What's in a name?

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,733
123
Lowassa katoa Buriani iliyoPinda bila Daftari kwa Ghasia kama kalewa Pombe vile.

Whats in a name? Next cabinet the Prezzo better be careful, lol!

_44410170_palowassa203.jpg



IFUATAYO ni hotuba fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward
Lowassa katika Bunge mjini Dodoma leo (Alhamisi Feb.
7, 2008) asubuhi, wakati wa mjadala wa Taarifa ya
Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni
ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi
"Richmond Development Company LLC" ya Huston, Texas,
Marekani mwaka 2006:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii
kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza
katika hoja hii.


Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe,
Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa
mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa
nzuri kweli.


Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri.
Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika
kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk.
Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa
anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa
anafundisha ni "Natural Justice".
Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala
la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza
watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya
mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi,
lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle
hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu.
Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama
wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na
nilikuwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba
wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu
katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu
ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza
Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa
kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata
utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema
mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records
na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini
chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika
nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki
haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda
vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini
wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa
nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa
kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana,
nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi
ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani
kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani
kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa
tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni
mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda
wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye
wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza
ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo
wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya
ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha
majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti
mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna
hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima
wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki
kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja.
Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia
nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki,
amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza
hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana
jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima
wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka
wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo
kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am
going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni
Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio
amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama
changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua
kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.
Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha
dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu
uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia
mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana
Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa
Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu
Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa
CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".
 
Back
Top Bottom