WhatsApp GB ni hatari kwa faragha zako kwenye simu

Jun 8, 2016
8
22
''GB WhatsApp'' ni toleo la WhatsApp lililoboreshwa kutoka WhatsApp halisia na kuongezewa vitu vya ziada kama vile Kuficha kitiki pale ujumbe unapofika, kuona ujumbe uliofutwa, kuona status iliyofutwa na mengine mengi ndani yake.

Sasa ni zipi faida za kutumia GB WhatsApp?

Kutumia WhatsApp mbili kwenye simu moja.

Inakupa chaguo la yenyewe kujibu ujumbe kama ifanyavyo WhatsApp Business.

Kusoma jumbe zilizofutwa (Deleted Messages)

Machaguo mengi zaidi ya kuficha soga(chats).

Ku-download WhatsApp status.

Kubadili muundo wa maandishi.

Ki-uhalisia haina faida ila kwa baadhi ya watumiaji wametanabiasha sifa tajwa hapo juu kama faida kwao kimatumizi.

Hasara za kutumia GB WhatsApp

Haiko rasmi kwenye masoko ya kupakua Application (Playstore/Appstore) hivyo inakuitaji kwenye Website ili kuipakua.

Ni kinyume na sheria kwa maana hairuhusiwi kimatumizi.

Sio salama kwa maana ya mfumo wake, huweza kuchukua taarifa zako.

Account yako kufutwa na WhatsApp wenyewe, na hapa ndipo watu wengi wamekumbana na kadhia kwa kipindi cha hivi karibuni.

ACADEMIC TEACHER ONLINE hatushauri mtumiaji wa simu janja kutumia aina hii ya WhatsApp, kwani haiko salama kwa upande wa Faragha zako.
 
Asante
 
Hamna kitu hapo, changamoto ya hizi WhatsApp mods ni kupigwa ban na WhatsApp tu, sasa usalama wa mtu kama mimi ni wa nini sasa, kwanza pamoja na kuwa ziko moded ila security bado ni ile ile end to end Encryption kama sijakosea.
 
Sasa mkuu mimi usalama wangu hata hao developers wa hizo apps wakichukua taarifa zangu watapeleka wapi mkuu.
Kuna mambo madogo madogo ambayo si hatari kwa nchi lakini yanalinda utu wako kama binadamu.

Mfano, chatting talks zako na wanawake zikiwekwa public ulivyokatiliwa watu wakaanza kuzichambua utaona privacy yako haijatendewa haki.
 
Hivi kwa mfano me hata wakichukua taarifa zangu zinaweza wasaidia nn au kuniumiza nn? Binafsi sioni faida wala hasara ila situmii hizo app za michongo
 
Gb WhatsApp inatoa vipengele vingi vya ubinafsishaji vinavyoruhusu watumiaji kubinafsisha mwonekano wa programu. Watumiaji wanaweza kuchagua kutoka mandhari mbalimbali, kubadilisha ikoni ya programu, na kubinafsisha mandharinyuma ya gumzo, fonti na rangi kulingana na mapendeleo yao. Gb WhatsApp inaruhusu uhamishaji wa faili kubwa. Watumiaji wanaweza kutuma faili hadi ukubwa wa MB 50, ikilinganishwa na kikomo cha MB 16 cha programu asili.
 
Back
Top Bottom