Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

what about "DUCHE" of Kim il sung (DPRK)?, naona kama yote alikopi huko "ujamaa na kujitegemea".
 
Naam, nimeiandika mwenyewe. Sina tatizo na wasifu wangu kujulikana. Kama kuna mtu anataka nakala ya hiyo mada anipe anuani ya barua pepe yake nami nitamtumia mara moja. Katiba yetu, katika Ibara ya 18, inasema kila mtu ana haki ya kupata taarifa muhimu kama hizi zinazohusu maendeleo ya jamii yetu.
bevic@rocketmail.com
 
Kuhusu ujamaa wa Nyerere kufail,ni kwa kuwa hakukuwa na base?Nyerere haku adopt Ujamaa wa kidemokrasia japo focus yake ilikuwa kwa nia njema sana.

Hata China awali ilidumaa kiuchumi kutokana na sera za Rais Mao ,Mao aliamini sana Ujamaa wa Kikomunisti.

Waziri mkuu wake,Zioping alipojaribu kumkosoa kuhusu aina ya Ujamaa uliotakiwa kuwa ulipaswa kuwa wa Kidemokrasia unaoruhusu ushirikishwaji wa wananchi katika kufanya maamuzi ya rasilimali zao.

Zioping aliishia kuwekwa Jela ,alifungwa Mara tatu akipigania ujamaa wa Kidemokrasia unaoruhu uwekezaji.

Baada ya Rais Mao kurariki Dunia ,China ilitafuta mtu anaeweza kuiondoa China kwenye Mkwamo,wakakubaliana kwenda kumpigia Magoti Zioping,alikuwa Kijiji akiwa fundi wa Matrekta.

Akarejea madarakani na kufanya mabadiliko makubwa yaliyofanya China kuruhusu Makampuni ya Kigeni kuanza kuwekeza China,ni kwa msingi huo China ikajikwamua kiuchumi na kuwa China ya sasa tunayoiheshimu...
 
Kwa tafsiri ya haraka tulitakiwa tumtafute Kambona na kumpigia magoti. Na sio kumuita haini. Kama ilivyokuwa miaka hiyo ya kawawa mfuata upepo. Yote kwa yote ni muda muafaka sasa kufanya mapinduzi ya kifikra kisha tutambue kuwa Tanzania ni yetu sote na sio ya wanabagamoyo kama ilivyo sasa.
 
Kwa tafsiri ya haraka tulitakiwa tumtafute Kambona na kumpigia magoti. Na sio kumuita haini. Kama ilivyokuwa miaka hiyo ya kawawa mfuata upepo. Yote kwa yote ni muda muafaka sasa kufanya mapinduzi ya kifikra kisha tutambue kuwa Tanzania ni yetu sote na sio ya wanabagamoyo kama ilivyo sasa.

neno kubwa hilo........kuna laana zipo tu na watanzania na vizazi vyao; kuna vizazi viliingizwa chaka na kudanganywa sana; viliimba mchakamchaka , vilitukana na kulaani ili hali walikuwa wamedanganywa

aibu!
 
Mimi siko UK wala USA, nipo hapa URT. Karibu sana tujenge nchi ya watu ambao Mwalimu Nyerere aliwatabarukia vitabu vyake vya Ujamaa. Sasa tunaanza upya baada ya SAPs na PRSP kushindwa kazi kwa miaka 28 ambayo ni miaka mingi zaidi ya miaka 10 tuliyotekeleza Azimio la Arusha la Ujamaa na Kujitegemea. Tunaanza kwa kurudisha Mwongozo. Hii itasaidia watumishi wa umma wasichanganye utumishi na biashara binafsi kama walivyochanganya kina Richmonduli. Hivi jiulize inakuwaje waziri awe na biashara ya ndege alafu akipoteza tu uwaziri eti hiyo biashara inafilisikia!Mwongozo utahakikisha kuwa kamwe kodi zetu hazibeiliauti mafisadi!Kwa jasho lao watakula!Ujamaa, kama ulivyo Uhuru, ni kazi!Na hata misahafu inasema asiyefanya kazi na asile!Haisemi liwa ule!

Almost 7 seven years now. Tell me how things are moving down there?
 
Waungwana,

Ni nani na ni misingi gani ya utashi iliyojijenga kwenye akili za Julius Kambarage wa Nyerere kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na hata Azimio la Arusha?

Wengi tunadhania kuwa ni safari yake ya China 1966. Wengine wanadai ni wale ma-Labor na Socialist wa Uingereza.

Tunajua kuwa tumeangalia sana Ujamaa wetu na Azimio kwa mkao wa Great Leap Forward na Cultural Revolution za China ya Mao na Leninism/Stalinism ya Command Economy, New Economic Policy, Collective farming, na hata matunda ya Bolshevik revolution na sera kama Prodrazvyorstka!

Tukija huku kwetu Afrika tunadai kuna Ujamaa wa Kiafrika, Pan Africanism na mengine mengi.

Lakini bado nafikiri ni kitendawili kwetu kuwa ni ushawishi gani na kwa maono gani Nyerere alikaa chini na kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha?

Nikirudia Historia na kuangalia kinachotokea Marekani kiuchumi mwaka huu na nyakati hizi, narudi kujiuliza, falsafa za kiuchumi na kujenga jamii za Marekani zilimkosha Mwalimu Nyerere hasa kuangalia Historia ya great depression?

Je FDR (Franklin Delano Roosevelt) na New Deal yake, Fransiscans/Jesuit philosophy na hata Keynesian Policies zilimbadilisha vipi huyu Mkulu wetu? Planned Economy za National Recovery Administration wakati wa Great Depression ya Marekani na hata Public Works ya Nazi German vilikuwa na nafasi gani?Je alichungulia Front Populaire ya Leon Blum wa Ufaransa na kudonoa mambo kadhaa?

Je kujinasua kwa Marekani baada ya Uhuru wake kutoka Uingereza na kujijenga kama taifa linalojitegemea na si kutegemea falme ya Uingereza na kiburi cha Kimarekani pia kilichangia kumjenga Nyerere kuwa na kiburi cha masikini jeuri?

Twajua Julius Nyerere alikuwa mwana historia mzuri hata ukiangalia na kumpima kutafsiri kwake kwa Julius Kaisari na Mfanyabiashara wa Venisi kazi za William Shakespear zinaonyesha ni influence gani ya fasihi, historia na falsafa alikuwa nayo.


Je Keynes alikuwa na infuence gani kwa Nyerere ambaye alisoma fasihi, historia , uchumi na falsafa alipokuwa Makerere na hata Edinburgh?

What about Wealth of nations, je Nyerere alifanya modification ya principles za Adam Smith akipewa baraka na Labor Party ya Uingereza chini ya ushawishi wa Mama Joy Wickens? Maana ukiangalia Azimio la Arusha, pamoja na kuuzwa kuwa linapiga vita Ubepari, in fact linaruhusu ubepari na mfumo wa Kibepari kwa kiasi fulani hasa linaposema kuwa Viongozi wasiwe na zaidi ya hisa katika makampuni mawili!

Je Plato, Aristotle, Socrates, Ghandi na hata Yesu au Mtume Mohamed wali-play part gani kum-influence Nyerere?

Je alisoma sana Das Kapital na Communist Manifesto ya Karl Marx, akamchanganya Trosky na Friederich Engels?

Je sisi kama Taifa kwa kumfuata Kiongozi wetu tulikuwa ni majaribio (experiment) ambayo mataifa makubwa yalikaa kando kuangalia huyu mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Afrika akikoroga na kuunganisha mifumo ya kiuchumi ya Ubepari, Ukabaila, Ukomunisti na Ujamaa na kuunda Ujamaa wa Kiafrika ambao ulilenga kwenye kujitegema na hata kuzaa Azimio la Arusha kubana tabaka la viongozi na kuhamasisha umiliki wa mali kwa umma na si watu binafsi?

Tumeegemea sana kusema tumeunda Ujamaa wetu kutokana na ziara yake ya China na kuharibika kwa uhusiano wetu na Uingereza kulikotokea kipindi hicho hicho.

Je inawezekana kuwa kiwango kikubwa cha falsafa zake za Ujamaa na Azimio ni mgawanyiko sawa wa influence za magharibi wakati wa depression na mashariki wakati wa uprising na mapinduzi?
Nyerere alikuwa akifuatilia mrengo wa Labor akiwa Uingereza lakini aliye mu influence UJAMAA ni AbdulRahman Babu.
 
Lakini akamtelekeza sana Babu na Hanga. Na kuruhusu wapotezwe na Manyang'au.Inaniudhi sana historia hii
hakuwatelekeza mkuu ila hakuwa na jinsi na ndio maana alisema ule ujumbe kama angekuwa na uwezo angekisukuma kisiwa kizima cha Zanzibar mbali huko katika kati ya bahari kwa sababu Km70 ni ndani ya Uzio wetu wa kiusalama (200 Km) huwezi kuwakimbia. Ujue ilikuwa kazi kubwa kuwapatanisha ASP na watu wenye Ukomunist ama asili ya Kiasia Unguja.

Kwao baharia Karume alikuwa hafai kuwa rais (Elimu) lakini upande wa pili Karume naye alikuwa mtoto wa kihuni, alijua ni swala la muda tu Umma Party na wasomi watamshusha ikabidi aonyeshe kifua na makucha yake. Kikatiba Zanzibar walikuwa na mahakama zao, Nyerere asingeweza kupindua maana mapinduzi mengine ya Zanzibar ndio yangekuwa Mapinduzi ya Muungano. Kuna tuhuma za kijasusi mitaani enzi hizo zilisema Nassoro Moyo ambaye alikuwa kundi nao ndiye alomtonya Karume sijui kama kuna Ukweli..
 
Back
Top Bottom