Who are your parents to you? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who are your parents to you?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Cathode Rays, Nov 13, 2011.

 1. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Habari zenu ndugu zangu,

  Ukweli usiopinga ni kuwa mzazi (bila kujalisha alivyo) ana sehemu kubwa na ya muhimu kwenye maisha yako katika ujumla wake. Nimelia sana leo baada ya kumuona mama mmoja leo nikitoka kanisani akilia msaada kwa kuwa anaumwa na watoto wake walipo hawana habari nae.

  Nilichukua jukumu la kusimamisha safari yangu na kumchukua kumpeleka hospitali kwa matibabu lakini njia nzima akilia kwa kutupwa na watoto wake aliowabeba tumboni mwenyewe na kujinyima kila kitu kwa ajili yao ili wafikie malengo ya maisha.

  Ndugu zangu, ogopa chozi la mzazi......lina weza beba baraka kwako (kama ni kwa furaha) au laana (akilia kwa huzuni)

  A Call: Can you do something for your parents this coming week to make them smile? Inaweza kuwa apology kwa mahali fulani ambapo hukufanya vema au hata kizawadi kidogo cha kurudisha trust yao kwako na kuwafanya wajue yuko mtoto anaejali...........Please do something for your parents this week

  Thanks
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Huyo mzazi aliwafanya nini watoto wake hadi wamemtelekeza.
  Usiangalie upande mmoja na kulaumu.
  Kuna wazazi wanaishi na watoto wao utafikiri hawajawazaa wao.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Tumekusikia na asante kwa ukumbusho wako
   
 4. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Ni kweli Husninyo lakini huyu mama alikuwa anasema watoto wake wamampotea tu na hajui alichowakosea.....

  Lakini pamoja na hayo (kwa mtazamo wangu) hata kama mzazi alikufanyia nini hupaswi kumnrudishia hivyo...retribution haifai bali kusamehe na kumuonesha upendo kwa nafasi yake kama mzazi..

  Kwa mtazamo wangu, hatufanyi kitu kwa wazazi kwa kuwa walitufanyia mema tu, ila kwa kuwa ni mzazi, hilo tu latosha
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna mambo au elimu ya aina mbili;Mosi,unapokuwa kijana ni wakati wako wa kutengeneza maisha yako ya sasa na baadae,uamuzi wa kutafuta watoto ni wako mwenyewe hujawashirikisha watoto,so watafute wale ambao utaweza kuwahudumia ipasavyo,kumbuka hii sio hisani ni lazima uwahudumie na usidai fadhila,wakati unawahudumia kumbuka kujenga future yako na yote hayo yaani watoto na future yafanyike kwa usawa.Pili,wazazi sio wa kudharau,kumbuka bado ana umuhimu kwako sana kwa mambo mengi kama ushauri n.k!Tuwe makini!
   
 6. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Well said Eiyer.........parents are simply PARENTS

  Chozi la huyu mama (forgetting everything behind) lilinifanya kujisikia vibaya njia nzima na kuwaza mengi sana
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  watoto wake wangapi? Ni vipi wapotee wote?
  Kweli sio vizuri kumfanyia maovu mzazi ila mzazi anaweza kuwa chanzo cha yeye kufanyiwa ubaya na watoto aliowazaa mwenyewe. Siwalaumu hao watoto labda kama ningejua A-Z ya kilichotokea.
   
 8. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  By the way it was to read "mtoto wake".....hiki kiluga hiki ndugu

  The issue ni kwamba alikuwa na watoto wa-3 na mkubwa ambae amemuendeleza na anakazi yake sasa anasema yuko Morogoro na wa kati alifariki na amebaki na mdogo na huyu mkubwa kila anapojaribu kutafuta mawasiliano nae hafanikiwi and it is like jamaa kaamua kumpotezea.....Kwa sasa yeye ni mjane na alipoteza mume na mtoto wa pili kwa kufuatana kipindi cha kama miezi miwili hivi.

  Amenipa namba yake huyu kijana na nitamtafuta baadae (nilimpigia simu yake haipatikani) ili tuongee nae kwa undani
   
 9. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Ila Husn hebu turudi upande wa pili, tufanye assumption kwamba mzazi alifanya kitu ambacho huyu mtoto hakukipenda, je hii ni njia sahihi ya kumlipiza kwa kile alichofanya?

  Unadhani mzazi atajisikiaje siku umemwendea na kumwambia "mama/baba nimefutilia yote ya kale na sasa nitawaheshimu kama mzazi/wazazi wangu bila kujalisha tulipotoka"...can you imagine watajisikiaje na wewe mwenyewe utakuwa umetua mzigo kiasi gani? Just thinking
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Cathode u'he finish ur part,it was kumpa msaada bas but all an all ni vyema tukawa makini sana!
   
 11. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  una akili snaa shost ndio mana nakupendaga
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  sio watu wote wanauwezo wa kusamehe waliyotendewa na sio wakosaji wote huweza kuomba msamaha wanapokesea.
  Cathode ukinikosea kosa kubwa na ukachuna hata kama uwe mzazi wangu sitokusamehe na kama nikikusamehe mwenyewe sitokuwa na ukaribu na wewe.
  Nisingependa kuongea mengi hapa ila hongera kwa moyo wa upendo na kwa msaada uliompa huyo mama.
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ndio eiyer. Awe makini maana mjini hapa matapeli nao wengi.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hahaha! Hakunaga kama wewe.
  Samahani cathode tumechakachua kiduchu.
   
 15. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Dada angu kuchakachua kwenye kuumwa....mmmmh, hii ngumu, bora wangekuwa wale wa "ninunulie soda" au "chakula"

  Bahati nzuri ni kwamba nilikaa nae hospital mpaka alipomaliza matibabu ni nikarudi nae hadi nyumbani kwake na "nilivimba bichwa" alivyotoa machozi ya furaha kwa kumjali japo sio mwanae wala hatufahamiani
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mzazi, hasa mama, ambaye hakuna wasiwasi wote kuwa yeye ndie mama, hapaswi kudharauliwa hata kidogo.
  Ile hali tu ya kukubeba miezi tisa (angeweza kukutoa na usije duniani), ni sababu tosha ya kustahiki heshima na mapenzi toka kwako.
  Mama ni mama, hata awe na roho mbaya, hata uone anakuchukia, hata awe mlevi, malaya...na sifa yoyote mbaya utayompachika, bado atabaki kuwa ni mama. Alikupa uhai, alikubeba miezi tisa, akapata uchungu wa kukuzaa, akakulea (mengine kama kukupatia elimu, ni fursa kwake, ikiwa uwezo haukuwa unaruhusu si kosa lake) mpaka umekuwa mkubwa na akili za kujua jema na baya, iweje leo usione mabaya yote yaliyomo ulimwenguni uone ubaya wa mama yako? Inasikitisha na ni aibu.

  Katu hatuwezi kulipa fadhila za mama. Kuna wengine kwa ujinga wao hudai "Nilikutuma unizae?, Nikulipe pesa ngapi kufidia gharama za kunizaa na kunilea? Umenizaa kwa raha zako, umalaya wako. Mimi sistahiki kuwa na mama kama wewe" na ujuba mwengine kama huo.

  Tuwajali wazazi wetu (na walezi wetu pale inapokuwa hivyo). Hawahitaji tuwarejeshee gharama, hawahitaji material properties zetu, bali mapenzi, huruma na heshima. Tumwogope Mungu.
   
 17. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mmesamehewa ili msichakachue zaidi maana kuna watu hili linawahusu, mtu anakata mamiezi hata kuulizia wazazi wake wanaendeleaje wanaona ni upuuzi, wakati wao walipokuwa wadogo shule mama akikosa tu visiting day anafura kama chura
   
 18. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  inawezekana ni kweli. lakini inawezekana huyo mama hiyo ni namna ya kujipatia riziki pia. ni vizuri kuwasaidia watu wa aina hii, ila kama wanadanganya basi nao wanaweza kuadhibiwa kwa kusema uongo. siku hizi kumjua mwenye shida ya kweli ni ngumu. kwani shida za ukweli zipo , na ndizo zinawafanya watu waongezee na uongo ili wasaidiwe
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  una upendo sana we mdada/ mkaka.
  Mungu akubariki. Ahsante kwa kukumbushia watu umuhimu wa wazazi.
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Duh!Husna dunia hii toa msaada uwe msaada usitarajie something in return!!
   
Loading...