Ndoa hujengwa kwa vitendo siyo maneno

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
NDOA NI TOFAUTI KABISA NA KUTAFUNA KARANGA UNAWEZA UKAJIKUTA UMEOKOTA NDIMU CHINI YA MZABIBU.

Yaheshimuni mabati na milango yenu maana yanawafichiaa siri kubwa katika ndoaa zenu , yaheshimuni mageti yenu na walinzi wenu maana wanayo siri kubwa juu ya ndoa zenu ,wapendeni wafanya kazi wenu wa ndani maana wanajua uchafu mwingi na mauza uza yaliyo katika ndoa zenu ,msijisifie kwa kuolewa na mabwana wenye pesa Au kuoa wanawake wazuri ila umizeni kichwa kuhakikisha ndoa zenu amani na furaha imetawala ,usione milango imefungwa na taa zinawaka ukajuaa kuna amani , kukimbilia kuolewa au kuoa haimanishi umemaliza maana ndoa inaweza ikakumaliza pia ni suala la mda tu, tambuaa umeingia kwenye mchezo ambao refa ni wewe ,kocha ni wewe mwenyewe na mshabiki ni wewe ndoa inapaswa kuheshimiwa ndoa ni tofauti na kucheza singeli au kuangalia kipindi cha shilawadu muheshimu mke wako muheshimu mme wako hata kama amechoka ungana naye muwe kitu kimo UNAFIKI, USALITI ,MAJIGAMBO NA VISASI vitaangamiza na kupoteza utamu wa ndoa.

Kuna wakati Ndoa ni kama kamali kuna kuliwa kuna kupata, lazima uwe mwepesi wa kuona visivyoonekana , pukurushani zipo mauzi na changamoto ni mambo ya kawaida lakini ukijifanya unayajua na umevurugwa utajikuta unaposti instagramu kwamba WANAUME WOTE NI NYOKO TU wakati una mme ndani ndoa haitaki mihemko maana mwisho wa siku utajikuta unashitaki ndoa yako facebook badala ya mahakamani ukiparamia utajikuta unamposti MCHEPUKO WAKO KWAMBA NAKUPENDA MILELE WAKATI UNA MKE NDANI.

Utajikuta unatukana wazazi wako waliokuzaa matusi makubwa kisa ndoa imekuvuruga ,punguza mchecheto katika ndoa ,ukianza sarakasi zako unahatarisha ndo yako ,sio kidogo tu umenuna ,kidogo tu umekimbilia kwenu kwa wazazi wako ,Mara umetafuta mwanaume mwingine mme wako humtaki ukiulizwa kwa nini ooh mwanaume mashine bwana.!! sasa tangu lini uliambiwa mashine zinaoa ..?

Waungwana ambao mko kwenye ndoa na ambao mnatamani kuwa wake au waume apo baadae tambueni kwamba ndoaa NI KAMA MCHEZO WA DRAFTI maana ukiwa na hasira kwenye mchezo wa drafti hutaweza kucheza na watu maana mwisho wa siku utarusha mgumi na mateke, ebana NDOA HAITAKI HASIRA KABISA , inaitaji kuwa mwelevuu kama nyoka ina hiitaji khekima na maamuzi,ndoa haitaki bangi wala pombe ,usipeleke usomi wako kwenye ndoa utaaumiaa ,usipeleke usupa star wako kwenye ndoa ,usipeleke uzuri wako kwenye ndoa ukifanya ivoo basi huna ndoa dada yangu ,ukipeleka ukuaji na ujuvi ndoa imekushinda hakika ,kuwa mstaarabu kama kinyonga na mwenye akili nyingi kama sisimizi ,kuwe mwepesi wa kusamehe nakufuta makosa mapema iwezekanavyo maana ndoa siyo vitaa ndugu zangu ,unakuta mtu anamtandika mwanamke vibaya mno uku akipayuka mbele za watu huyu mwanamke malaya sana uku akimshushia makombora na mvua ya ngumi ukifanya ivo hiyo siyo ndoa imekushinda.

Inavyoonekana kwa sasa Mapenzi ya kweli yanapatikana nje ya ndoaa na siyo ndani ya ndoa sana sana katika nyakati hizi maisha yanaonekana kuwaacha vijana chini ya mti kavu ,kipindi hicho utasikiia watu wanaitana majina ya ajabu ajabu mara utasikia malaika wangu sijui ni lini malaika akaishi duniani ,tangu lini malaika akafanana na binadamu mtu anamwita mpenzi wake malaika wangu na hapo ndipo tunapoonza kufeli ,nje ya ndoa inaonekana watu wakila bata sana kuliko ndani ya ndoa ,watu wanakula bata tu na siyo kuku tena ,kila kona wapo,wanajiachia hatari hatari hawasikii hawaambiliki lakini hayo yote ni mbwe mbwe tu ngoja wafunge ndoa kama utawaona tena facebook ama whatsap atakupenda na kukujali ukiwa hijamuoa au kuolewa je kwenye ndoa pia atakuheshimu na kukujali kama enzi za uchumba..??, je alikwambia atakupenda mpaka kufa ni ya kweli hayo..? alisema atakuwa na wewe katika shida na raha tafakari je ni ya kweli hayo au anang'ata na kupuuliza tu kama panya..!!,,pimeni kauli za wapenzi wenu kabla ya ndoa siyo mnaunga mkono kila kitu ,mtu anapokwambia atakufa na wewe je anamaanisha maana hakuna mtu anayekufa kwa ajili ya binadamu mwenzake isipokuwa Yesu mwana wa Mungu.

Mfalme suleimani ndoa ilimshinda mbali na kwamba alikuwa na wanawake 700 na wengine 300 jumlaa 1000 ,alikuwa na hekima ambazo zilitosha kabisa kuwadhibiti lakini hilo lilionekana kuwa tofauti kwake,alikuwa na utajiri ambao haujawahi kutokea duniani lakini wanawake walimchanganya akamsahau MUUMBA WAKE ,ndoa ni mtihani ambao umewashinda wengi sana,kumbe pesa siyo kigezo cha wewe kudumu katika ndoa ,maaarifa na elimu siyo kigezo cha wewe kudumu katika ndoa ,umaarufu ulionao siyo kigezo cha kudumu katika ndoa ni vyema pia Kumtanguliza Mungu ili ndoa yako iwe imetulia na yenye furaha na yenye mafaniikio siku zote.

kumfahamu mwanamke siyo jambo la usiku umoja ,inaweza ikakuchukua miaka 3-5 kumfahamu mwanaume siyo jambo la mwaka 1 itakuchukua miaka pengine hata 15 kumfahamu mme wako hivyo basi hata kama Tunamuomba Mungu atusaidie Lakini pia na sisi tusilale na kubweteka tukimuachia Mungu lazima tutumie akili zetu za kibinadamu ,kuna wengine wanaona leo kesho jioni kila mtu yuko kwao ,kuna wengine wanaona leo wiki mbili baadae wamechomana visu vya tumbo ,ndoa kweli walisema ndiono yaani kuna mwingine kafunda ndoa juma pia jioni kesho mchana kafuniwa na baba mwenye nyumba ,unampenda mtu sana lakini mnaenda kucheki afya unaambiwa mmoja wenu ana ukimwi tayari malengo yamekufa na unaenda kucheki afya unaambiwa na wewe una ukimwi ,mnafunga ndoa leo kesho asubuhi unasikia bwana harusi amekutwa amekufa chooni ,FUNGENI NDOA ZA GHARAMA LAKINI TAMBUENI MNAINGIA KWENYE MKATABA ULIOJAA HOJA NA VIOJA.

Watu wengi wanafunga ndoa katika umri mdogo wapo katika athari kubwa ya kuachana na mke au waume zao,kuanzia miaka 21-25 ndoa nyingi zimeonekana kuvunjika fanya mental tour Tanzania hii utagundua wengi walioana katika miaka ya 21-25 ndoa zao 70% zimevunjika na kuwakimbia watoto wao na wake zao kwa ujumla ,KUOA KATIKA UMRI MDOGO KUMEONEKANA KUWA NI CHANZO,wengi ndoa nyingi pia zimevunjika kwa sababu wengi wameonekana kuwa wadogo ambao bado hawajakomaa sawa na hawajui namna ya kuishi na wake au wanaume zao,hawa ndio unakuta ameoa lakini utoto mwingi kichwani hatambui hata majukumu yake japokuwa hili lipo hata kwa watu wazima ,ameoa lakini yupo kucheza drafti au mpira usiokuwa na tija wengine wana wake ndani kutwa nzima wanacheza pulitable au yupo vijiweni anapiga soga na tarihi vijana wengi wanakimbilia ndoa katika umri mdogo ndoa zimeonekana kuto kudumu nyingi huchukua miaka siyo chini ya 1-5 hawa ndoa wale wanapokuwa kwenyw shida wanaanza kulia au kuwasukumia mzigo wazazi wazazi wao KWENYE NDOA KIDOGO VITA KIDOGO AMANI hayo ndio maisha ya ndoa lazima ujifunze kuyazoea hayo maisha .

UMSHAOLEWA TULIZANA, UMESHAOA ACHA KUCHEZA KWANGARU MPENDE MKEO ,siyo umekuta sms tu unataka kung'oa pua ya mkeo au mmeo,kosa dogo ushatangazia ummaa kwamba kimeshanuka huelewi wala husikii hakimu wewe mshtakiwa wewe,hujakaa hujatulia kijasho kinakutoka unaojiona wewe doni unarusha mateke as if unatolewa nyongo macho yamekutoka kama unauwa nyoka hapana ndoa inahitaji utulivu uliotukuka ,siyoo kidogo tu mara umeenda kuomba suluhisho kwa padre ,hukulazimishwa kuolewa au kuoa Bali ulitaka mwenyewe sasa in vyema ukapunguza mchecheto pambana maana ndoa siyo uwanja wa maonyesho bali ndoa ni sehemu ya pili muhimu katika maisha yako kabla ya kifo usichezee na usikurupuke kama upendo umepotea ndani ya ndoa Muombe Mungu maaana pengine ndoa yako inayumba kwa sababu umekuwa mbali na Mungu wako.

Katika ndoa mchezaji ni wewe mpiga penati ni wewe mwenyewe lakini tambua pia mshabiki ni wewe ,hata punda atembee kwa kuinama inama lakini mzigo ufike na mshindi apatikane ndio ilivyo ukiolewa ujue umeingia kwenye sayari nyingine usilete maisha uliyokuwa ukiishi pale ulipokuwa single, kama umeishi na mke wako miaka 10-20 basi mwambie Mungu asante , kuna dada wengi wameachika tena wengine wameachiwa watoto wanaume wamewakimbia kuna wanaume wameachwa wakiwa wamesimama na miguu yao wamebaki wanatukana na kufyonza fyonza ovyo, kunaa wengime walikuwa wanakula utamu wakasahau kwamba unapoona utamu tu tambua pia uchungu upo karibu ndoa ni sawa na vitani kidogo tu mambomu kidogo tu risasi kuishi kwenye ndoa kunahitaji roho ngumu na ustadi wa hali ya juu.

TABIA ZA KITOTO HAZITAKIWI KATIKA NDOA,ndoa nyingi zimewashinda watu wazima kwa kuendekeza utoto ,ndoa nyimgi zimeshindikana maana watu hawataki kibadili tabia miaka yote ni yule yule tu ,ukiendekeza utoto na ushenzi ushenzi wewe huna ndoa na itakushinda siku ya juma pili na juma tatu kazini ,Ameoa mda mwingi yupo club anadai anakula maisha tangu lini maisha yakaliwa, hayo maisha si ukale na mke wako nyumbani, mtu ameolewa lakini halali ndani kurudi kwake asubuhi,ameolewa lakini nguo anazovaa anaacha makalio njee sasa uliolewa ili iweje kama kuvaa kwenyewe huwezi,,mataifa kama mashariki mwa ulaya hawatakuruhusu kuwa na mke kama hujafikisha miaka 25 na kuendeleaa na kama humjajuana kwa mda wa miaka isiyopungua 2-5 wazazi hawatakuruhusu upate mke au mume pia ,na kigezo kikubwa ni kwamba lazima uwe umejijenga kiuchumi na maisha yakoo yanaeleweka lakini pia lazima wazazi wahakikishe unajiweza kimawazo ,siyo uku Afrika mtu akiona ana makalio makubwa basi anataka kuolewa mtu akiona amevimba kifuaa na kajikazi tayari anatangaza mke kanisani ,KWENYE NDOA KUNA MITIHANI PUNGUZA UTANI ILE ULIYOFANYA UKIWA SHULENI AU CHUONI NI TEST TU.

Wapimeni na kuwachunguza wachumba kwa kina zaidi ,siyo mnakubali kila kitu kwa sababu tu ana makalio makubwa na shape kama tunda,msiwe wepesi wa kuitika kila kitu kisa anakupa vihela hela vya kubadilishia nguo ,tafakari ahadi zake wengine wanaongea ivo wakiwa usingizini msiwaamini sana ,katika 100 ni 20 tu wanafurahia maisha yao ya ndoa lakini 80 kati yao wanalia kila kukicha na yote haya ni kwa sababu ya ugumu wa maisha au kutokuelewana baina ya mke na mume au pengine magonjwa , kawaida utadekezwa ukiwa kwenye uchumba lakini ukishaolewa mambo yote haya hupoteaa kama mvuke,ukiingiaa kwenye ndoa hakuna kudekezwa tenaa sijui kunakuwaga na shida gani kwenye maisha ya ndoaa ,ukiwa kwenye uchumba ukiliaa kidogoo tu huyu hapa,ukiomba kitu kidogo tu tayari ushapewa au kupata .

Wengi wanaamini kwamba maisha ya kwenye uchumba ni sawa na maisha ya kwenye ndoa,au kuna wengine wanategemea makubwa watakapoingia kwenye ndoa wakiamimi kwamba atapata raha kuliko maelezo,wengi wanaamini kwamba jinsi anavyosikilizwa akiwa kwenye uchumba basi na kwenye ndoa itakuwa ivoivo kwenye ndoa. Atakujali sana maana anapaliliaa shamba lake lakini kishakuwa kwenye ndoa mambo yana badilika maana mmeingia kwenywe maisha mengine na tofauti kabisa na ya uchumba hapo kama alikuwa anakuita my blanketi ,my queen ,my boo ,my life ,my everytino ,wangu wa ubani ,sijui malaika wangu hutasikia tena hayo majina hakika ,hutasikia tenaa anakupa mahaba ya moto ,hutasikia sauti ile ya kumtoa nyoka pangoni zaidi ya hapo utasikia lugha zingine ambazo hukuwahi kuzisikia kamaa *hivi wewe una akili ,hivi sijui kwa nini niliolewa na wewe *utasikia nilifikiri nimepata mume kumbe michosho tu ,"utasikia kama umehoka naomba uende kwenu *hayo ndio maisha ya ndoaa yanahitaji moyo wa nyama na roho mgumu yenye uvumilivu wa hali ya juu .

Wapendeni wake zenu kila jua linavyochomoza na kuzama maaana hao ndio faraja waoneni kama lulu muwatiapo machoniye , ongeeni nao kwa sauti ya upole na busara hata wamewatenda vibaya,watiini na muwaheshimu waume zenu hata pale wanakuwa wanapitia kwenye magumu kuweni faraja kwao maana MUNGU HUBARIKI NDOA ZENYE UPENDO WA KWELI,Vijana wa kizazi hiki hawajui kuchagua wanawake maana wake zao wengi wanawatolea instagramu na facebook na vyuoni uko pasipo kusahau whatsapp ,vijana wa sasa wanataka wanawake ambao wamejaza nyuma lakini siyo kichwani ,vijana wa sasa wanataka wanawake ambao wakitembea nao barabarani waonekane kama wanapaa na watu wawasifie ,mtu akiona ana kashape kama chura wa migombani na vinyonyo vimebinuka kama mkuki wa kimasai na anazijua zipi mihogo na zipi magimbi tayari watu wanamsumbua sumbua tayari mtu anaona afaa kuolewa nani amekudanganya kwamba kwenye ndoa ni uwanja wa maonyesho , kwa wanaume akipata kikazi tu cha mshahara wa laki 300000-500000 basi anaona amekamilika na anaweza kuwa na mke anayemtaka ,KUWA NA MAKALIO MAKUBWA SIYO KIGEZO CHA WEWE KUOLEWA NDOA NI TOFAUTI NA MAONYESHO YA NANE NANE ,na hata hivyo ukienda ujerumani mashariki na maeneo kama marekani ndoa nyingi hufungwa kwa mikataba hakuna kuchezeana chezeana mkataba ukiisha basi kila mtu anafuata mambo yake .

kuna mtaalamu mmoja aliwahi kusema kitu pekee ambacho dunia inapaswa kujivunia kama urithi basi ni utandawazi na utandawazi huu umeonekana kuwa hatari sana endapo tu hutakuwa makini nao ,watu wameolewa lakini hawataki kuacha ujana kabisa na hawako tayari kuacha usasa mtu kaolewa lakini hataki kuacha kuvaa vimini ,hataki kuacha kujibinua binua makali na kujipitisha pitisha mbele ya vijana ,mtu ameolewa lakini usiku ndio kwanza anapigiwa simu hovyo na watu wasioeleweka siku ukiachwa unasema umerogwa,kijana ameoa hata mwaka hana tayari unamkuta anasimama na vibinti na wasichana ambao hawajaolewa bado ,VIJANA KWA WANAWAKE WAMEPOFUKA MACHO WANAONA VITU VISIVYO ONEKANA kuna wanawake wanalewa kwa kigezo kimoja tu na hicho ni pesa ,ukiwa na pesa basi hata ukitangaza ndoa usiku wa maneno utapata mke usiku huo huo maana kuna watu wanakesha kama popo kutafuta wanawake na ukishampata siku pesa zikiisha basi anaondoka maana alichokupendea ni pesa na siyo vinginevyo .

Lakini hili limeonekana kuwa tofauti sana Afrika kwanza ndoa nyingi hufungwa kienyeji enyeji pasipo kufuata mpangilio unavyotaka ,mtu anavuta bangi ni mlevi naye kaoa tayari ,mtu haeleweki na kazi hana tayari unakuta naye ana mke ndani ,watu wanaoana hovyo hovyo kitu ambacho kinakuja kuwaletea shida na mushikeli baadae suala la kuwa na mke au mme siyo suala la kuparamiaa paramia ovyo kama kifurushi cha chuo lazima ujipange kiakili na kiuchumi pia ,kabla hujaolewa hakikisha umekomaa kisawa sawa na unaweza kuhandle hisia zako na kutatua matatizo yako mwenyewe kwanza pasipo kumpelekea balozi au baba paroko ,UBISHI ,UBISHOO,KIBURI NA USHINDANI USIOKUWA NA MAANA NI SUMU KATIKA NDOA,kama mlikubaliana kupenda na kulindana kwani mnaanza tena kushindana katika ndoa kama nyinyi ni kitu kimoja ,kuna familia zingine hujui mke ni nani baba ni nani maana kila mtu anaongea la kwake ,kwenye ndoa kila siku maneno utafikiri watangazaji heshima hakuna wanapigazana kelele utafikiri waganga wa kienyeji KWENYE NDOA MAELEWANO YA MUHIMU BILA HIVYO HAKUNA NDOA ,kuoa au kuolewa ni jambo la heshima lakini unapotaka kuolewa tafakari kwa kina maana ndoa siyo sehemu ya kufanyia majaribio .

Ndoa nyingi zinavunjika lakini zingine hazina sababu za msingi utasikia tu mtu kamuacha mke wake kahamia kwa mwanamke mwingine ,utaona huyu naye kamuache mme wako kaolewa na bosi wake ,kuna wengine wanaachana kwa sababu ya kuvimbiiana kwenye nyumba hajulikana SIMBA DUME NI NANI SIMBA JIKE NI NANI..?Huku piaa utaambiwa nimeachana na mke wangu maana NIMEMFUMANIA na fundi viatu ,ukimuuliza huyu naye atakwambiaa mimi nimeshindwana na baba njorogwe kwa sababu MAISHA MAGUMU, magumu siwezi kuteseka mimi wakati bado binti, swali ni je ni lini maisha yalikuwa marais,yaani sababu nyingi kupita maaelezo lakini sababu nyingi hizi zinavumulika na kurekebishika kabisa na watu wakaendelea kula matunda ya ndoa ,kuna wengine watakwambia mimi nimeachana na mme wangu kwa sababu ana KIBAMIA HANIFIKISHI KILELENI ,hayo ndio maisha ya ndoa yalivyo kama uko kwenye ndoa kuwa makini na ujifunze jinsi ya kucheza na alama za nyakati maana unaweza ukahisi umemaliza kumbe umemalizwa kuwa mbunifu kuwa mjanja ulifunga ndoa mwenyewe bila kulazimishwa na mtu hivyo TAMBUA NDOA HAIJENGWI KWA MANENO BALI HUJENGWA KWA VITENDO.
 
Ehuuuuuu! Walimu wa lugha sijui hawakueleweka zaidi juu ya kufupisha habari.
 
Back
Top Bottom