Where is Love here?

Where is true love?

  • From GOD

    Votes: 10 66.7%
  • From Parents

    Votes: 5 33.3%
  • From Relatives

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    15

August_Shao

Senior Member
Nov 23, 2007
164
47
JAMANI NASHUKURU SANA KWA USHAURI WENU NDUGU......NIMEFARIJIKA SANA NA NIMEAMUA KUIONDOA HII MAPEMA AS KUWEKA KILA USHAURI UWE KWANGU TU NA KUTOKUACHA ANY TRACES..............

Thank all guys and ladies
 
Last edited:
Shukrani zako zimepokelewa mkuu! Na mimi nimeondoa ushauri wangu pia.. LOL!
 
Last edited:
kaka mi nakushauri ubaki na huyo uliyezaa naye, kwanza nionavyo mimi huyo binti wa Tambaza hakuwa na msimamo japo ulim-let down kwa kuzaa na mtu mwingine ila alitakiwa ku-stick with u.Pili, kaka kuzaazaa na mwanamke zaidi ya mmoja inapunguza concentration ya mapenzi na matunzo kwa watoto. Ili kuondoa fikra za huyo wa Tambaza tafuta mabaya yake na wala si mazuri au ulimbwende wake.Halafu siku nyingine uwe unatumia condom, maana inaonekana umeanza kitambo mambo hayo, na Mungu bado anakupenda maana gonjwa linavizia kutungua watu.
 
mkuu mbona jibu liko wazi tu, uliyezaa naye unampenda anakupenda hadi 'unachukia'. wa pili unadai unampenda na huku amesha 'move on' na mijamaa miwili kwa uchache manake wengine hajakwambia.

hebu mchukue mama mtoto muendelee na maisha uyo wa pili utafulia kaka.

halafu iyo poll inahusianaje na hii thread? am just curious
 
hata hivyo hujatulia kabisaaaa! na tena nionavyo mimi umekuja kuulizia wakati majibu unayo comment zako umedai huyu wa mtoto hajawahi kutoka nje halafu umeshaambiwa kwamba huyu mwingine kabilingishwa na wanaume wawili kwani unadhani utakuwa na radha gani ya mapenzi wakati hujui walikuwa wakifanya naye vipi kwa mazingira yapi japo kakwambia hawakufaa kama wewe! how sure? na kama anasumbuliwa na tamaa zake na ndo maana kajirudisha? who knows kwamba amekwambia idadi ya kweli kwamba walikuwa wawili pekee? labda niwe mwizi nijipeleke kituo cha polisi nikapige makelele "excuse me sir I am a thief" stop kiding yourself! stop kidding the jamii team as we have so many to focus on! lea mwanao na mama yake Tamaa zitakuua kijana AMINA
 
Unapenda wasichana wawili? Hayo siyo mapenzi. Sema unatamani hao wasichana wawili. Kwanza mtindo wa wewe kurefer to them kama mademu inaonyesha bado hauja fikia kuweza kumheshimu mwanamke kama mkeo. Bro my advise is that acha kuchezea mabinti wa wenzio. If you are not ready to commit then let them be. Maana wewe unaye wajua fika walivyo umeshindwa kuchagua sasa sisi tusio wafahamu tuta kuchaguliaje?
 
Kwanza kabisa kitendo ulichofanya cha kuwa na wasichana 2 kilikuwa kibaya, wewe ni mmojawapo wa wale wanaume waongo.
Pili hujui kupenda, ungejua kupenda hapa jibu tayari ungekuwa nalo. Usiwaaribie muda mabinti za watu amua moja, maana ww ndio unajua.
 
Ishi na mama mtoto wako acha tamaa ya kuwa na wanawake wawili...huyo ambaye hujazaa nae mwache aende zake...akapate mwingine.
Kuwa imara simama kiume...acha kuendeshwa na tamaa za kuwa na wanawanake wawili.Na kwa maelezo yako wewe ndio unamtaka huyo binti ambaye huja zaa nae.

Maelezi ya mtoto akiwa chini ya wazazi wake wote ni bora...kaa ukifikiri mtoto wako awe anaishi na mama yake wewe uwe umeoa mtu mwingine?Ni watoto wangapi out there wangepata faraja kuwa na wazazi wote wawili wakawalea?Lakini hawajapata kwa ajiri ya baba zao kuwa na mtizamo kama wako?Una nafasi bado ya kufanya maamuzi makubwa kwa kizazi kijacho play ur part bro.
 
Kwanza kabisa kitendo ulichofanya cha kuwa na wasichana 2 kilikuwa kibaya, wewe ni mmojawapo wa wale wanaume waongo.
Pili hujui kupenda, ungejua kupenda hapa jibu tayari ungekuwa nalo. Usiwaaribie muda mabinti za watu amua moja, maana ww ndio unajua.
aaah ubaya wake nini?
Dini inaturuhusu hata wa4 sembuse wa2? acha kabisa.....nyie ndio mnaomsakama ofisa Kitila mkumbo kwa kummega HG wake....

..ushauri bwana shao angalia shori mkali kwako kwa kila kitu ndio ukae nae....kwa nionavyo mzazo mwenzio anakufaa zaidi
 
Mkuu angalia kifaa ambacho kinakujali na wewe unakipenda unaweza ukampenda huyo mwenye mtoto kumbe yeye hakupendi jaribu kuwa makini.
 
mimi nakushauri uusikilize moyo wako,iili ukae na mtu unayempenda!watu watakushauri weeeeeeeeeeeeeeeee lakin finally wewe ndo utakae ishi na mmoja wapo!

HALLA BACK!
 
Mkuu unajua dini yake mpaka useme inaruhusu wake hata wanne au una presume? If that was the case then kulikuwa na haja gani yeye kuomba ushauri hapa? Si angewaoa wote wawili kama ndiyo hivyo? The guy doesn't love any of them ndiyo maana mpaka sasa hajui amchague yupi. Angekua na mapenzi ya kweli angekwisha mchagua anayempenda zaidi. Sasa yeye anaomba ushauri hapa sisi tutajuaje moyo wake upo kwa nani?
 
pamoja na bold yako sijakuelewa.....point yako ni ipi?
 
Mkuu angalia kifaa ambacho kinakujali na wewe unakipenda unaweza ukampenda huyo mwenye mtoto kumbe yeye hakupendi jaribu kuwa makini.

Macho yako yana matatizo? kwani hujasoma amesema huyo mwenye mtoto anampenda sana hadi anachukia.

Lea mtoto wako , anahitaji mapenzi ya baba na mama huyo mwingine muache atafute wa kwake,
Halafu kuzaazaa kila mtoto na mama yake ni vibaya tena kwa kujitakia kama wewe.
 
Kaka chukua uliyezaa nae tu!!Maana kwa mujibu wa melezo yako hakuna tatizo lolote juu ya uliyezaa nae.Kwa mlinganisho hata km unasema unawapenda wote, huyo unayemwita "DEM" wa Tambaza ana kasoro tayari.Kwanza huna hakika km anakupenda, pili amashamegwa na watu wawili(huenda zaidi). Huyo uliyezaa nae nakupenda mpaka unachukia,pili kwa mijibu wa kauli zako hajawahi kukusaliti(Ingawaje Only God can Confirm that).Oa uliyezaa nae,ni faida kwako na kwa mtoto.
 
Macho yako yana matatizo? kwani hujasoma amesema huyo mwenye mtoto anampenda sana hadi anachukia.

Lea mtoto wako , anahitaji mapenzi ya baba na mama huyo mwingine muache atafute wa kwake,
Halafu kuzaazaa kila mtoto na mama yake ni vibaya tena kwa kujitakia kama wewe.
ubaya wake upi?
 
nimeshangaa hapo anaposema anawapenda wote...kijana unajidanganya!huwezi penda wawili kwa wakati mmoja lazima kuna unaempenda zaidi na anakurudhisha kwa namna moja ama nyingine, mchukue mwenye mwanao mana nahic ndio unaempenda zaidi huyo mwingine unajidanganya, ndio mana wakati mwingine mnashikwa mackio matokeo yake wanaume wengine wanaogopa kuoa, tamaa tamaa.....
 
mimi nakushauri uusikilize moyo wako,iili ukae na mtu unayempenda!watu watakushauri weeeeeeeeeeeeeeeee lakin finally wewe ndo utakae ishi na mmoja wapo!

HALLA BACK!

Mkuu ile ishu yako hiviumetupa feeedback? Lol naona kama inafanana kidogo na hii?
 
Back
Top Bottom