Ilikuwa ni game ya fainali ya kombe la Caf mwaka 93 kati ya Simba Sport Club Vs Stella Abidjan ya Ivory Coast.. Tetesi zilizoenea mitaa ya jiji la Dar WS Salaam na viunga vyake ni kwamba Simba Sc waliuza hiyo game..Wadau wa Soka la Bongo ..What do u think ? Ni kweli Simba waliuza hiyo game ? Kama waliuza nani walihusika na mchezo huo mchafu ?
Jumapili ya 19/5/2019 kwenye kipindi cha Sports AM kinacho rushwa na Azam TV kikiongozwa na Mahmud Zuber, Ali ulizwa mgeni mwalikwa aliyekua mchezaji wa Simba na aliyekuwepo kwenye timu iliyo ingia fainali ya 1993 Fikiri Magoso.
Alichosema Aliyekua mfadhili ndugu Azim Dwji japo yeye Fikiri Magoso hakutaka kumtaja jina ila anafahamika nani alikua mfadhili kwa wakati ule.
Dewji aliwapa fedha baadhi ya nyota wa Simba ili wafungwe. Kwamujibu wa Magoso anadai inawezekana labda ahadi aliyoitoa ilikua ni kubwa na hakutegemea timu itafika fainali.
Anadai kule Angola baada ya mechi kwisha kwa suluhu ya bilabila na timu kufuzu baadaya ushindi wa tatu kwa moja, Dwji alizimia na yeye alikua mmoja wa watu waliomsaidia wakati amezimia kwakua alikua kwenye bench.
Baada ya Mechi ya fainali hapa DAR kwisha wao walijua ninikilitokea mbaka wakapoteza ile mechi na baadhi ya wachezaji akiwemo yeye Magoso , Godwin Aswile,Ramadhan Reny, Dua Said na mwingine ambaye alimtaja ila Mimi nimemsahau , waliamua kutaka kuitoa siri ya nini kilitokea kwakua lawama zote zilikua juu yao wachezaji.
Mfadhili aliwaita pembeni wale waliotaka kutoa siri na kuwapa shilingi lakitano kila mmoja.
Shida ilikuja baadae, Baada ya kukosa kombe waliahidiwa watapewa zawadi ya gari ndogo. Baada ya gari ndogo kutolewa kwa wachezaji, shida ikarudi kwake yeye na wale walio pewa zile lakitano kwa kila mmoja.
Mfadhili alitaka kwanza warudishe zile laki tano, ndio wapewe zile gari ndogo, kwaiyo wachezaji karibu wote walipewa zile gari ila wao waliopewa kiziba mdomo walichenjiwa kibao, sasa katiyao kila mmoja alitumia njia yake kuweza kupewa gari. Anadai katiyao (walio kula kiziba mdomo) kunawengine hawakurudisha ila gari walipewa ila yeye alitafuta mbaka akaipata iyo laki tano na kuipeleka na kukabidhiwa gariyake ndogo.