Wezi wananifilisi

M16_kwaoz

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2017
Posts
247
Reaction score
474
Habari wanajamvi...

Kwamuda wa mwaka na miezi kadhaa,nimekuwa nasumbuliwa na wezi kuiba kwenye sehemu ninapofanyia shughuli zangu za uzalishaji wa kipato cha kila leo.

Ninafanya shuguhuli za bustani ya mazao ya kilimo haswa michikichi na miti(matunda) na ya kawaida..Wezi wamekuwa wakiniibia mbegu kila wanavyojisikia kufanya hivo na nimejitahidi kufanya mbinu kadhaa ikiwemo kuripoti polisi bila mafanikio,kuweka waganga kadhaa napo sijafanikiwa maana dawa zao hazijafanya kazi,kuweka walinzi wa kampuni na wamasai napo hakujaleta mafanikio yoyote.

Tafadhali,kwa yoyote anayeweza kunisaidia mbinu mbadala nitashukuru sana. Imefikia hatua nashindwa kuendeleza shughuli hii kwani kila ninapopata mbegu hizo,wezi wanaziiba wanavyojiskia.
Natanguliza shukrani.
 
Hakuna mganga nchi hii wala dunia hii akusaidie wakati yeye menyewe hawezi kujisaidia ana maisha magumu mpaka kwenye meno
 
Kwanza achana kabisa na kitu kinaitwa waganga.. Maana hao watakufilisi na hata kukugombanisha na watu
Watakuwekea masharti magumu ili wajivue lawama madawa yao feki yakibuma.. Siku hizi uganga umekuwa ni utapeli
Nashauri
1. Funga ving'ora vile vya solar wakisogea tu vinapiga kelele
2. Tega mitego ya kamba na ya mashimo
3. Tega upupu
4. Nk
 
Hapo kwa mganga utaenda kuibiwa kwa mara nyingine tena🐼
Hakuna mganga nchi hii wala dunia hii akusaidie wakati yeye menyewe hawezi kujisaidia ana maisha magumu mpaka kwenye meno
Shida yenu mnajifungia hapo Kinondoni mkijua mambo ya mjini tu, hii nchi kubwa.

Kuna mzee ana shamba lake jamaa alimuibia ndizi alivyokata mkungu asubuhi ile akaupeleka nyumbani kwake. Kufika kule akatua chini mkungu ukatoa sauti na kumuuliza mbona umepitiliza kwetu. Yule bwana ikabidi aubebe ampelekee mwenyewe na alipofika akujieleza sana alidai alikuta mkungu umeanguka amewasaidia kuwaletea na mmiliki halali akatoa shukrani. Bila drama, bila kuumizana wala kuleta taharuki.

Ukienda mikoani ukazunguka vijijini utajionea mwenyewe, upande wa kulia shamba moja mahindi yameibiwa shambani, upande wa kushoto hata lililoanguka kwa upepo halijajibiwa linaliwa na ndege. Kasoro tu wanafunzi wa shule ndio wagumu kudhibitiwa.
 
Sasa ulikuwepo?
 
Uchawi upo unafanya kazi, shida ni kumpata huyo mganga mwenyewe..
Mzee hapo ni kutega mitego kama anodi ama komando kipensi, ama fuga mbwa, shughuli umeimaliza
 
Weka mtu eneo la kazi mkuu aishi huko awe mbabe na mbwa pia fuga Kisha camera kama utaweza uzionni muhimu pia kulinganisha na uzalishaji wako
Shukrani mkuu..ingawa kwa nature ya eneo ilivyo,camera inaweza isiwe msaada mkubwa sana kukomesha wezi..kuhusu kuweka mtu wa kuishi hapo,walishakuwepo zaidi ya watatu na bado matukio hayajakoma.
 
Nitafute pm,nitakupa dawa ambayo mtu akiiba si ataacha nyayo? Unaifunika kisha nakuja mimi naitengenezea dawa,huyo mwizi eidha atawehuka,kama sio kufa kabisa
 
Nitafute pm,nitakupa dawa ambayo mtu akiiba si ataacha nyayo? Unaifunika kisha nakuja mimi naitengenezea dawa,huyo mwizi eidha atawehuka,kama sio kufa kabisa
 
Samahani mkuu,naweza kumpata huyo mzee?
 
Hapo inabidi uingie mwenyewe mzigo na wati wako kadhaa mkikamata mmoja mmtolee mfano na onyo ili wenzie wakisikia na kuona wakae mbali na hiyo bustani
 
Shukran..nitajaribu hapo nione nitachoambulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…