Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba
ampandishie mshahara….. Mama mwenye nyumba
akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka
kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kwenye mambo yetu kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa
tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara
moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi
najitahidi kwa bed kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie.
Nitakupandishia mshahara wako mara tatu!!


