Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

mwachine mzee watu apumzike. tujaribu kuendeleza utamaduni wetu wa kutokuwachonoa viongozi wakuu yaani state leaders wanapomaliza muda wao,hii ndio ya Tanzania iliyojijengea tangu zamani.

thx


Ni yeye mwenyewe anayelikoroga!

Awe makini na muwazi anapotaja mapungufu ya awamu zilizopita lakini zaidi ya awamu ya sasa ili nayo ijirekebishe mapema kutuondolea muendelezo wa lawama kwa kila Rais anayemaliza muda wake.

Mzee Mwinyi bado ni kiongozi wa juu ndani ya chama tawala (CC, NEC) hivyo anayo nafasi ya kukemea akasikilizwa, akawasemea wanachama wanyonge na wananchi. Hafanyi hivyo!!

Hotuba zake zina taswira ya kuwalinda watawala na si wananchi.

Niambie iweje Mwinyi akiwa ndani ya CC ya CCM amsifie JK pasipo kumshauri au kushauri chama kuchukua hatua kwa Kiongozi aliyethibitika dhahiri kukiuka maadiri ya uongozi walau ya kuficha ukweli wa mali anazomiliki na kuzificha nje ya nchi? Yapo yasiyostahili kusubiri SFO achiria mbali TAKUKURU!!!
Yeye yoko upande gani???

 
Baada ya siasa ya ujamaa kupindwa , kupekechwa na hatimaye kupigwa bonge la "ruksa" hakuna mwana siasa aliyekuja na falsafa mbadala ya kuwaendeleza watanzania.Viongozi wote wana reflections za ujamaa na wanapembua hapa na pale kuchota kile wanachokihitaji na kuacha kile wasichokitaka.
Siasa ndo ilivyo lakini, kwa msisititizo, it is far easier to criticise than put forward a workable policy.
Mzee Mwinyi akiwa bado hai hili ni jukumu lake.
Ujamaa wa Nyerere uligusa kila fani ya maisha:Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,Siasa ni Kilimo,Elimu ya Kujitegemea nk.
Mimi sitaki kurudi huko kwenye enzi ya hiyo siasa ambayo kimsingi imepitwa na wakati lakini je hivi sasa hatuna "philosophical thinkers" wenye uwezo wa kuonyesha dira ya kule tunakoelekea?
 
Anayo ardhi kubwa sana kule Kingoruhira, Morogoro. Aliipata akiwa Ikuru,hivyo aliipata kwa kutumia kofia ya jumba hilo. Ni ardhi kubwa isiyotumika ambayo wangepewa wawekezaji ikalimwa na kutatua tatizo la njaa nchini.


Mwinyi hakuimiliki ardhi akiwa ikulu alikuwa na mashamba yake ambayo umiliki wake ulilingana na kipato chake tofauti na Lowasa na Mkapa.
 
kwa hiyo unataka kusema nyerere alifanya makosa kutunga vitabu akiwa ikulu. Kwa sababu mpaka sasa anaendelea kulipwa kama mtunzi.

Na vitabu vingine vilitumika kwa sababu yeye alikuwa ni rais tu lakini bila cheo hicho hakuna ambaye angenunua.

....duh!!!!
 
Mwinyi!! Mwinyi kwelikweli.mtaalamu wa kiswahili naam mwalimu wa Kiswahili.
Katoa mpya; KUNGUNI KUPEKECHA MTI.
mtoto wa mkulima nimekulia kwenye kunguni, nikasoma shule zenye kunguni.sijao kunguni kuwa ubavu wa kupekeche hata hizo kamba za kitanda achilia mbali tendegu. walitunyonya sana, tukapata maarifa ya kupambana nao.
Nakwepa kudandia gari kwa mbele, n'sije n'kaumia.Kwani babu kazungumza kisichokuwepo kama vile kipo ili waliopo waamini kilikuwepo."Kunguni wa babu" walilifukamia gogo la mti hou, wakaanza kulipekecha wakati wao wanaubavu wa kulifyonza/kulinyonya.
Ujamaa ulipata nguvu zaidi kwa msaada wa Azimio la Arusha. "Kunguni wa babu" wakakutana Zenj-bar, babu akiwemo.Kunguni "wakalipekecha" Azimio la Arusha na vumbi la Azimio la Zanz... likawa ndiyo matokeo.gogo la ujamaa puu!! Mze kifimbo akashikwa na simanzi hata akasema"inakubidi uwe na akili za mwendawazimu kulitetea Azimio la Arusha".
Ni kama ujamaa umekufa lakini kwenye KATIBA UMO. Ni kama vile ujamaa upo lakini viongozi wanamiliki NJIA KUU ZA UCHUMI.
ninaendelea kutafakari; kunguni kupekecha mti.Kisichokuwepo kama kipo ili kionekane kilikuwepo na sasa hakipo.
 
come to think of it-hivi kunguni anauwezo wa kupekecha mti! Pengine Babu alimaanisha mdudu mwingine!Hata hivyo tunamuelewa anamaanisha kunguni-mtu.
 
LOL!...kuna ufisadi kweli ambao mtu hafaidiki kwa chochote.... ha ha ha ha!

Yesterday I was bored and in a pugilistic mood. So I picked a fight with you man.
. I expected irrational reactions, but you took it very easy.

Tukirudi kwenye mada. Mwinyi is a very shrewd politician. Anaelewa kabisa all politics is local. Alikuwa anazungumza kwenye maadhimisho ya CCM na alichotakiwa ni kutoa mafanikio ya chama chao. Hivyo katika shughuli kama hile amefanya maigizo tu.

Miezi michache iliyopita aliongea na waandishi wa habari na alisema kuwa Ujamaa ulikuwa hauwezekani na ilikuwa taabu kuupindisha ujamaa wakati Mwalimu akiwa hai.

Mwinyi hakuamini ujamaa au Azimio la Arusha. Na alishasema kuwa kila binadamu ana matakwa yake na kuwafanya binadamu kupata sawa ni kitu kisichowezekana kwa sababu binadamu ameumbwa na matamanio yake.

CCM inaboronga lakini wana expertise katika Damage Control programs. Hivyo viongozi wa juu wa CCM wanapo-control damage, watu mnawataka waseme vile mnavyotaka nyinyi. Sasa hiyo sio siasa.
 
Suala si kuwa kamili or 100% right suala ni kuangalia position za Mwalimu katika maamuzi yake si makosa ni maamuzi ya makusudi kabisa kuanzia kwenye uhuru,Biafra,Azimio la Arusha,Umoja wa Africa,Uhujumu uchumi,Mauaji ya Zanzibar 1964,Vita ya Kagera,Uteuzi wa Mkapa,Kifo cha Sokoine n.k.Ukiachilia mbali civil war za nchi ngapi za Africa ambazo Mwalimu ni architect,then everybody knows how inteligent he was and you still call this mistake ? May be we need a therapist to open our eyes because we can not help ourselves.

SAHIBA.
 

Bado tunarudi kwenye dira , inaelekea Mheshimiwa Zakumi una propose kuwa kwa sasa hivi hakuna dira yoyote isipokuwa hisia za mtu au watu na wakiboronga kutokana na matatizo ya kibinadamu kunachofuata ni "Damage Control" na watu wanasonga mbele kusiko julikana?
Au kwa kweli siasa sasa hivi ni funika funika bora liende.
 
Kwa kweli mzee Mwinyi na Spika Wameongea mambo yenye mantiki na tija kwa taifa hili.

huu in ukomavu wa siaisa za vyama vingi na demokrasia nchini, hongera chama tawala ccm kWA KUWEKA UWANJA mpana kwa kila mtu kuvinjari kivyake.

Tatizo ni kuwa huko CCM kwenyewe kuna mambo hayo hayo yanayoonekana kwa wapinzani. Hivyo hatuoni mtafaruku na matusi kati ya viongozi wa CCM?
Namkubali Mzee ruksa kuwa ametowa mawazo yake kutoka moyoni kwani alishakuwa Rais wa wote lakini kauli ya Spika inanitia wasi wasi kwani si kweli kuwa CCM inahisi kuwepo kwa wapinzani ni changamoto bali ni tishio kwao. Matendo ya chama hicho kwa wapinzani ni ushahidi tosha wa ninayoyasema. Pengine Spika anafuwa nguo ya Ijumaa leo jumatano wala hangojei Alhamis kama alivyoshauri Mzee ruksa kuwa nguo ya Ijumaa ifuliwe Alhamis.
 

Una hakika na unachokieleza? Hivyo Mrema angekuwa na ubavu gani wa kumkabili mke wa Rais na kumpekuwa wakati ule? Habari nyengine zinapingana na real situations na ndio maana kuna kitu miracle. Pengine hii ilikuwa moja kati ya hizo miracles. Nitaendelea kuamini kuwa una lengo la kumchafulia mtu jina HADI PALE utakaponithibitishia kuwa usemayo ni kweli.
 

Nakumbuka kusoma sehemu inayosema kuwa JK anachofanya sasa ni kurekebisha maovu yaliyofanywa kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tau. Kwangu miye ningehisi kuwa hiyo ni kauli ya kukubali makosa, sijui wewe unaonaje?
 

Pengine wangekwenda kummuliza Aboud Jumbe vipi aliiweza sera ya kubadilisha mawaziri ovyo ovyo.
 

Inawezekana kuwa sisi tulio nje ya madaraka tunaona utendaji wa Mawaziri kuwa ni kushindwa lakini pengine hayo ndio maelekezo na maagizo (ilani ) ya hao tuliowachaguwa kutuongoza. Kwa desturi hakuna kiongozi yoyote aliye tayari kumuonea haya kiongozi anaemuhatarishia uongozi wake. Aidha Chama kinachowapa nafasi pia hakiko tayari kuona kuwa masilahi yake yanahatarishwa na kwa hilo CCm ingekwishawachukulia hatuwa Mawaziri tunaowaona wanaboronga kama walivyochokuliwa hatuwa Jumbe, Seif, Hamad Rashid, Mrema na kadhalika. Ukishalitambuwa hilo basi ni rahisi kufikia uamuzi kuwa hicho wanachokifanya ndicho wenyewe CCM wamesimama nacho.
Chukulia mfano wa mtu kama Rostam Aziz na anavyoonekana na jamii lakini tunasikia amefadhili ule mkutano wa Vijana kule Zanzibar.
Hakuna haja ya kumlaumu JK kwa kuwakumbatia Mawaziri walioboronga kwani nafikiri hatukuikubali na wala hatukubali sera za CCM. Ni wale tu waliokubali sera zao ndio wanaoweza kuamuwa kama wakifanyacho Mawaziri ni sawa au la lakini kwa mimi nahisi kwa mfano Waziri Masha kuingilia tenda kutakakomletea commission atakayoweza kuitumia kwa kuikampenia CCM 2010 si kosa kwa CCM.
 

Susuviri:

Hapa unaboronga. Kutunga kitabu ukiwa ndani ya ofisi tayari unaingiza interests zako katika shughuli za serikali.

Viongozi uliotaja wewe hapo juu wametunga vitabu. Guess what? Wametunga vitabu baada ya kuachia ngazi.

Mao Tse Tung alitunga vitabu wakati akiwa Chairman lakini mapato yanaingia kwa taifa na sio familia yake.

Ukifanya ufumbuzi katika kazi ya Phd au Masters, mmiliki ni shule na sio wewe.

Sasa kama Nyerere alitunga kitabu akiwa ofisini na kwa kupata access iliyotokana na cheo chake, mapato ya utunzi wake, hotuba zake na vinginevyo ni mali ya taifa (period).
 
Pengine wangekwenda kummuliza Aboud Jumbe vipi aliiweza sera ya kubadilisha mawaziri ovyo ovyo.


Kumbuka Aboud Jumbe alitafunwa na Seif Sharif(kibaraka wa Nyerere wakati ule) kwa uroho wa madaraka alitegemea kuwa Rais,Sasa serikali itakwenda vipi wakati waziri kiongozi wako is there to destroy you.

SAHIBA.
 

Lole Gwakisa:

Nchi za kiAfrika zilipoteza mabilioni ya pesa, watu na muda wa miaka mingi toka kupata uhuru kwa kufuata dira zisizowezekana, mojawapo zikiwemo african socialism za Nyerere, Nkrumah, Senghor, Sekou Toure n,k

Dira bila kuwa na expertise ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hivyo mimi sio mshabiki wa siasa za dira. Nina sababu muhimu lakini kuzielezea kwake itabidi niumize kichwa kidogo kitu ambacho siko tayari kukifanya kwa sasa.

Tukirudi kwenye mada wanasema: All politics is local. Kwa maoni yangu sioni ubaya wa aliyosema Mwinyi kwa sababu hotuba yake aliitoa kwa hard core CCM supporters wakiwa wana-sherehekea miaka 32 ya kuanzishwa kwa chama chao.

Hii ilikuwa ni BIRTHDAY PARTY. Unapokuwa kwenye BIRTHDAY PARTY, mnakumbushana Good Old Days kama zipo. Na kama hazipo basi angalau selective nostalgia.

Sasa watu wanataka kwenye BIRTHDAY PARTY, babu aende kuzungumza mambo ya mafisadi. Sasa kazi ya upinzani hiko wapi?
 

Mheshimiwa Zakumi, bila dira ya kule tuendako, kwa hakika hata ile hatua tupigazo ni za kuzunguka pale tulipo.
This is a very serious issue, na sikubaliani kabisa kuwa inabidi uwe msomi wa kupidukia ndio upate dira.Ndio wasomi watasaidia kujaza details za utekelezaji wa dira hiyo.
Kwa mfano,mtu unapooa unategemea watu muwe wengi kenye nyumba hivyo basi, mzee wa nyumba ni jukumu lake kutengeneza dira ya kukidhi matakwa ya kuwa baada ya miaka kadhaa mtakapopata watoto, inabidi kufanya kazi kwa bidii au biashara ili kumudu maisha na kusomesha watoto na pengine ingalau ziada ya maendeleo ya baadaye.Huu ni mfano mdogo tu tena wa maisha ya kila siku.
Dira ni mpango tu wa kimaisha na kisiasa yenye details nyingi sana,.
Kinachohitajika ni kuwa na mpango na kuwa committed kwa mpango hua wa kimaisha na kisiasa.Hili ndo linakosekana.
Kwa kukosa hilo kila kiongozi ana mipango yake ya kibinafsi, anayetaka kutawala tu haya, anyetaka kuiba/kufisadi haya, miiko ya kimaisha/kiutawala hakuna.
Hivi tutapata kigugumizi kikubwa sana kudhibiti matukio yasiyo tarajiwa katika jamii.Kwa mfano siyo bure kuwa:
mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanaongezeka, wakati wafugaji wanaruhusiwa kuzurura na mifugo yao nchi nzima,
-kuna viongozi wanajitwalia mali ya umma/au kutumia madaraka vibaya kupindukia bila uongozi kustukia jambo hili mpaka wananchi wanapoanza kulalama
-mwongozo wa kiuchumi/viwanda kutokuwa na strategy zinazolenga maendeleo ya wananchi,

The list is endless!

Mheshimiwa Zakumi,birthday celebrations for its sake haileti maana sana bila kujua kule utakako na kule uelekeako , hasa kwa chama cha siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…