Whatsssssss!!!!!!!!!????

Whatsssssss!!!!!!!!!????

Jamaa mmoja kakodi tax akiwa anatembea katika jiji mara akapita gest moja akamuona mkewe akiingia ndani ya gesti, jamaa akamwambia dereva simama, jee? unataka laki tatu za chap chap? dereva akajibu ndio, jamaa akamwambia nenda mle gesti kamtoe mke wangu picha yake hii hapa, tena uwe unampiga ngumi, mateke, vichwa, makofi mpaka ufike nae hapa, dereva kaingia ile kutoka anakuja na mwanamke mwingine na kichapo kinaendelea, Jamaa kaduwaa na kusema we vipi mbona huyo sio yeye? Dereva akajibu huyu mke wangu, subiri nitakwenda kumtoa wa kwako pia
 
Demu: Mambo
Demu: Nna mimba
Boy: Unasemaje? Si tulitumia condom
Demu : Kwani nimesema ni mimba yako?
 
Juzi nilisinziaa kanisani mara nkasikia jirani yangu ananimbia pembenii!mpendwa amkaa!!Nikasikiaa na mchungajii uko!! NYANYUKAA!!nikasimaama watu wakapigaa makofi
mchungaji😱ooh asanteh sana haya mwinginee anaetoaa million 2 kama mchangoo wa shughul za kanisaa??
my frend nilizimiaa ndo nimeshtuka sasa hivi
 
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!
 
Kuna mtoto wa jirani ananibore sana kila nkimtuma kitu dukani lazima aonje, Jana nlimtuma sukari akala yote..

Sasa nmemtuma superglue haongei
 
Madem mnavaa earings kwa masikio, mapua, ulimi, kitovu, sijui kwa uso.manecklaces ka mia mbili bangili mikononi handbag nayo ina makorokoro elfu2..sasa itokee ujikwae udondoke unatoa sauti kama kabati la vyombo limedondoka
 
binafsi hua namuogopa sana mwanamke ambae haombi ela hua simuelewi anataka nini kwasababu akisema anataka mapenzi tu najua uongo

ni sawa na shetani akwambie bwana yesu asifiwe unashindwa kuelewa uitikie amen au ukemee
 
Nakumbuka kipindi tupo Sunday school mwalimu akatuuliza nani anataka kwenda mbinguni wote wakanyoosha nikabaki mm tu aliponiuliza kwa nini sijanyoosha nikamwambia Mama kanambia nikitoka kanisani nisiende popote ninyooshe nyumbani.
 
Kuna jamaa kwenye daladala hapa, alikuwa anaongea na simu

"Haloo leo sitaweza Kuja nimepanda gari moja na mmeo"

Unaambiwa wanaume wote wenye wake wamemng'ang'ania aoneshe hiyo namba aliyokuwa anaongea nayo.
 
Jana nilipanda daladala basi ile kaka yenu nikawa nimejiachia kuchati, kuna jamaa akawa anasoma msg zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati...

Basi nikasema ngoja nimtie Adabu.. Nikaamua nimtext jamaa "Oya Alex ngoja nilipue hii daladala muda ushafika" Yule jamaa akajirusha dirishani
 
Back
Top Bottom