, lakini unabadilisha direction ya maisha yako, mazingira yako, choices zako, na malezi yatakayofuata.

Ndiyo maana mimi nasema suluhisho si kutokuzalisha (Kuzaa) , bali ni mtu kujitambua na kujifunza kidogo kidogo kujiondoa kwenye hiyo pattern. Kwa sababu unapobadilika wewe, huwi media au intermediate host wa kupitisha mbele script ile ile kwa nguvu ile ile. Vizazi vinavyokuja havipokei mazingira yale yale, malezi yale yale, na responses zile zile. Hapo ndipo cycle inaanza kufa.

Kwahiyo yeye azae kama anataka, lakini ajifunze kwanza kuitambua hiyo pattern, aifanyie kazi, na aianze kuivunja. Maana cycle nyingi haziishii kwa kukata kizazi, zinaishia kwa mtu mmoja kuamua kuishi tofauti.
 
Kwahiyo yeye azae kama anataka, lakini ajifunze kwanza kuitambua hiyo pattern, aifanyie kazi, na aianze kuivunja. Maana cycle nyingi haziishii kwa kukata kizazi, zinaishia kwa mtu mmoja kuamua kuishi tofauti.
Na mimi mkuu nilichomaanisha ni hivi sio kwamba asizae kabisa kuendeleza Genetics zake ila km atazaa basi asiendeleze kile alichonacho yaan mfano anazaa yeye ni msabato pure au ni mlokole pure au Mwislamu safi basi akataka amshinikize na mtoto wake apite njia ile ile anayoitaka yeye, yaan amuache mtoto wake achague njia yake mwenyewe kabisa anayoitaka asimwambie usipite huku pita huku mfano wa hofu ya kifo ni sawa na mama anaetembea na mtoto wake mdogo anamvusha mpaka barabara amuachi avuke mwenyewe kwanini..? Kwa sababu akivuka vibaya gari likija litamgonga atakufa.
Sasa hapo ndio unaiendeleza ile cycle ya kuogopa kifo.

Unajua kuna sehemu km tunataka kufanana kwa namna fulani ila kuna namna tunapishana deep inside kuna kitu tupo equal ila km vile wewe unapita kushoto mimi napita kulia ila tunazungumzia kitu kile kile - how to break generational cycle and create your own legacy, lakini najua unaelewa namaanisha nini.
 
naelewa upande wako sana, naona mjadala unaanza kukua sasa....How comes anaweza kumfanya mwanae achague anachotaka after brainwashed him/her?
kwa mfano uliochagua yaani yeye kama ni msabato au Mwislamu atamwambia achague atakacho?
lakini usisahau mtoto anakuwa kwenye mazingira ambayo ni tegemezi mpaka atakapojitambua wakati huo tayari umeshamlisha ideology za generation cycle yako Kibao unategemea atachagua nini??? zaidi ya Hiyo hiyo cycle...

kwa mfano una mtoto amezaliwa Roma amekulia vatican unahisi atachgua uislam ,uhindu au ubuddha kuwa dini yake?? na hiyo ndo huwa Ngumu kuvunja cycle.. kwa sbabu ideology tunawaingizia watoto wetu kabla hawajafikia uchaguzi maalumu kuna kitu kinaitwa Illusion of choice..au Power of manipulation.... hiki ndo unachokizungumzia?

wazazi mara nyingine tunakuwa kitu kinaitwa
arhitektonikí ton epilogón
yaani Choice Architect.. "kupanga mazingira ya uchaguzi kwa namna inayomfanya aelekee option fulani tunayotaka sisi" na hapo sasa tunakuwa hatuvunji cycle tunacreate cycle iliyo cements yaani yenye reasoning ya kwanini yupo kwenye cycle hiyo.....Sijui kama unanielewa?

Kwa lugha nyingine jiondoe kabisa kwenye cycle kama unaona haikufai na mtoto atafuatilia maamuzi yako tangu akiwa mdogo na ataamua then cycle itavunjika...
 
How comes anaweza kumfanya mwanae achague anachotaka after brainwashed him/her?
Inatakiwa iwe hivyo ili cycle ife yeye anataka kuiua cycle na ukitaka kuiua cycle hutakiwi kuiendeleza ni sawa na yule Mama alieenda kumtupa mwanae Guest akachukuliwa na familia namba 1 nchini anaishi kule hatoishi maisha aliyokua anaishi mama yake hatokua anakatazwa km ambavyo angekua anakatazwa na mama yake dini hatokua na ile dini aliyokua nayo mama yake labda alikua msabato au mlokole kule atakua Mwislamu kwa sababu lazima apitishwe kwenye cycle aliyopo na ataishi ndani ya hio cycle kwa jinsi cycle inavyotaka, napenda kutumia mifano hai sio mifano ya kupikwa kwenye Internet
 
Mkuu umechambua vizuri sana,lakini pengine wasomaji wangetamani kujua mechanism za kuvunja hizo pattern...
 
vizuri!,
but nieleze How comes unaweza Kuua cycle kwa kucements za existing cycle?
yaani unawezaje kutengeneza Reasoning for teaching Faith and believing?
sijajua upande wako kiukweli!
yaani kusema kwamba inabidi uwe kwenye cycle iliyopo ili kuvunja cycle ni sawa na kusema ili kufungua minyororo ya Pingu ni bora kuiacha mikononi hivyo hivyo itaoza yenyewe!
thats ideology haiko sawa..
Yaani ili uweze kushiba inabdii ukae kwenye njaa?
huyo mtoto uliyemtaja hapo hajavunja Generational cycle ila amechange destiny kabisa ya maisha yake na so Yuko nje kabisa ya cycle yaani Universe imemtoa nje ya cycle...
kwanini Hatajua mzazi wake ni nani,Wala hatojua Ukoo wake ni upi so hatoishi kwenye Mazingira yanayoinfluence his culture na cycle yake (kwahiyo mfano wako Uko taofauti kabisa na Ideas za mtoa Mada)

natamani kujua uliposimamia ili tuweke mjadala sawa
 
kwa mfano uliochagua yaani yeye kama ni msabato au Mwislamu atamwambia achague atakacho?
Yes, ni sawa unapoona mtoto wako anachezea wembe au anachezea moto au analisogelea shimo refu ambalo akiingia linaweza kuchukua uhai wake basi muache apambanie nafsi yake km patatokea mtu wa kumsaidia atokee na amsaidie kwa namna yake ila sio wewe, wewe si unataka kuiua cycle au unataka kufanyaje?

Anachezea wembe mwache ajikate atajifunza kwamba wembe sio wa kuchezea ataanza kujitengenezea cycle ya kwake mwenyewe, anachezea moto umemchoma ataanza kugundua kumbe huu ni moto na unaunguza ataanza kutengeneza cycle yake kwamba moto sio wa kuchezea ila sio kwamba Baba alisema au Mama alisema moto unaunguza kwa hio nisiuchezee, subiri kwanza aungue ndio anatengeneza cycle yake sio cycle yako
 
Uzi ulitakiwa ufungwe hapa.!!
Umemaliza yote mwanakwetu. Bravo 🤩
 
Mkuu ninaweza kukuthibitishia kuwa Kuna study kadhaa zimefanyika na zimeonyesha kuwa Meditation inauwezo wa Kurewrite DNA na kuweka sawa na kubadili baadhi ya information Genetically ukihitaji mjadala kuhusu Hilo nipo nakusubiria..
 
safi sasa Hapo tuko pamoja kabisa!
but usisahau kuwa infuencer wa Hayo yote ni Mazingira..

but you made a Point
 
lakini usisahau mtoto anakuwa kwenye mazingira ambayo ni tegemezi mpaka atakapojitambua wakati huo tayari umeshamlisha ideology za generation cycle yako Kibao unategemea atachagua nini??? zaidi ya Hiyo hiyo cycle...
Sasa ukitaka kuiua cycle hutakiwi kuiendeleza ile cycle unapokua na new generation iache new generation ijiendeleze yenyewe sio ipate feed-in kutoka kwako kwenye cycle yako kuingia kwenye new cycle inakua cycle ni ile ile haifi inaendelea kuwepo vile vile vizazi na vizazi,
 
Mkuu ninaweza kukuthibitishia kuwa Kuna study kadhaa zimefanyika na zimeonyesha kuwa Meditation inauwezo wa Kurewrite DNA na kuweka sawa na kubadili baadhi ya information Genetically ukihitaji mjadala kuhusu Hilo nipo nakusubiria..
Seran umemsoma huyu jamaa? Achana na yule anakuambia kuhusu damu ya yesu.
 
kwa mfano una mtoto amezaliwa Roma amekulia vatican unahisi atachgua uislam ,uhindu au ubuddha kuwa dini yake??
Hapa ni kwenye kumuacha yeye achague mwenyewe sio kumchagulia mpe nafasi ya kuchagua, mfano muache mwenyewe ajifunze kuhusu uislamu, uhindu, ukristo, nk kisha mpe mwenyewe achagua anataka kukaa wapi na hio ndio cycle yake sio ya kwako
 
Hapa ni kwenye kumuacha yeye achague mwenyewe sio kumchagulia mpe nafasi ya kuchagua, mfano muache mwenyewe ajifunze kuhusu uislamu, uhindu, ukristo, nk kisha mpe mwenyewe achagua anataka kukaa wapi na hio ndio cycle yake sio ya kwako
nipe Notion ya mtoto wa Miaka 5 (kipindi ambacho huwa mtoto anafuata mazingira na mafundisho na anayahifadhi kichwani kuliko wakati wote) utaweza kumfundisha kufuata na kusoma Uhindu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…