Who is Dr Haji Mponda? CV please...

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Jamaa yuko Live ITV- dakika 45, nilikuwa namheshimu lakini, anaonekana hayuko 'oriented' kabisa na mazingira na kila kitu! Elimu yake ikoje huyu daktari??? CV Please!
 
Huyu ni Doctor of Phylosophy, alisoma sociology, then amefanya kazi na Ifakara Health Insitute mambo ya Reseach na kusoma masters ya Health Policy huko London School of Tropical Medicine. Kifupi he is not a Medical Doctor
 
Eti hajui kama Muhimbili Intern Drs wamefukuzwa, pia hajui kama Intern Drs ni members wa MAT. Ina maana hata haelewi organisation iliyokuwa chini ya wizara yake inafanya nini! be serious Dr. Mponda! take ur tyme uchungulie hapa bac.. www.mat-tz.org/members.html
 
Eti hajui kama Muhimbili Intern Drs wamefukuzwa, pia hajui kama Intern Drs ni members wa MAT. Ina maana hata haelewi organisation iliyokuwa chini ya wizara yake inafanya nini! be serious Dr. Mponda! take ur tyme uchungulie hapa bac.. www.mat-tz.org/members.html


Kwa waziri yeyote kutojua nini (hasa matukio makubwa) kinaendelea ndani ya moja ya idara zake ni udhaifu usiokubalika. Muhimbili haiko mbali kabisa toka kwenye office za Wizara ya Afya. Sasa kama Dr Mponda (waziri wa afya) hana habari za intern doctors kugoma atajuaje mambo yanayoendelea huko mikoani? Ni huyu huyu Waziri alieyeleta kigugumizi kuhusu vipimo vya HIV sasa anatangaza waziwazi kuwa hajui nini kinaendelea kwenye idara nyeti kama hospitali kuu ya taifa!

Au pengine anatukumbusha kuwa hospitali kuu imehamia India hivyo yanatokea hapa Dar hayamhusu? Tumeona wakubwa wakiugua wanakimbizwa India, walalahoi wataenda wapi?

Kama kuna jambo la kuomba msamaha ni basi ni hili la waziri kutojua nini kinachoendelea wizarani kwake. Kwa maneno mengine hafai.
 
huyu ni waziri aliyewekwa kuhakikisha sherehe za miaka hamsini ya uhuru zinafana pale MoHSW.
 
sijajua kama mponda ni dk wa phd au wa kutibu, ila ni kweli hayuko oriented na mazingira yetu. Wakati fulani bungeni akitetea bajeti yake alikosea mara zote alipokuwa akitamka CCBRT na kusema CCRBT. Ina maana haijui hii hospitali?
 
Back
Top Bottom