Mkuu umekaa na UTAWALA WA CCM miaka zadi ya 45 hukupata hayo maji sasa unataka MDEE akupe maji kwa muda wa Miaka 2.
Yeye ndiye WAZIRI WA MAJI.?...Biohazard...nadhani mtu aliyebuni kuwepo na kitu kinachoitwa bungwe alitumia busara sana. Sidhani kama wananchi wote tungekusanyika kwenye ofisi ya waziri wa maji au ofisi ya manispaa kupeleka kero zetu. Halima ametumwa na tuliompigia kura anawajibika kwetu 100% hiyo haina ubishi. Kuzungumza bungeni peke yake sio lengo anatakiwa kufuatilia na kutupa taarifa tuliomtuma ili kujua wapi amekwama na tufany nini? anapokaa kimya eti ameongea bungeni haina maana. Magamba kwa miaka 47 walishindwa kufanya na ndio maana tukasema basi na wao. Je na hawa nao tukae kimya mpaka wafikishe miaka 47? Hapana!!
Kinachonishangaza mie ni kwamba unadai umepoteza kura yako wakati ni miaka miwili tu. Bado mapema kumbeza Halima...Kuna mambo magumu sana wanayopitia wabunge wetu hasa wa upinzani.... Wanashindwa kupinga Bajeti yetu ya MAJI, UJENZI nk sababu ya uchache wao sasa cjui unataka wapigane Bungeni ili Makongo juu nayo iwemo kwenye mgao wa kupata maji katika bajeti?
Mie nadhani Fungu lenu huwa linakuwemo kwenye bajeti ila kuna mambo mawili huwa ambayo Serikali yako DHAIFU inafanya na Halima amekua akifuatilia kwa ukaribu zaidi ya unavyofikiria.
1. Fedha kutumika katika mradi mwingine kwa mapenzi ya Mkurugenzi wa Halmashauri. yani Re allocation
2. Fedha kutokufika katika Halmashauri husika.... Hii kasumba inanifurahisha sana... Wadau wanasema katika Miradi mingi fedha zinazofika katika Halmashauri hata kfikia ROBO ya fedha kamili iliyoainishwa kwnye BAJETI ni ishu.
LAWAMA ITUPIE WIZARA YAKO HIYO na BAJETI DHAIFU pa moja na watendaji DHAIFU wa HALMASHAURI
inawezekana Halima sio Waziri wa Maji, je ni Waziri wa migogoro ya Ardhi Kinondoni?
Hujapata Maswaibu ya ARDHI ndugu yangu.
ARDHI ndo ilikua chanzo cha VITA kila Mahala duniani. NDULI IDD AMIN tulipigana nae kwa kusingizia ARDHI dont mess with ARDHI
Watu wamepigana na Kutoana roho TEGETA kisa ARDHI.
Sidhani kama Kusambaa kwa maji kunaweza kusababisha MAUAJI hapa Mjini ndugu.
Ndgu wanalogana na Kuuana kisa ARDHI.
Pliz usiongee chochote kuhusu ARDHI
Angalia Wafugaji na Wakulima kule kilosa na Rufiji wanagombana kisa nn--- Je ni Maji ya Mto au Ardhi?
Ardhi ni sensitive kuliko Maji... Let her shout
Mkuu hapa Umejibu Maswali yake yote.
...Dogo usidhani kuwa hilo bunge huwa hatufatilii tunaelewa kila kinachoendelea huko bungeni na hata hivyo vikwazo wanavyopata kwenye hizo bajeti tunaelewa. Haimaanishi kuwa ndio mwisho wa yeye kama mbunge aweke mikono nyuma akae chini. May be nikupe ushauri tu dogo unaweza kuacha jazba za kitoto yeye kama mbunge hukutananna madiwani na kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake hapa ndipo nguvu na busara ya mbunge inapoonekana. Hata huyio mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni anapokuta mbunge na madiwani wako firm usitegemee kama ataleta ujinga.....kwani akiongea kule mjengoni akaonekana runingani ndio basi???Mie nashangaa utadhani Halima huwa anashangilia kupitisha Bajeti ya MAJI na UJENZI
...Dogo usidhani kuwa hilo bunge huwa hatufatilii tunaelewa kila kinachoendelea huko bungeni na hata hivyo vikwazo wanavyopata kwenye hizo bajeti tunaelewa. Haimaanishi kuwa ndio mwisho wa yeye kama mbunge aweke mikono nyuma akae chini. May be nikupe ushauri tu dogo unaweza kuacha jazba za kitoto yeye kama mbunge hukutananna madiwani na kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake hapa ndipo nguvu na busara ya mbunge inapoonekana. Hata huyio mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni anapokuta mbunge na madiwani wako firm usitegemee kama ataleta ujinga.....kwani akiongea kule mjengoni akaonekana runingani ndio basi???
Ameshiriki vikao vya bunge na amehusika kataika kuibana serikali ililete maendeleo.
halima mdee kama mwakilishi wa wana kawe ndio mwenye haki ya kuiuliza serikali imefanya yapi pale jimboni kawe kuanzia uhuru mpaka leo hii.
Jee Kawe- specifically amefanya nini ili angalau wanachi wamchague tena 2015 pale Kawe...
Amefanya mengi sana huyu dada wana kawe ndio tunaojua
kuna wabunge wangapi nchi nzima mpaka umseme Mdee peke yake? Una lako jambo wewe. Jiulize wewe mwenyewe umeifanyia nini familia yako kwanza. Achana na Halima awakilishe jimbo.
Jee amefanya hivyo... mara nyingi bungeni mimi huwa naona anatetea mambo mengine.... kwanini asiwe kama Ndesamburo kule Moshi....