Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,700
- 1,857
Itazame makala hii: http://www.abc.net.au/foreign/content/2013/s3683920.htm
Wazungu wawili wanatembela Tanzania kutazama jinsi biashara haramu ya meno ya ndovu inavyofanyka. Haichukui muda wanaata wauzaji kwa urahisi jijini Dar, ambao wanawapeleka mpaka kwenye kibanda chao na kuwaonesha magunia yaliyojaa meno ya ndovu.
Katika uchunguzi wao wanakutana na wafanyibiasha Wa-Asia Watanzania ambao dhahiri wanakula na wakubwa. Hawa wana mapande makubwa ya mbuga wanazomiliki, na hata mmoja wao alikuwa anajaribu kuuza Uranium iliyoko katika hilo pande lake kwa shirika moja la Autralaia kwa mamilioni ya dola!
Wazungu hao wanatambua mara moja kuwa biashara hiyo isingewezekana kushamiri bila ya viongozi wa ngazi za juu kuihami.
Tanzania, pamoja na kuwa idadi ya ndovu inashuka vibaya sana, bado inatoa ruhusa ya kuwinda wanyama hao na kupokea dola 10,000-15,000 kwa mnyama. Hizi fedha zitatumalizia wanyama na wala hatuzioni!
Wanakwenda Kenya, utaona tofauti na Tanzania, Wakenya wanalichukulia tatizo la uwindaji serious. Wana askari mbuga na magari na hata helikpta zinazozunguka na kuwasaka hawa. Pia Kenya wana kituo kizima cha ndovu yatima, ambao wameokotwa baada ya mama zao kuuawa na wawindaji. Vitu vyote hivi hakuna TZ, watu wanajali kula pesa tu.
Hatimaye filamu inaisha kwa kusema, baada ya miaka ishirini kuanzia sasa huenda kusiwe na ndovu Tanzania!