What if Freeman Alkaeli Mbowe was Compromised?

DALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
2,259
Reaction score
4,691
Amani iwe kwenu!

Najiuliza tu kama binadamu wa kawaida. Kule Afrika ya kusini ilitokea, kabla ya Nelson Mandela kuachiwa huru hadharani kulikuwa na mchakato uliopelekea yeye kuachiwa.

Watu kama Oliver Tambo na wapinagaji wengine waliokuwa nje hawakujua kwamba tayari Mandela alikuwa na majadiliano na Botha wakati ule na sehemu kubwa ya mjadala ulishafikia hatua ya makubaliano.

Mandela alitolewa kule Robben Island alipokuwa anatumikia kifungo chake na kupewa nyumba Cape Town ambapo alihudumiwa kifalme chini ya ulinzi mkali.

Kutoka pale, aliweza kwenda kwenye majadiliano kisirisiri na kupokea wageni kutoka upande wa serikali waliokuwa na kazi ya kufanya majadiliano juu ya mustakabali wa wazungu na mali zao pindi Mandela atakapoachiwa huru.

Ikumbukwe kwamba Mandela alifungwa muda mrefu hivyo wapiganaji kama Oliver Tambo ndo walikuwa na ufahamu wa hali halisi ya mapambano na serikali iliogopa kwamba wangepewa kina Tambo madaraka, makaburu wangekiona cha moto hivyo ilikuwa rahisi kujadiliana na Mandela ambaye kwa wakati ule, alishapondeka hasa na kukosa matumaini.

Kwake ile ilikuwa ni a second chance hivyo alikuwa tayari kuachia uchumi mikononi mwa makaburu huku yeye akishikilia bendera na kuwashashiwi weusi kuwasamehe makaburu.

Pamoja na kwamba ni jambo jema, ila bado najiuliza ile haraka ya Freeman Mbowe kwenda ikulu hata kabla ya kutulia angalau?

Sina uhakika kama alipata hata nafasi ya kushauriana na viongozi wa chama chake kwa ukaribu kujua hali halisi na kujenga msimamo wa pamoja?

Kwanini alienda peke yake?

Sina maana ya kwamba simuamini ila kwenye siasa hakuna ajali.

Hivyo najiuliza tu.

Naomba muongozo.
 
Unaweza kwenda ikulu ya nchi kuonana na rais kwa kujiamulia?.Naamini tofauti na rais mwenyewe kuagiza mtu aende hakuna sio mbowe mwenyewe wala mtu mwingine ambaye angeweza kumpangia mbowe safari kujipeleka ikulu.

Sasa jiulize kama hakuna anayeweza kujipeleka wito wa mbowe kwenda ikulu utakua umetoka wapi?.Bila shaka unajua wito ulitoka wapi sasa niambie ni nani mwenye jeuri yakukataa wito wa rais wa nchi ata kwa sekunde.
 
Ondoka hapo ni seat ya VIP! Kakae kule nyuma wanapokaa kajamba nani wenzako. Kenge wewe!
Kuongoza harakati ni kazi ngumu hasa kama unaojaribu kuwapigania hawaoni hata kama wanahitaji kupiganiwa.
Kuna muda watu wanaona to hell na upambanaji maana watu wenyewe hawana habari
 
Tatizo Ni kwamba tuna macho hatuoni. Mbowe kapitia mangapi tukiona?. Alitajwa kwenye madawa, alifunguliwa kesi kwenye mauaji ya akwilina, kachukuliwa ubunge wake refer statement ya museveni, kabomolewa bilcanas, alifungiwa gazetu lake la Tanzania daima yake, kafukuzwa kwenye Jengo la NHC, kaharibiwa shamba lake na DC Byakanwa, akaunti zake zote zilifungwa na pesa zake kuchukuliwa na mwisho kufunguliwa kesi ya ugaidi.

Naomba niulize maswali, wakati manyanyaso yote niliyoyataja hapo juu yanatokea, tulikuwa tunamcheka na kumsimanga na hata kumuita Gaidi. Nakumbuka Kuna kipindi Mbowe alishambuliwa hadi kuvunjika mguu na watu wasiojulikana, lakini tukamdhihaki kwamba alikuwa amelewa pombe.

Maswali yangu kwako.
1. Je Leo Mh Mbowe katoka kaitikia wito wa Rais na kwenda ikulu tunapata wapi uhalali wa kumwambia yupo compromised ?.

2. Je kama Mh Mbowe alishindwa kuwa compromised wakati wa manyanyaso na mateso kipindi Cha awamu ya tano, je anaweza kuwa compromised kwenye kipindi ambacho manyanyaso na mateso yamepungua kiasi?
 
You never know huenda Mama alimuita Ikulu ili kumwomba Msamaha mheshimiwa Mbowe!
Anyway huenda aliambiwa akithubutu kuendelea na madai ya Katiba Mpya safari hii Dunia itamsahau.
 
Kuongoza harakati ni kazi ngumu hasa kama unaojaribu kuwapigania hawaoni hata kama wanahitaji kupiganiwa.
Kuna muda watu wanaona to hell na upambanaji maana watu wenyewe hawana habari

This is true
 
You never know huenda Mama alimuita Ikulu ili kumwomba Msamaha mheshimiwa Mbowe!
Anyway huenda aliambiwa akithubutu kuendelea na madai ya Katiba Mpya safari hii Dunia itamsahau.

Inawezekana
 
Lolote linawezekana!!! …inawezekana pia alitishwa asirudie au kupewa pole au pia kuendeleza majadiliano ….
 
Chadema mkikubali ujinga wa kumvunjia heshma Freeman Mbowe hakika mtakuwa mnafanya kosa kubwa kuliko la kumteua Ngoyai 2015

Kwny Siasa kuna flexibility na tulikuwa tunawaeleza mnatukana sana…
 
Amani iwe kwenu!

Najiuliza tu kama binadamu wa kawaida. Kule Afrika ya kusini ilitokea, kabla ya Nelson Mandela kuachiwa huru hadharani kulikuwa na mchakato uliopelekea yeye kuachiwa.

Watu kama Oliver Tambo na wapinagaji wengine waliokuwa nje hawakujua kwamba tayari Mandela alikuwa na majadiliano na Botha wakati ule na sehemu kubwa ya mjadala ulishafikia hatua ya makubaliano.

Mandela alitolewa kule Robben Island alipokuwa anatumikia kifungo chake na kupewa nyumba Cape Town ambapo alihudumiwa kifalme chini ya ulinzi mkali.

Kutoka pale, aliweza kwenda kwenye majadiliano kisirisiri na kupokea wageni kutoka upande wa serikali waliokuwa na kazi ya kufanya majadiliano juu ya mustakabali wa wazungu na mali zao pindi Mandela atakapoachiwa huru.

Ikumbukwe kwamba Mandela alifungwa muda mrefu hivyo wapiganaji kama Oliver Tambo ndo walikuwa na ufahamu wa hali halisi ya mapambano na serikali iliogopa kwamba wangepewa kina Tambo madaraka, makaburu wangekiona cha moto hivyo ilikuwa rahisi kujadiliana na Mandela ambaye kwa wakati ule, alishapondeka hasa na kukosa matumaini.

Kwake ile ilikuwa ni a second chance hivyo alikuwa tayari kuachia uchumi mikononi mwa makaburu huku yeye akishikilia bendera na kuwashashiwi weusi kuwasamehe makaburu.

Pamoja na kwamba ni jambo jema, ila bado najiuliza ile haraka ya Freeman Mbowe kwenda ikulu hata kabla ya kutulia angalau?

Sina uhakika kama alipata hata nafasi ya kushauriana na viongozi wa chama chake kwa ukaribu kujua hali halisi na kujenga msimamo wa pamoja?

Kwanini alienda peke yake?

Sina maana ya kwamba simuamini ila kwenye siasa hakuna ajali.

Hivyo najiuliza tu.

Naomba muongozo.

Compromise itadhibitishwa huko mbeleni tukiona mabadiliko yanayotia Shaka. Kwa Sasa hakuna ushahidi wa compromise.
 
Chadema mkikubali ujinga wa kumvunjia heshma Freeman Mbowe hakika mtakuwa mnafanya kosa kubwa kuliko la kumteua Ngoyai 2015

Kwny Siasa kuna flexibility na tulikuwa tunawaeleza mnatukana sana…

CHADEMA haiwezi kumvunjia heshima Mbowe kwa kujitoa kwake mpaka leo. Wengi walishindwa harakati wakakimbia ila yeye amebaki pamoja na manyanyaso yote. Wanaomvunjia heshima ni ccm waliodandia na kumshutumu kuwa amejipeleka mwenyewe Ikulu wakati Rais kamwalika mwenyewe.
 
Kwa sasa Huyu ni wa kumwangalia kwa ‘makengeza’ asije tutumbukiza mtoni huku tunaona!
 
Back
Top Bottom