Now we are getting somewhere. Ni kweli redio haiwezi kuua watu. Lakini inaweza kutumiwa kuchochea mauaji ya watu.
Yale mapanga, mashoka, na visu vilivyotumiwa na Interahamwe kuwaua Watusi ni kazi iliyopangwa zamani. Ilipangwa na nani? That is a million dollar question. Wafaransa waliisapoti serikali ya Wahutu. They share the blame. Yule mama wa Kihutu aliyekuwa Prime Minister aliuawa siku hiyo hiyo. Ni kwa nini? Aliunga mkono upatanishi na RPF. Ni nani aliyepinga mapatano na RPF? Ni jeshi la Kihutu. Nani aliyekuwa amedhibiti uwanja wa ndege? Ni jeshi la Kihutu. Nani alikuwa na more to lose kutokana na mapatano kati ya Habyarimana na RPF? Ni jeshi la Wahutu. Now we are getting somewhere. Nchi za magharibi zimekata misaada kwa Kagame, si kwa sababu ya kutunguliwa kwa ndege ya Habyarimana, lakini kwa sababu Kagame anaunga mkono kundi linaloongozwa na Watusti mashariki mwa Congo, M23.
Mkuu hivi yale mabox yaliyo kuwa yamajaa mapanga mapya kutoka uchina yalikuwa yamenunuliwa kwa madhumuni gani? Hivi kweli hile ilikuwa a true story au adithi za kutunga, kusema ukweli mapanga niliyo yaona kwenye video clip ile sikuamini kama kweli Serikali ya Habyarimana ilikuwa imepanga mauaji before hand - kwa nini wafanye hivyo! Kama shida ilikuwa kuuua watu emass kwa nini wasitumie machine gun, hand granade na explosive charges!!!
Kwani upatanishi na RPF ulikuwa una entail vitu gani ambavyo wahutu walikuwa hawa hafikiani navyo, mbona waziri mkuu alikuwa ni mwana mama Mtutsi, kwani ni kitu gani kingebadilika drastically katika utawala wa Habyarimana mpaka kiwafanye Wahutu wa-revolt against Raisi wa kabila lao - it doesn't add UP mkuu.
Ni kweli sehemu nyingi zilikuwa zinadhibitiwa na majeshi ya Habyarimna lakini na majeshi yenu yalikuwa yamekwisha inflitrate mji mzima, mlicho kuwa mna subiri ni tukio la ghafla ambalo lingewafanya jeshi la Habyarimana liamaki liwe in disarry ili nyinyi muweze kutimiza malengo yenu, hamkujali maisha ya Watutsi wenzenu ambao walikuwa Serikalini na vijijini
(I am sorry kusema hilo) Si amini kama mlikuwa na nia thabiti ya kuwa na Serikali ya mseto na Habyarimana - ingekuwa vurugu tupu.
Nyinyi watu si rahisi kupatana, tangu nikiwa mtoto mdogo tulikuwa tunapokea wakimbizi kutoka Rwanda, tunaishi nao kama ndugu, wengine wali ishi kwetu zaidi ya miaka 45+ wengi wao walikuwa wanazunguma kilugha chetu wala usingejuwa kama ni Wanyarwanda and besides we gotta lot in common, walipo kuwa wanatusimulia atrocities walizo wahi kukumbana nazo nchini mwao tulikasirika sana, ndio maana wakati mwingine unaniona nakuwa mkali sana linapokuja suala la RWANDA.
Nyie wote are equally guilty - mtu akiwasikiliza hawezi kujuwa nani anasema ukweli nani ni Muongo, mpunguze tabia ya kuwakumbusha wenzenu kwamba
"Ujuhi mimi Mtutsi" hii ina set a very bad precedence, kwa nini umfanye mwenzako aji-feel inferior! Bila ku-address mind set zenu hamtaweza kukaa kwa amani kwa muda mrefu, we fikilia nchi yenu ina makabila matatu tu:Watutsi, Wahutu na Batwa mnashindwa kuelewana je mgekuwa makabila 120+ kama Tanzania si ndio ingekuwa balaa! mkiona vipi basi unganeni na Tanzania iwe nchi moja kama ilivyo kuwa wakati wa enzi za Wajerumani, oh yes msabazwe Tanzania nzima na Watanzania wengine wapelekwe Rwanda hiyo ndio ingekuwa final solution.
La mwisho ni kweli saction kutoka nchi za magharibi linatokana na matatizo ya Congo specifically M-23, lakini usije ukajidanganya kwamba suala ya kutunguliwa ndege ya Habyarimana will go away any time soon. Tunaitakia mema RWANDA, nimalizie kwa kusema msipende pende kupigana vita, vita havilipi.