Wewe Unakumbuka nini.....?

kutoroka darasan na kwenda kula matunda.niki kumbuka hii hua na cheka sana:smile-big:
 
kufuta stamp za Posta kwa kutumia sabuni na ka kipande cha godoro ili kutuma barua bure from boarding school to home.. Halafu barua yenyewe inaomba TMO or EMO
mkuuuuuu....kwi kwi kwiiiiih...
 
hiyo 13 daaaaaah...
 
Namkumbuka mdudu flani hivi,ukimwambia Arusha wapi anaelekeza mkia,na kingine ukipoteza kitu unajaza mate mkononi af unayapiga
hahahaaaaaaaaa,hiyo ya kuweka mate umeniteka mbaaali mkuu!
 
1.Kupakaa mate kwenye ugoko unaporudi nyumban jion ili usionekane mchafu ukapigwa.
2. Kulilia kununuliwa nguo mpya kila inapokaribia sikukuu.
3. Kugawana kisheti kimoja au Andaz 1 watu kama kumi hivi.
au kitumbua au kiazi usipowagawia wanakutenga kesho yake!
 
Kukaanga mahindi halafu unayaloweka kwenye kidumu unaenda nayo shule
 
1: Kugawa andaz au chochte then ukimaliza lako unawadai uliowapa kwa kilio
2:Kufunuana nan hajavaa chupi (nilikuwa mstari wa mbele kufunua wenzangu ila kuna siku nikagoma kuwafunua huku nawatetea. wajanja wakagundua na mi sjavaa. Acha nikimbizwe bana duh! )
3:Kueka kioo chini ya miguu kumchungulia mwenzio(hasa boys)
4:Njaa ikiuma Xul nalia eti naumwa tumbo ili niruhucwe kurd hm.
 
hiyo namba 3 imenivunja mbavu daaah!nilifanya hvo nikapelekwa kwa mwlmu,nilitandikwa balaa
 

Hiyo no 8 mmh!
 
nelly nely umenipa raha. Kuna jamaa mmoja alinifanyia ivo, tulimkimbza hadi kwao. Sasa kagroup kangu kote hakuna aliekumbuka njia
 
kuweka kioo chini ya madawati ya wasichana na kutizama details zote.
 
Unanikumbusha mbali,kuna jamaa alikuwa anazunguka darasa zima kumbe anajamba kimya kimya mwisho darasa halikaliki.
 
1. kuweka mkaa mlangoni ili mwalim akipita asahau adhabu aliyopanga kutupa
2. kusahau ufagio wa chelewa,unakwenda unaiba mbilimbili hadi unaukamilisha
3. kusimuliana muvi za kihindi na kinigeria darasani.mtu anaimba mpaka wimbo asee
4. kung'atiana ice cream
5. kumgaya mtu mchoyo.
6. Kuitwa mchumba,mume au mke na watu wazima au wazee
7. kucheza kwenye majani yanayowasha,kuoga jion unawashwa zaid
8. kugoma kuoga
9. kila siku kwenda kwa jiran kucheza.wao hawaji!
10. Wale wambea,marafiki na watoto wa walim,wale wa naenda kukusemea!wale tulikuwa tunawapa kichapo kila siku kwenye njia ya kwenda hom
 
kidali pooh,kombolela, kam:faint2:ba ya mkonge kuwa mkanda
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…