Wezi wavamia Kanisa Katoliki na kuiba vifaa vya 'Tabernacle'

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,691
Majambazi Yavamia Kanisani na Kuiba Chombo Kinachotumika Kuhifadhia Ekaristi Takatifu......Kwa Mujibu wa Sheria Za Roma, Ukristo Ndo Basi Tena Eneo Hilo

=========

Watu watano wamevamia na kuvunja madirisha ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Malolo na kuiba chombo kinachotumika kuhifadhia ekaristi takatifu (TABERNACULO).

Imeelezwa kuwa majambazi hayo yalidhani chombo hicho kimetengenezwa kwa dhahabu.

Tukio hilo lilitokea juzi, saa 8:30 usiku, baada ya majambazi hayo kuvunja madirisha ya kanisa hilo.

Kanisa hilo ni miongoni mwa makanisa makongwe na yenye historia kubwa hapa nchini, ambalo lilijengwa mwaka 1939.

Paroko wa kanisa hilo, Theophan Membe, alisema siku ya tukio alikuwa Lindi kuhudhuria misa takatifu ya mapadre wa jimbo la Lindi, iliyoongozwa na Askofu wa jimbo hilo Mhashamu Bruno Ngonyani.

Alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kigango cha Malolo, Cleophas Nnonjela, na badaye walitoa taarifa polisi.

Membe alisema parokia ya Malolo ni miongoni mwa parokia zilizotoa wasomi wengi mkoani Lindi kutokana na historia yake.

Alisema kwa mujibu wa sheria za Roma za kanisa hilo, sehemu inayoibiwa Tarbenaculo, ukristo hufa mpaka wahusika walioiba kifaa hicho watakapokiri kuwa wameiba.

Membe alisema baada ya wahusika kukiri kama wameiba, askofu wa jimbo anaondoa dhambi ya mauti kutoka kwa waumini kwenda kwa wezi hao.

Alisema kutokana na kuibiwa kifaa hicho, waumini wa kigango hicho watakosa baadhi ya huduma ikiwemo ibada ya Jumapili, misa ya kila siku asubuhi, misa ya katekista na upigwaji wa kengele zinazoashiria saa kwa waumini.

Alisema katika kipindi hicho huduma za ubatizo, kipaimara, komunio takatifu, kitubio, misa za mazishi, mpako kwa wagonjwa, sherehe za ndoa na masuala yote ya msingi yanayohusu Kanisa Katoliki hayatakuwepo.

Chanzo: Mpekuzi blog
 
Hizi sasa ni laana, unaenda kuiba Kanisani?

Ni ukweli kabisa hivyo vyombo vya. kuhifadhia Ekaristi Takatifu vimetengenezwa kwa Dhahabu safi kabisa. Ila hao wezi watarudisha wenyewe.

Ila hii ya kwamba kwasababu ya kuibiwa chambo hicho ukristu wa sehemu hiyo hufa kwa Muda nadhani chumvi imeongezwa hapo Unless niwe siujui utaratibu husika. Kwamba waumini wa Kanisa hilo watakasa ibada ya Jumapili na mambo mengine kadha wa kadha yaliyoorodheshwa hapo, sijui ila nadhani kuna upotoshaji hapa.

Na hii ya kusema kwa kuibiwa kwa chombo hicho ni mpaka mtu aliyeiba chombo hicho akili kwamba kaiba na kwamba, Itaondolewa Dhambi ya Mauti kwa Waumini na kwenda kwa wezi hao, naona ni upotoshaji mwingine. Kamwe Kanisa Katoliki la Mitume halijawahi kuwa na kitu kama KULIPIZA KISASI huu ni uchochezi wa waziwazi..!

Mkuu Otorong'ong'o MTAZAMO pitieni hapa.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

Hilo ni miongoni mwa makanisa yaliyojengwa na wakoloni, na mara nyingi watu wanaamini makanisa hayo yana hazina kubwa ikiwemo vyombo vya dhahabu kama vikombe vya kwenye ibada, vyombo vya kuwekea mishumaa nk, nadhani hao wezi walihisi hicho kisanduku kilichoibwa kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu
 
Watakuwa ni waamini wenzetu hao, ila watarudisha tu hata wakipeleka kwa sonara lazima atawahoji.
Ipo siku wataiba hadi ile Ekaristi Takatifu.
 
Mtoa uzi kanichanganya juu kataja jina la padri
Ghafla chini lemegeuka likawa Membe sijui ni mimi sijaelewa?au ni yeye haeleweki?nimebaki njia panda
 
Hilo ni miongoni mwa makanisa yaliyojengwa na wakoloni, na mara nyingi watu wanaamini makanisa hayo yana hazina kubwa ikiwemo vyombo vya dhahabu kama vikombe vya kwenye ibada, vyombo vya kuwekea mishumaa nk, nadhani hao wezi walihisi hicho kisanduku kilichoibwa kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu

Mkuu habari ya hivyo vyombo kutengenezwa kwa Dhahabu safi siyo ya kudhani, hiyo ni kweli tupu. Bahati mbaya sina Biblia hapa ningekuwekea andiko linaloamuru vyombo hivyo kutengenezwa hivyo.

Na hiki kimekuwa kikifuatwa Sehemu zote likipokanisa Katoliki.

Wakati napata kipaimara sehemu fulani (Sitataja eneo lilipo Kanisa hilo) Niliweza kuthibitisha hilo Padre alituweka wazi juu ya suala hilo. Kwahiyo hii si tu kwa Makanisa makongwe bali Kanisa lolote linaloitwa Katoliki mahala kokote.

Ninachokipinga hapa ni mtililiko wa habari yenyewe, hebu jaribu kuipitia kwa utulivu.

BACK TANGANYIKA
 
''askofu wa jimbo anaondoa dhambi ya mauti kutoka kwa waumini kwenda kwa wezi hao''. Mmmmmh, Askofu anauwezo wa kuondoa dhambi?
 
Mtoa uzi kanichanganya juu kataja jina la padri
Ghafla chini lemegeuka likawa Membe sijui ni mimi sijaelewa?au ni yeye haeleweki?nimebaki njia panda

Mkuu hakuna ilipochanganywa....Paroko anaitwa Padre Theophan Membe....siyo huyu Membe joka la mdimu
 
Mkuu habari ya hivyo vyombo kutengenezwa kwa Dhahabu safi siyo ya kudhani, hiyo ni kweli tupu. Bahati mbaya sina Biblia hapa ningekuwekea andiko linaloamuru vyombo hivyo kutengenezwa hivyo.

Na hiki kimekuwa kikifuatwa Sehemu zote likipokanisa Katoliki.

Wakati napata kipaimara sehemu fulani (Sitataja eneo lilipo Kanisa hilo) Niliweza kuthibitisha hilo Padre alituweka wazi juu ya suala hilo. Kwahiyo hii si tu kwa Makanisa makongwe bali Kanisa lolote linaloitwa Katoliki mahala kokote.

Ninachokipinga hapa ni mtililiko wa habari yenyewe, hebu jaribu kuipitia kwa utulivu.

BACK TANGANYIKA

Mtiririko upi unaokuchanganya mkuu??
 
Kylie eleison, Christe eleison
Lamb of God who takes away the sins of the world, have mercy on us........
Agnus Dei, qui tollis peccatta Mundi, miserere nobis..........
 
Novena ili warudishe vyombo/wajisalimishe inaanza lini?
 
Kylie eleison, Christe eleison
Lamb of God who takes away the sins of the world, have mercy on us........
Agnus Dei, qui tollis peccatta Mundi, miserere nobis..........

Ora pro nobis
 
Ukisikia binaadamu aliyechoshwa na maisha na ana hamu ya kufa na kamwe mwili wake usikaonekana na mwanadamu yoyote ndo hao sasa.kwel kabsa nyumba ya Mungu binadamu unadhubutu kuiba?
 
Hizi sasa ni laana, unaenda kuiba Kanisani?

Ni ukweli kabisa hivyo vyombo vya. kuhifadhia Ekaristi Takatifu vimetengenezwa kwa Dhahabu safi kabisa. Ila hao wezi watarudisha wenyewe.

Ila hii ya kwamba kwasababu ya kuibiwa chambo hicho ukristu wa sehemu hiyo hufa kwa Muda nadhani chumvi imeongezwa hapo Unless niwe siujui utaratibu husika. Kwamba waumini wa Kanisa hilo watakasa ibada ya Jumapili na mambo mengine kadha wa kadha yaliyoorodheshwa hapo, sijui ila nadhani kuna upotoshaji hapa.

Na hii ya kusema kwa kuibiwa kwa chombo hicho ni mpaka mtu aliyeiba chombo hicho akili kwamba kaiba na kwamba, Itaondolewa Dhambi ya Mauti kwa Waumini na kwenda kwa wezi hao, naona ni upotoshaji mwingine. Kamwe Kanisa Katoliki la Mitume halijawahi kuwa na kitu kama KULIPIZA KISASI huu ni uchochezi wa waziwazi..!

Mkuu Otorong'ong'o MTAZAMO pitieni hapa.

BACK TANGANYIKA
!

Sheria ya kanisa namba 897 inasema: The most venerable sacrament is the blessed Eucharist in which Christ the Lord himself is contained, offered and received, and by which the church continually lives and grows... Sheria ya kanisa namba 898 inasema, Christ's faithful are to hold the blessed Eucharist in the highest honour...Hivyo turudi kwenye mada yetu dhambi uliyofanyika hapo ni dhambi ya kukufuru yaani sacrilege.Sasa hii dhambi inategemeana nani kaifanya kama ni Shemas,padre au askofu, mlei wa kawaida au mpagani asiyejua maana ya Ekaristi hapo adhabu zitatofautiana. Sheria ya kanisa namba 1367 inasema kama aliyefanya kosa hilo ni shemas, padr au askofu basi adhabu yake nikuvuliwa ukleri nakufanyiwa excommunication yaani kutengwa na kanisa kwa lugha nyepesi. Lakini kama ni walei basi wanapoteza haki fulani kadiri ya sheria ya kanisa namba 1335. Tukumbuke hii dhambi ya kukufuru Ekaristi takatifu ruhusa ya kuiondoa hutoka Roma isipo kuwa katika hatari ya kufa padre yeyote huweza kuiondoa. Sheria ya kanisa mamba 1357.Turudi kwenye mada, kwavile haijulikani ni nani aliyefanya hivyo basi busara ya kichungaji imetumika kwanza jambo lililofanyika ni kubwa, haiwezekani mtu afanye bila kuwa na picha na ramani ya kanisa husika hivyo wanafungiwa wote kwanza ili uchunguzi ufanyike na kisha mambo yatarudi kwenye mwenendo wake wa kawaida.Kwavile jambo lenyewe linahusu matakatifu bac wasingeacha kama kijatokea kitu, nilazima kuonesha kwa vitendo kwamba kilichofanyika siyo kitu kidogo nachakawaida. Kwa kifupi ni hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ninavyofahamu Kristo unakaa ndani ya mtu anayemwamini Yesu Kristo, na kamwe hauwezi kuibiwa kwa mtu kuiba chombo cha kuhifadhia ekaristi.

Halafu inakuwaje kuiba aibe mwingine halafu dhambi iwe juu ya waumini?

Wakristo tuamkeni, tusome Neno la Mungu na tulielewe na kisha tuachane na mapokeo yasiyo sawasawa na Biblia
 
Biblia ipi unayoisema wewe isiyo na haya mambo??watu hawajakurupuka na wala sio yote juu ya mapokeo tu...haya ni maagizo toka ktk maandiko matakatifu
Mathayo 26:26-29 Yesu anawaagiza wanafunzi wake anawaambia

"Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate,akaubariki,akaumega,akawapa wafuasi wake akasema..,twaeni mle;huu ndio mwili wangu....27:Akakitwaa kikombe,akashukuru,akawapa,akisema nyweni wote ktk hiki,kwa maana hii ndio damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi...Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"

Huu ndio msingi wa Ekaristi takatifu,yaani mwili na damu wa Yesu ktk maumbo ya mkate na divai,hii ni juu ya IMANI na siyo Propaganda
 
Nionyeshe panaposema ekaristi ikiibiwa ukristu umeibiwa
 
Back
Top Bottom