Usiku wa tar. 19th October, walinifanyia kitu mbaya hao wezi! waliipukutisha Toyota Raum yangu, hata hamu sina! Police waliniuliza "kijana unatakaje?" Sikujibu!
Nilikuja hapa nikaweka uzi wangu wa masikitiko yangu, watu wakanipa pole, nikaahidi sintasamehe mtu, kuwa nitadeal nao kivyetuvyetu! Na tayari "mtaalamu kanipa proposal yake ya kwanza, KUWATANGULIZA MMOJA MMOJA!"
Hii imentisha, nimempa proposal yangu, cha kuwafanya wabaya wangu, ameikubali! Leo hapa ofisini nimeshajaza EMERGENCY LEAVE ya 2 days, kesho ntashinda sokoni TANDALE kukusanya mahitaji ya "mtaalamu wangu!" Baada ya hapo napanda basi UBUNGO, safari!!
Nitaleta mrejesho baada ya kurudi kutoka kwa "mtaalamu"