Mkuu wangu, nilikuwa sijui kuwa Lipumba nae ni kiongozi wa CHADEMA. Nadhani mambo yanakwenda haraka kuliko nilivyodhani. Kama si kiongozi wa CHADEMA na kama anakiri kutojua taratibu za uchaguzi ndani ya chama hicho, anapata wapi mamlaka ya kutoka public na kulaumu taratibu hizo (asizozijua)? Nilidhani yeye kama kiongozi wa chama kitaifa na msomi aliebobea, angekuwa na busara ya kupata ukweli na kuuchambua kabla ya kusema au kutoa hukumu kama alivyofanya. Hasa maelezo mengi yanapokuwa yametolewa kuhusiana na sababu za kuahirisha uchaguzi huo au kutangazwa kwa matokeo.
Ni dhahiri kuwa, kama uchaguzi ulikuwa una makosa mengi, hata uhalali wa matokeo unapotea. Hakuna haja ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mchafu. Hivyo ni vyema kuchunguza na kujiridhisha kuwa tuhuma za uchafu wa uchaguzi huo hazipo, ndipo kuyatangaza matokeo hayo.
Vile vile, sioni unazungumzia chama kuwa driven kwa tribe gani, ya Dr. Slaa alietangaza au ya nani hasa?
Kwanini Chadema wamemwalika Lipumba? kwa hiyo wakati wamemwalika wenyewe kwanini asiwaambie ukweli kuwa mnapindisha Democras..
Mbona Lipumba anazungumza sana kuhusu kupindishwa kwa Democras ktk ccm,mbona hata chadema wanazungumza kupindishwa kwa democras ktk ccm,au sisi hatuna haki ya kuhoji chadema inavoendeshwa kishaghlabaghla. wakiwa wataharibi Democras kila mtu ana haki ya kuwatolea macho,na sio itolewe macho kwa ccm tu. mkiambiwa inakuumeni lkn huo ndio ukweli.