When you are in denial state..Make sure you are not condemned..!!!

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,121
2,000
Nimeishia kuandika heading ya kimombo halafu huku chini natiririka kibantu.. Usinipige mawe.. Nimekosa maneno sahihi mafupi yanayotoshelea heading.. Ngoja sasa nifafanue
Denial state inatokana na neno deny.. Yaani kukataa ama kukataliwa.. Kwahiyo unapokuwa kwenye hiyo hali wewe ni makataa yani umekataliwa na hukubaliki tena.. Yani hata ufanye zuri gani litaonekana baya machoni pa wengi
Sasa ni afadhali kuwa kwenye denial state(makataa) kuliko kufikia hali ya kuwa condemned! Denial state is the primary level.. Condemned is the secondary level

Unapohukumiwa kifo hii inaitwa denial level.. Adhabu ya kifo inapotekelezwa unakuwa sasa wewe ni condemned! Ndio maana siku ya kunyongwa baada ya kumaliza taratibu zote chumba cha mwisho unachoingia kabla ya kufikia kitanzi (kifo chako) kile chumba pale kwenye mlango wake kuna maandishi makubwa mekundu yameandikwa kwa herufi kubwa CONDEMNED
Huo mlango ni wa njia moja tuu... Ni wa kuingia tu huwezi kuutumia kutokea.. Condemn kwa tafsiri ya Google ni laaniwa au laanifu.. Lakini pengine si neno sahihi sana.. Pengine Google wamelitumia kwakuwa LAANA haina TIBA ukishalaaniwa umelaanika hakuna rivasi.. YOU ARE CONDEMNED!
Kwahiyo sasa denial inavumilika kuna nafasi ya kurekebisha tena lakini condemn ni kwamba hufai tena.. Huna thamani tena..
Wengi wetu hupitia hii hali ya makataa (denial) kwenye jamii wakati wa makuzi yetu na kwenye harakati za maisha na sometimes kwenye mahusiano au kwenye mambo ya kijamii kama siasa, madaraka na uongozi.. Na hii yote husababishwa na tabia hulka ama nyota kufifia
Kuna baadhi hujistukia mapema na kuanza kutafuta suluhisho mapema sana na kuna baadhi huamua kuchagua njia sahihi ya kuishi na hiyo hali.. Shida ipo kwa wale ambao hawajikubali kuwa wana hiyo shida hivyo hujikuta ni watu wa kugombana na kila mtu kila mahali kila mahali na kujikuta wanajiona kama adui wa jamii (public enemy) hii hali ikiwa sugu unakuwa condemned na jamii na likikupata baya lolote badala ya jamii ikupe sympathy.
Ndio kwanza inashangilia na kufurahia...

Anakufa mtu mtaani kila mtu anasikitika na kuhuzunika sana na sifa zote nzuri anapewa yeye mpaka shetani anaona wivu halafu mtaa huohuo anakufa mwingine na jamii inalipuka kwa shangwe vifijo na nderemo..
Watu wana kunywa pombe kwa furaha
Wengine wanafanya karamu
Wengine wanataka waione maiti yako waipige mawe
Wengine wanataka kuitemea mate
Wengine bila kujali ni maiti bado wataendelea kuipiga na kuitukana
Wengine wanaweza hata kutafuta mafuta na kibiriti waichome moto
Ni usiku mwingi huu lakini niko macho.. Natafakari mengi mno.. Kuna binadamu tuna roho mbaya sana.. Huwa hatupendi kuona wengine wakipata ama kuwa na furaha.. Tutawatupia kimavi.. Makataa ya kishirikina (gundu la mavi) ogopa sana hii kitu.. Utakimbiwa mpaka na shetani..

Unajikuta unakuwa mtu wa mawazo mpaka unakonda.. Unatafakari nimewakosea nini hawa binadamu? Mbona najitahidi sana,? Tatizo ninini? Ni wakati unajiuliza haya kumbe nao wanakuwazia mabaya.. Unawashangaa wanakushangaa.. Mnabaki kuwindana.. Unawawinda ukiamini kuna wachache wanatumika kukuharibia kwa wengi.. Wanakuwinda useme tena watengeneze story za kukuponda
Katika magundu yote.. Ogopa gundu la kimavi cha kinyesi.. Pata picha pale unapohisi umekanyaga kinyesi tena na kiatu.. Hakuna maumivu unayopata lakini lazima uchechemee

Rest in peace Siad Barre.. Sorry Farrah Aidid also rest in peace....!!!! U 2...In advance !!!!?

Jr
I like the last sentence!

Jana tumekuwa treated na sinema ya vipimo vya corona. Kwa jicho la tatu, hadithi hiyo haina tofauti na ile ya makinikia na Noah zetu. Mwisho wake utakuwa ni huo huo. Hamna kitu!
 

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,300
2,000
Mada fikirishi na ina mazingatio makubwa ndani yake ,inatokea sana kwenye maisha yetu ya kawaida hata kwenye mahusiano muhimu ni kuchange gia haraka kama unaona kuna sehemu unakosea kabla kufika stage mbaya zaidi.Hayo ndiyo nimejifunza kama kuna mtu kalengwa mambo yao nawaachia wenyewe .
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,040
2,000
Mada fikirishi na ina mazingatio makubwa ndani yake ,inatokea sana kwenye maisha yetu ya kawaida hata kwenye mahusiano muhimu ni kuchange gia haraka kama unaona kuna sehemu unakosea kabla kufika stage mbaya zaidi.Hayo ndiyo nimejifunza kama kuna mtu kalengwa mambo yao nawaachia wenyewe .
sijalenga mtu ni mada ya wote

Jr
 

aldeo

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,642
2,000
Bagonza huyu bana... Unaweza kuwaza kuwa ni HEKIMA ya mwendawazimu... Lakini inatafakarisha sana... Waja wanaweza kuchuliana kifo sasa View attachment 1439340

Jr


Unapoteza muda kuumiza kichwa Chako kwa kitu ambacho hata ufanyeje uwezi kukuweka utakavyo.

Subiri kampen hamasisha watu vizuri, nenden mkaamue kwenye sanduku la kura.

Tofauti nahapo ndugu yangu n kilio Cha samaki machozi huenda na maji.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
14,157
2,000
Brother mshana. This is how unandika post inayoeleweka na deep thinkers. Ndio maana wale trash politicians huku kwenye post yako huwaoni.
Back to the topic hili jiwe ni special.. japokuwa kuna mtu ameguswa indirect.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,040
2,000
Brother mshana. This is how unandika post inayoeleweka na deep thinkers. Ndio maana wale trash politicians huku kwenye post yako huwaoni.
Back to the topic hili jiwe ni special.. japokuwa kuna mtu ameguswa indirect.

Sent using Jamii Forums mobile app
downloadfile.jpg


Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom