marriage instead of merriage!
product za mlimani hizo mkuu.....!
Badala ya kwenda kwenye hoja ya msingi tunaanza kuangalia vitu vidogo vidogo ili mradi kumkwaza tu mtu jambo ambalo si la kiungwana,hakuna ambaye hakosei humu na kama unataka kumrekebisha mtu basi tumia njia ambayo haitamfanya aonekane hajui na ikibidi mpe namna ambayo itamfanya ajifunze zaidi.
Mlimani wapi wewe,hao hawana msingi mzuri wa kingreza....toa bias hapa inawezekana huyu ni wa cbe unaposoma.
Kwa ufahamu wangu mimi ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili kuishi pamoja kama mume na mke,makubaliano haya yanalenga katika kuijenga au kuanzisha familia na mambo megine ya kimaisha.Inapokuja pale hakuna makubaliano basi hiyo sio ndoa,au mmoja akaoa/kuolewa "KWA SABABU YA...",hapo hakuna ndoa.asilimia kubwa ya ndoa zetu za sasa hivi hazidumu(huvunjika) ni kwa ajili wengi wetu tunaoa/kuolewa kwa sababu ya... (KULAZIMISHWA,PESA,UZURI,KUFUATA MKUMBO..n.k),Yule aliyekubali kuoa/kuolewa kwa dhati ni yule mwenye kukubali yote yale yanayotakiwa kuwepo katika ndoa ikiwepo UAMINIFU,UKWELI,UPENDO,....na kubwa zaidi ni kumkubali mwanandoa mwenzako jinsi alivyo ikiwemo mapungufu yake au udhaifu wake.Zaidi ya yote uaminifu ndio muhimili mkubwa sana katika ndoa.Wapo wanao owa au kuolewa hali akiwa bado anamahusiano na mpenzi wa zamani,hapo hamna ndoa.Kwa mimi nadhani huo ndio ufahamu wangu katika ndoa,naomba kwa wale wenye upeo zaidi watujuze juu ya hili
hebu tujadili hoja za msingi, makosa haya ni ya kawaida, it doesn't mean kuwa hajui-just a typing error ambayo hata muingereza mwenyewe anafanya. Hacheni kuwa na mawazo "mgando". Kama huna hoja kaa pembeni upige umbeya ma'ke ndo inaonekana fani yako wewe na wengine wa aina yako!:a s 13:]samaki mkunje angali mbichi....penda mtu anayekusahihisha kwa mambo madogomadogo[/color] .
Do you get marriage or married?
ndoa yako imesambarika nini mkuu, nakumbuka kuna thread ulianzisha hapa yale machungu uliyatoa kuhusu ndoa kuvunjika! ukijumlisha na hii ya leo,? life life
umesema vizuri kuhusu ndoa. Ila kuna wengine ambao hubadilika, kabla ya kuoana anakuwa mtu mpole, mwenye upendo wa dhani na kujali mpaka mwenzake anasema huyu ndio mwenza wangu wa kufa na kuzikana. Na akakubali kuoa au kuolewa naye kwa kusema haya mapungufu madogo madogo hayana matatizo nitakwenda taratibu tukirekebishana. Lakini wakishaoana na kuisha pamoja zaidi ya miezi 6 basi makucha ya huyo mwenza yaannza kufunguka na vituko visivyovumilika vinaanza, hapo ndipo doa linaanza na kupelekea baadhi ya ndoa kuvunjika.
Muhimu ni kuwa wakweli tangu mwanzo ili muweze kujuaana kwa undani, jua tabia za mwenzako vizuri. Kikubwa kuliko vyote ni uvumilivu. Mkiishi watu wawili ambao mlilelewa tofauti lazima mtapishana kiswahili kidogo kwahiyo mnahitaji kuvumiliana na kuaminiana, mkufuata hayo mtadumu kwenye ndoa.
shukuuru mungu yanayolipuka ndan ya mwaka wengine wana wajukuu na magari majumba unakosa sababu nini nini??hii n laana ya kuvunjwa wapwa hatari sana..na hizi zimeasisiwa na wazazi wetu,,,wewe mzazi unaenda kukutana na mkeo kwenye harusi ya mwanao baada ya mwaka mmoja ama miwili..uoni unaenda kumuongezea laana..aiwezekani baba mmeachana alafu mtoto aanze mambo yake uende kumsuluhisha kama nani..kwa nini usianze na ndoa yako.....embu ninyi wazee leo nasema ukweli bora muache kwenda arusi za watoto wenu kama mmeachana mnaleta unafiki wa kulishana keki za kina jeniffer,best byt kisa uwepo kwenye mkanda nasema ukome kabisa na harusi ni sehemu takatifu kama ulivyo mwili wa watoto zenu..acheni kwenda kunajisi harusi za watoto wenu aijalishi uko nae vipi...
Rekebisha ndoa na mkeo uende ya wanao..usijiaibishe kwa mambo madogo..kama pilau wambieni wawapelekee m nasema hivi nikimaanisha jamani....nawatakia maisha mema wanandoa walioamua ndoa kutoka mbinguni