What is This In CHADEMA ? six months ? Tupeni jibu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What is This In CHADEMA ? six months ? Tupeni jibu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 3, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim, Lipumba amesema, kitendo cha uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuzuia matokeo ya uchaguzi wa Baraza la vijana la chama hicho (Bavicha) na kuuahirisha uchaguzi wake, kinaleta tafsiri kwamba mtu waliyekuwa wanamtaka hakushinda.

  Juzi Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, alisitisha kutotangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Bavicha na kuahirisha uchaguzi wake kwa muda wa MIEZI SITA, jambo ambalo limepingwa na Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

  Alisema kwa kawaida uchaguzi unapofanyika, matokeo lazima yatangazwe na si kuahirisha kutangazwa kwa matokeo kama walivyofanya Chadema.

  “Kama umeruhusu uchaguzi ufanyike na ukafanyika na kura kuhesabiwa, hapo huna sababu ya kutoyatangaza matokeo, ukifanya kinyume maana yake ni kwamba unataka kufinyanga demokrasia na italeta tafsiri kwamba yule uliyekuwa unamtaka ashinde, hakushinda” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema hata katika chama chake, kuna matatizo lakini, hakidiriki kuficha matokeo ya uchaguzi na badala yake wanatangazwa na wasioridhika kukata rufaa.

  Profesa Lipumba alisema ingawa hana uhakika wa taratibu za uchaguzi ndani ya Chadema, lakini katika mambo ya msingi kama hilo, chama kinapaswa kujikita katika kuheshimu na kusimamia katiba na kanuni za uchaguzi za chama.

  Alisema wale wote wanaotuhumu matumizi ya fedha na kampeni chafu wanapaswa kuthibitisha hilo kwa ushahidi uliowazi, ili uongozi wa chama uweze kuwashughulikia wahusika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya chama husika.

  Tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi wa Chadema matukio, kumejitokeza matukio kadhaa yanayoambatana na vurugu za wafuasiwa wa Mwenyekiti wa sasa wa Chadema Freeman Mbowe na Naibu katibu mkuu wake, Kabwe.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  CHADEMA kwishne?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chama cha Demokrasia Makini ,embu tupeni umakini wa kuahirisha kipindi cha miezi sita,unakataza matokeo yasitangazwe afu unawambia wateja tukutane tena baada ya miezi sita ,what the hell of this bulliest annoucement here ?

  As we say this party driven as the tribal sector and the chairperson is the emperor or persecutor and seems to be the oppressor for the entire wanachama.

  Now unaweza kuona tofauti ya Zitto na Vigogo wa Chadema ,kwamba demokrasia haipo ndani ya Chadema as inavyotakiwa.miezi sitaa ,aloo bora mvunje chama.
   
 4. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hiyo inaitwa Demokrasia ya Kifisadi, yaani sitoshangaa ikawa ni Vibabu vile vile vilivyomshauri Zitto atoe jina lake kwenye kugombea uenyekiti wa chama ndio vimeamua tena kufuta matokeo ya uchaguzi wa vijana. Kwenye hili la kuamua kuficha matokeo na kuahirisha uchaguzi mpaka miezi sita ijayo hawana tofauti kabisa na chaguzi za Chama Cha Mafisadi (CCM).

  Ila naamini kwa sababu chama ni bado kichanga kina nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuachana na demokrasia fisadi. Ni matumaini yangu baada ya mikutano yao kutakuwa na mabadiliko katika utendaji wa baadhi ya mambo ili kila kitu kifuate haki na demokrasia ya kweli.
   
 5. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katiba ya Chadema inasema nini katika kutangaza matokeo ya uchaguzi?
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa ameeleza sababu kuwa amepokea malalamiko (kwa maandishi) na vielelezo vinavyoonyesha kuwa rushwa ilitembezwa wazi wazi tena na kigogo wa chama. Pia kura zilikuwa batili baada ya kuwa nyingi zaidi ya wapiga kura. Yaani kura 20 zilizidi wakati huo huo aliyeshinda amempita aliyeshindwa kwa kura pungufu ya 20. Dr. Slaa ametangaza kuwa katika muda huo (six months) wanafanya uchunguzi na kushughulikia hizo kasoro.

  Sasa Prof. Lipumba haoni kuwa hizo ni sababu za msingi? au ni Prof. uchara. Na wewe Mwiba acha ushabiki wa CUF na kumshabikia Lipumba ktk kila kitu, tumia akili yako.

  Palipo na ukweli tuache kushutumu bali tuunge mkono, wanapokosea tuwaambie.
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hakiwezi kuwa kwishne! hujaambiwa kuteleza siyo kuanguka? Baada ya chaguzi hizi kupita CHADEMA itaendelea kuwa kipenzi cha wananchi wanaotaka mageuzi. Pia CHADEMA itakuwa moja ilimradi tu Zitto avunje kundi lake.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ukishaoona wanasiasa/wananchi ambao sio wa chama chako wanakuwa-concerned na chaguzi za ndani za chama chako, basi jua chama chako kiko juu....

  Lipumba ameonyesha hii.... Hongereni CHADEMA
   
 9. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh,Yaani baado kuna watu wanaendelea kutete huu upuzi wa chadema?Katiba?kuna katiba inasema matokeo baada ya miezi sita?Mtashinda kwenye computer zenu lakini ukweli unabaki palepale mumechemsha.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi Mwiba unaitakia nini CHADEMA wewe?
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  "Ilimradi Zitto avunje kundi lake"? yamefikia hapo? Kwa nini Mbowe naye usimshauri avunje kundi lake? yaani la Freeman libaki na la dogo Zitto life? Kwa hiyo Freeman ale keki yake na abaki nayo mkononi? Kwa mtaji huu tutafika kweli?
   
 12. C

  Calipso JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya je na Naibu katibu mkuu Zitto hajui kama kuna tatizo ndo mana uchaguzi ukaahirishwa,au naye ni Zito uchwara? Je na slaa alitumia katiba gani kuahirisha uchaguzi bila ya kuitisha mkutano wa cc? je na yeye ni Docter uchwara? we lala,watu wanakula juu huko,mkiambiwa kweli mnanuna,Ama kweli mtu akipenda hata chongo atasema kengeza
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  Nae huyu na taasisi yake ya dini cuf anatuzingua tu,cuf sera zimewaishia wamebaki kuangalia chadema wanafanya nini.Baada ya operation sangara nao wanakuja na operation.......pamoja na uprofessor lakini huyu bwana ni mvivu wa kufikiri ile mbaya.
  ''USAWA HAUPATIKANI KWA MZANI KUWA SAWA,INATEGEMEA NA MPIMAJI MWENYEWE''
   
 14. C

  Calipso JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jana ktk hotuba yake Mbowe alikifagilia sana chama cha Cuf na akasema ni chama makini sana,na mwisho akasema atashirikiana vyama vinavyoonekana makini tu. katafute hotuba yake. usije ukalia peke yako lkn. na mambo yako ya udini yaeke kwako sio hapa,Ficha upumbavu wako.
   
 15. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hiozi siasa za bongo zinatia hasira sana. inaumiza sana kuona watu hawafati misingi wanayoiamini, they preach water and drink wine.
   
 16. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwiba,

  Hivi msemaji wa CHADEMA ni Lipumba au Slaa?
  Hii post yako inavyooneka imetokea CUF, we soma para ya kwanza!!
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Mkuu wangu, nilikuwa sijui kuwa Lipumba nae ni kiongozi wa CHADEMA. Nadhani mambo yanakwenda haraka kuliko nilivyodhani. Kama si kiongozi wa CHADEMA na kama anakiri kutojua taratibu za uchaguzi ndani ya chama hicho, anapata wapi mamlaka ya kutoka public na kulaumu taratibu hizo (asizozijua)? Nilidhani yeye kama kiongozi wa chama kitaifa na msomi aliebobea, angekuwa na busara ya kupata ukweli na kuuchambua kabla ya kusema au kutoa hukumu kama alivyofanya. Hasa maelezo mengi yanapokuwa yametolewa kuhusiana na sababu za kuahirisha uchaguzi huo au kutangazwa kwa matokeo.

  Ni dhahiri kuwa, kama uchaguzi ulikuwa una makosa mengi, hata uhalali wa matokeo unapotea. Hakuna haja ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mchafu. Hivyo ni vyema kuchunguza na kujiridhisha kuwa tuhuma za uchafu wa uchaguzi huo hazipo, ndipo kuyatangaza matokeo hayo.

  Vile vile, sioni unazungumzia chama kuwa driven kwa tribe gani, ya Dr. Slaa alietangaza au ya nani hasa?
   
 18. O

  Orche Senior Member

  #18
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na Dr. Slaa kuwa matokeo hayo yanaweza tu kuwa halali katika chama cha mafisadi na si chama makini kama CHADEMA. Sababu zilizotolewa zinatosha kabisa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wowote wa watu makini na lazima ufanye uchunguzi makini ili kujua chanzo cha matatizo na hatua nzuri ya kuchukua hivyo miezi sita ni sawa.
   
 19. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh...kweli Chadema sasa hivi iko juuu....
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Chadema inafilisika tu...!
   
Loading...