What should I do?

Ms eyes

JF-Expert Member
Feb 4, 2023
4,632
11,543
Hellow Guys!
Hope mnaendelea vizuri.

It’s “Ms Eyes” again.
Sorry naombeni ushauri ni kwa namna gani naweza kuongeza idadi ya watu as you all know dunia ya sasa hivi bila connections ni ngumu sana kutoboa na hizo connection huwa zinatoka kwa watu. Can you all imagine sina hata watu 90 kwenye mzunguko wangu wa maisha.

Mimi ni aina ya wale watu ambao napata shida ku interact na watu, ni ngumu sana kumzoea mtu, siwezi kukaa kwenye mkusanyiko wa watu wengi. Mara nyingi huwa nipo ndani haswa kama sina shughuli ya kufanya kwa siku hiyo au wakati huo.

Napata shida sana haswa kwa kipindi hichi ambacho nahitaji kazi, nilijaribu kufanya biashara ya kukopesha lakini sikuiweza kwasababu huwa sipendi kuongea na kugombana na watu, hata hivyo nilikuwa napata wakati mgumu kwasababu sikuwa na watu wengi wa kuwatembezea bidhaa zangu.

Marafiki ndio kabisa sina, napitia changamoto nyingi sana sina hata mtu wa kuongea nae au wa kunipa mawazo tofauti ili niweze kuwa sawa kwa kiasi fulani. Simu yangu inaweza isipigwe kwa muda hata wa siku tano😂💔.

NIKO HAPA KUPOKEA USHAURI WENU WAKUU. Ningependa kupewa majibu positive ili nisiendelee kuvunjika moyo though kuna watu wapo watanijibu negative.

HAPPY ENDING WEEKEND Y’ALL.😍

Karibuni!
 
Watu 90?? Mbona wengi sana

Kama unao 50 kwenye maisha yako wanatosha sana...hata hivyo kujuana sana sio issue wala nini,kwanza unajiepusha na mengi

Kuhusu kutopigiwa nayo mbona fresh tu...wewe huwa unawapigia lakini?
Hapo 90 bado hata sijafika huko, naelewa kuwa na watu wengi sio issue ila inasaidia wakati mwengine kupata connection. Huwa nawasiliana na familia yangu tu🙁.
 
Tupo wengi wenye maisha aina hiyo ila hapo kwenye simu hapana,, huna hat boyfriend?

Kuzungukwa na watu wengi inafariji hasa ukiwa katika mafanikio kinyume na hapo utajua waliokuzunguka hawakuwa watu ila wanafiki bora peke yako,,

Endapo ukihitaji sana shiriki shughuli za kijamii utapata marafiki wanafiki mpaka utawakwepa
 
Boyfriend hapana, wanani heartbreak sana nakuwa sina hata amani ya kuwa kwenye mahusiano.
 
Kuwa Mtu wa kwenda ibadani kila wakati sehemu za ibada ni sehemu nzuri kutengeneza networks maana pale watu wengi waliofanikiwa upenda kwenda kumshukuru Mungu kwa kuwafanyia Jambo na wengine kusali kawaida tu.

Pia Sehemu za starehe nenda Sehemu zenye utulivu Kama Kilimanjaro hotel hapo utaanza Kupata sura mpya pia kuwa mtu wa kusalimia watu usisubiri wao wakuanze .
 
Kwanza tambua na kubali kwamba wewe ni introvert.
Pili, jaribu kutafuta watu wa karibu na sio marafiki kama unavyo fikiri.
Marafiki unaweza ukawanao hata 1,000 na wote wasiwe marafiki wa faida katika maisha yako, na kwatabia za watu wa aina yako yawezekana marafiki wengi wasio na faida kwako ndio watakuongezea shida na makasiriko zaidi.
You better find a closer friend for your inner cycle, because they will be always there for you babe...😊
Yaani namaanisha kwamba.....
Nibora uwe na watu wako wa karibu ambao ni sahihi hata watano (5) ambao watakua tayari kusimama na wewe wakati wote, kuliko kua na marafiki 100 wasio na faida kwako.
Okay.......
Kua na marafiku wengi haikupi uhakika wa kutengeneza network kubwa.
 
Tupo wengi wenye maisha aina hiyo ila hapo kwenye simu hapana,, huna hat boyfriend?

Kuzungukwa na watu wengi inafariji hasa ukiwa katika mafanikio kinyume na hapo utajua waliokuzunguka hawakuwa watu ila wanafiki bora peke yako,,

Endapo ukihitaji sana shiriki shughuli za kijamii utapata marafiki wanafiki mpaka utawakwepa
Naomba niwe rafiki yako.
 
Back
Top Bottom