Hakuwa George Masatu, Ni Rashid AbdallahIle mechi Simba walizidiwa mbinu. Nakumbuka Boli Zozo alivyomgeuza George Masatu kama chapati kabla ya kupachika bau.
Hakuwa George Masatu, Ni Rashid AbdallahIle mechi Simba walizidiwa mbinu. Nakumbuka Boli Zozo alivyomgeuza George Masatu kama chapati kabla ya kupachika bau.
Hii Stori naitamani Sana niielewe kiundani wake zaidi. Nawaomba wale wajuzi wa kitu waje kutujuza basi.
azim dewji yeye alizimia kwa mshtuko mechi ya kabla ya fainali akidhani SIMBA haitatoboa to final. (Maelezo haya ni kutoka simulizi ya Fikiri MAGOSO... Beki wa SIMBA iliofika fainali)nakumbuka 1992 au93 marehemu Gulamali alilia badala ya kucheka Yanga walipofanya kweli pale kampala na kubeba ndoo ya cecafa bila kutegemea mdosi akawa ameahidi donge nono kama wangewafunga villa wenyeji kwenye final ambayo zamoyoni mogela alitupia goli 2
Mkuu umesahau Al harach ya algeriaTulianza Kwa kuwatoa Ferroviario ya Msumbiji Kwa advantage ya Goli la ugenini hapa tulitoka bila nila kwao tukatoka Moja Moja
Tukaenda Robo Fainali tukamchapa nje ndani Timu ya Manzini ya kule Swatziland
Tukaingia nusu Fainali tukacheza Na Club bingwa ya Angola ya wakati huo inaitwa Atletiko Aviacao hapa Taifa Tukampiga Tatu Kwa Moja then kwao tukapigwa Moja bila wakawa wametoka
Tunaingiza Fainali Sasa hapo, Ikawa Simba vs Stella Andijaa
Mechi ya kwanza tukaanza kule Kwao Ivory Coast tukatoka nao suluhu ya Bila ya kufungana
Sasa Kombe Uwanjani ya Kombe la CAF Africa nzima ikafanyika Uwanja wa Taifa
Mgeni wa Heshma akawa Rais Ally Hassan Mwinyi akisindikizwa Na Waziri wake wa Michezo Prof Philemon Sarungi ( Mshabiki wa Simba damu)
Wakati huo Kocha wa Simba akiwa Abdallah King Kibaden Mputa Na Msaidizi wake akiwa Hassan Hafif
Tukapigwa Goli la kwanza Uwanja Ukawa kimyaaaaa Mara likaingia la pili Mchomo uliopigwa umbali wa mita 18 hapo ndipo Kelele za Mashabiki wa Yanga '...Uzalendo umetushinda...' Ndio zikaanza
Mpaka Mwisho bila ya kutegemea Mzee Mwinyi akashuka Jukwaaani Kwa huzuni usoni lakin akiwa Na furaha moyoni Kwa Kuwa Nae Ni Yanga Damu Kuliko Mzee Akili Mali
Baadhi ya Wachezaji ninaowakumbuka wa Simba Ni Mohamed Mwameja, Hussein Masha, George Magere Masatu, Alfred Kategile, Damian Kimti, Alfred Kategile, Alphonce modest, Makenzi Ramadhan, Dua Said, Edward Chumila n.k
Personally naamini Kwa Umri wangu niliosalia sitoishuhudia Simba bora ya kiwango ile
Mzee Mwinyi akakabidhi Kombe Kwa kina Bolizozo nao usiku ule ule wakaondoka Na Kombe kupumzika Nairobi
Nakumbuka Siku chache kabla ya Mechi, Uongozi Na Mashabiki wa Simba hawakuwa wakijadili Mikakati ya Ushindi wa Mechi hiyo bali walikuwa wakijadili Kombe litakaa wapi baada ya Mechi hiyo wengine walisema Ikulu, wengine BOT hakuna kujadili Mikakati ya Ushindi
Boli Zozo huwezi sahaulika katika kumbukumbu za wana Simba.Simba waliuawa na mtu mmoja aliyeitwa Boli Zozo baada ya kumgeuza kama chapati kwa chenga mlinzi wa Simba Rashidi Abdallah.
Ilikuwa ni game ya fainali ya kombe la Caf mwaka 93 kati ya Simba Sport Club Vs Stella Abidjan ya Ivory Coast.. Tetesi zilizoenea mitaa ya jiji la Dar WS Salaam na viunga vyake ni kwamba Simba Sc waliuza hiyo game..Wadau wa Soka la Bongo ..What do u think ? Ni kweli Simba waliuza hiyo game ? Kama waliuza nani walihusika na mchezo huo mchafu ?
Uongo mtupu,hakuna aliyeuza game,uwezo uliishia pale hakuwa na la zaidi la kufanya.Wachezaji wa ndani tu na ligi ya ridhaa unachukuaje continental trophy? Miaka 22 baadye ndo timu inacheza final nyingine hamuoni kwamba nyakati zilikuwa bado?Aliahidi gari aina ya KIA kwa kila mchezaji,wachezaji walikua 30,sasa piga hesabu..baniani ikabidi afanye ubaya wake,akatembeza hela kwa wachezaji muhimu wa simba,simba akafungwa kizembe,mzee mwinyi akiwa mgeni rasmi ilimuuma sana,akawaomba wamwingize lunyamila,akaambiwa yule yanga
Wenzetu walikuwa tayari waepitia misingi ya soka.Hakuwa George Masatu, Ni Rashid Abdallah
Kitakuwa ni hikihiki kibabu....lakini tunakishukuru,maana tungehama mijini.Azim Dewji anajua