kwa kweli hii nihali mbaya sana na inakatisha tamaa kwa wana taaluma wetu ambao wamekuwa wanadai haki yao kwa muda mrefu,vitisho,ugaidi na mambo kama haya ka ma yaliyomkuta Ulimboka ni vitendo visivyo kubalika na kamwe watanzania wazalendo wasikubali kubariki matendo haya,watu wanadai haki zao wanahatarishwa maisha yao wakati kuna watu wamekaa tu wanafanya michongo mabilioni y afedha yanaingia tu kwenye akaunti zao halafu ndiyo hao hao wanasema serikali haina fedha za kuwalipa madaktari,billioni 300 watu wanajichotea kirahisi,hazina inatoa 3.5bilions ikiwa ni 1.5bilion extra(fedha iliyochakachuliwa) katika kipindi cha siku 7 halafu bado serikali inasema haina fedha,na kudiriki kutaka kuondoa maisha ya daktari kwa kusimamia na kudai haki za wanataaluma hao,mimi kwa kweli nasema sasa hivi hata hao madaktari BINGWA wanapaswa kuanza mgomo nao,kwa tukio lililotokea daktari atakayeendelea kufanya kazi ni kama vile anaunga mkono kitendo alichofanyiwa Ulimboka,Mungu amponye kijana wa watu!