'Who created God' is an Illogical Question!

Nimekuambia hivi, sasa hivi hapa naandika. Katika framework ya JF.

Ninavyoandika hapa, sasa hivi, nina imani.

Imani yangu ni kuwa utasoma ninachoandika.

Imani yangu hii ya sasa inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.

Ukijibu post yangu kwa kuni quote, nitathibitisha kwamba nilichoamini kwamba utasoma kilikuwa sahihi.

Baada ya kujibu, unachothibitisha ni kwamba imani yangu ilikuwa sahihi.

Baada ya kujibu sitaamini tena kwamba umesoma, nitajua.Kwa sababu utakuwa umethibitisha kwa kunijibu.

Kuna kuamini na kukubali. Maneno haya yasitumiwe interchangeably.
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Sasa akishaweza kuthibitisha kuwa mungu yupo,halafu aendelee kuamini uwepo wa mungu au inakuaje?

Maana umesema ukishathibitisha huwezi tena kuamini.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Unafikir kumfagilia Mungu hivyo ndio kwenda peponi?? Unaweza ukampinga na ukaenda peponi pia... matendo ya mtu ndio kipimo... huenda nikawa naswali, huenda nikao kwa taratibu za kidini... but nikubaliane na kila ninaloambiwa. Ndio maana kwa ulimwengu wa sasa na ule uliopita zama hizo kuna tofauti kubwa mno...(kizazi cha jua linazunguka dunia). Vile namfikira babu yangu ambae alikuwa na jina la asili... je, alikuwa kwenye kundi gani.. its obvious ni kundi lile lililokuwa linaamin Mungu yuko juu.. kwenye anga ya blue. Yaani ukitoboa kwenye anga ya blue basi utakuwa kwenye imaya yake... waliamini mpaka wamekufa, wakiwa na hayo na mawazo... kitu ukiwa haikujui lazima utakiwaza tofauti na uhalisia. Mfano ukitajiwa Mungu ni jinsi gani unam-decode... unapata picha ya aina gani?? Physical au non physical... (unaposema yupo hai, tunazungumzia uhai kwa namna ipi kama ya kwetu sisi??) ... or hayupo hai wala mfu.... ni Mungu hawezi kuwa na attributes zangu...( his attributes must be unique...). Nadhani tunazungumzia concept ya Mungu but ikiwa na very big variations... which to me naona no nonsense. (If I can't use my brain kujaji... nitajuaje kwmba sheikh au padri ndie anaesema ukweli???)
 
Ebwana kama ndiyo unataka kuanza yale matusi yako kama siku ile,bora uniambie nitulie tu.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Hakuna tusi hapo.

Mtu ambaye anakubali kitu chenye contradiction ni mjinga.

Wewe unakubali Mungu mwenye contradiction.

Wewe ni mjinga.
 
Sasa akishaweza kuthibitisha kuwa mungu yupo,halafu aendelee kuamini uwepo wa mungu au inakuaje?

Maana umesema ukishathibitisha huwezi tena kuamini.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Sitaki kuamini.

Nataka kujua ukweli.

Kuamini mjinga yeyote anaweza kuamini ujinga wowote bila uchunguzi wowote

Kujua ukweli kunataka uchunguzi wa kina kuhusu mambo specific kwa kutumia mantiki ya hali ya juu.
 
Kiranga ameshajibu swali lako hapa chini mkuu!!
........siyo vizuri mimi kujaza server za JF wakati umeshajibiwa!
Kiranga hapo kazungumzia vitu viwili.

Kazungumzia "kukubali" na akasema huwezi kukubali jambo bila uthibitisho,halafu akazungumzia "kuamini" na akasema unaweza kuamini jambo bila kuthibitisha. Na ndiyo akatoa mfano wake yeye kuwa anaamini jua litachomoza kesho na hajathibitisha.

Hivyo ndiyo nilivyomuelewa je,wewe umeelewa vp?

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Hao ni wachungaji ukiwauliza watakwambia kwa nini.
Sio ukomo wa uelewa kwenye mathematics hauwezi kuwepo maana uko ndani ya limit ye uelewa wa mwanadamu. Na we need to in-cooperate some assumptions to prove the theory. hapa tunazungumzia vitu vingine na kushindwa kuelewa kitu leo haimaanishi hakipo. Ndio maana einstain alikufa bila kujua gravitational waves zipo kiuhalisia lakini leo wanafizikia wameweza kuproof existence of gravitational force. hata wewe yawezekana unalimited knowledge katika unachotafuta sio dhambi bali ni call for higher knowledge sikulaumu
 
Tatizo sio Mimi bali mfuasi wako.

Yeye anataka uthibitishe kwanza kuwa mimi nitaisoma post yako kisha ndiyo uamini kuwa mimi nitaisoma post yako.

Sasa sijui kati yenu nani yupo sahihi?

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna tusi hapo.

Mtu ambaye anakubali kitu chenye contradiction ni mjinga.

Wewe unakubali Mungu mwenye contradiction.

Wewe ni mjinga.
Hakuna niliposema nakubali mungu mwenye contradiction, hizo contradiction s ni wewe ndiye unataka ziwe.

Hivyo siwezi kuwa mjinga mkuu.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo sio Mimi bali mfuasi wako.

Yeye anataka uthibitishe kwanza kuwa mimi nitaisoma post yako kisha ndiyo uamini kuwa mimi nitaisoma post yako.

Sasa sijui kati yenu nani yupo sahihi?

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Kuna imani tofauti, imani isiyothibitishwa inapothibitishwa inaacha kuwa imani, inakuwa ujuzi.

Ulichoambiwa ni kwamba usikubali kitu kama ukweli mpaka ukitibitishe kwanza.

Umeelewa?

Hujathibitisha kwamba Mungu yupo. Huwezi kuthibitisha. Na zaidi, umeelezwa jinsi Mungu wako alivyo na contradiction.

Kwa nini unaendelea kuamini kitu chenye contradiction ambayo huwezi kuiondoa?
 
Sitaki kuamini.

Nataka kujua ukweli.

Kuamini mjinga yeyote anaweza kuamini ujinga wowote bila uchunguzi wowote

Kujua ukweli kunataka uchunguzi wa kina kuhusu mambo specific kwa kutumia mantiki ya hali ya juu.
Nani kwambia uamini?

Nimesema huyo uliyemwambia au kumuuliza kama anaweza kuthibitisha kuwa mungu yupo?endapo ataweza kufanya hivyo hatotakiwa tena kuamini kuwa mungu yupo kwa sababu ukishathibitisha huwezi tena kuamini.

Hapo umenielewa kwanza kabla sijaendelea?

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna niliposema nakubali mungu mwenye contradiction, hizo contradiction s ni wewe ndiye unataka ziwe.

Hivyo siwezi kuwa mjinga mkuu.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Hujaweza kuzikanusha.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

That is a contradiction.
 
Ungekuwa wajuwa maana Yake,wala usingeuliza.
 
Sawa.

Wewe unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…