FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Hivi karibuni WhatsApp itasitisha programu yake kwa mamilioni ya simu baada ya kutangaza kwamba programu hiyo itaacha kufanya kazi katika simu za zamani.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na Facebook iliweka wazi katika ukurasa wake wa msaada, simu za mikononi ambazo hazitaweza kupata programu hiyo, ikidai hatua hiyo inahitajika kuhakikisha usalama wa watumiaji wake.
Matoleo mbalimbali ya simu za Android, iPhone na Windows zitaathiriwa pale huduma ya programu hiyo itakapositishwa rasmi tarehe 1 Februari, 2020.
WhatsApp haitafanya kazi tena kwenye iPhones zozote zinazoendesha kwa mfumo wa iOS 8 au kabla ya huo, ambao ulizinduliwa na Apple mnamo 2014. Hii inamaanisha mtu yeyote aliye na iPhone 6 au mpya ya hiyo hatahitaji kuwa na wasiwasi juu ya kupoteza WhatsApp.
Simu za Android zinazotumia toleo la zamani kuliko 2.3.3, pia likijulikana kama Gingerbread hazitawezeshwa tena na programu ya WhatsApp na mtu yeyote atakayejaribu kufungua akaunti mpya au kuhakiki akaunti iliyopo kwa kutumia matoleo ya zamani ya Android atazuiwa.
Simu za Windows zinazoendeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Windows 8.1 au zaidi zitaendelea na huduma ya WhatsApp kwa kutumia programu hiyo.
Chanzo: Independent UK