WHO: Hakuna ugonjwa wa Zika Tanzania

WHO: Hakuna ugonjwa wa Zika Tanzania

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa zika Tanzania na hakujawahi patikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.

Hayo yamesemwa leo (Jumamosi) na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.

"WHO inafanya kazi na wizara ya afya kufatilia taarifa za magonjwa unaofanyika kila siku katika maeneo yote ya afya, na taarifa huletwa wizarani kisha tunashirikishwa ili kutoa katika tovuti yetu, nachoweza kusema hatujapata taarifa za magonjwa ambazo zinazoonyesha dalili za mgonjwa yoyote mwenye zika Tanzania," amesema Dk Saguti.

Pia, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya ina mfumo maalum wa kupata taarifa za magonjwa na hakuna taarifa iliyoonyesha uwepo wa ugonjwa wa zika.

"Hakuna mgonjwa yoyote wa Zika Tanzania…narudia mara ya pili hakuna mgonjwa wa zika Tanzania," amesema Dk Kambi.

16-2015.jpg
 
Ukawa na wapinzani wa serikali wataikataa taarifa hii sababu ya wanayoyawaza wao.. Ila taarifa ya Mwele ingekua imesema hakuna Zika, alafu wakaja, who wakasema ipo ukawa wangeunga mkono hii ya who.. Wanapenda kusikia taarifa mbaya tu katika Taifa
 
Yaani huyu wa WHO anasema hivi: Tanzania hakuna ugonjwa wa Zika kwa sababu hakuna mtoto aliyezaliwa na dalili hizo. Kwa maneno mengine kipimo cha kuwepo Zika ni kuzaliwa mtoto mwenye dalili za Zika na wala sio kutumia njia nyingine kubaini ugonjwa huo. Je, WHO wamepitia utafiti wa NIMR tayari na kukuta kuwa ule utafiti ulikuwa ni wa kutengeneza?
 
Haya mambo watu hawakaurupukii! Watafuta Kick walishapiga kelele sana mpaka makoo yamewakauka.
 
Ukawa na wapinzani wa serikali wataikataa taarifa hii sababu ya wanayoyawaza wao.. Ila taarifa ya Mwele ingekua imesema hakuna Zika, alafu wakaja, who wakasema ipo ukawa wangeunga mkono hii ya who.. Wanapenda kusikia taarifa mbaya tu katika Taifa
Ndivyo livyo.
 
WHO: Hakuna ugonjwa wa Zika Tanzania

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa Tanzania na hakujawahi patikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.

Hayo yamesemwa leo (Jumamosi) na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa Tanzania na hakujawahi patikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.
mwananchi.co.tz
Kwa hiyo utumbuzi alioufanya Mh. Rais ni halali?!
 
Back
Top Bottom