Wewe Unakumbuka nini.....?


Hiyo namba saba tulikuwa tunaitwa NJUKA, au SALAMANDA au UNYOYA dah
 
Kuandika jina kwenye kipand cha kalatasi na kuki2mbukiza kwenye bomba la peni
 
kunawa miguu asubuhi kabla ya kwenda shule!!
 
Kuweka blueband kwenye chai kwa kujificha ili mama asinione
 
1.Kupakaa mate kwenye ugoko unaporudi nyumban jion ili usionekane mchafu ukapigwa.
2. Kulilia kununuliwa nguo mpya kila inapokaribia sikukuu.
3. Kugawana kisheti kimoja au Andaz 1 watu kama kumi hivi.
 
Namkumbuka mdudu flani hivi,ukimwambia Arusha wapi anaelekeza mkia,na kingine ukipoteza kitu unajaza mate mkononi af unayapiga
 
1.Kumpiga mjusi halafu mnakimbiza kunywa maji kabla mkia wake haujaacha kuruka ruka.
2.Kutengeneza mpira wa nage kwa kutumia soksi za shule...
3. Kuvaa soksi za pundamilia zilizotoboka kwenye kisigino
4. Raba maarufu za losso na viatu vya chachacha...
5.kubeba madaftari ya shule na mifuko ya rambo
6 kupiga passport size yaani kuosha maeneo muhimu tu ya mwili nikiwa boarding sababu ya baridi au uhaba wa maji.
7.kuweka maharage au makande sukari blueband na peanut butter.
8.mchezo wa heshima ya ndege au mzinga bomoa...acha kabisa unaweza kubutuliwa ngumi ukaona nyota.
9.kuogelea mtoni kutwa nzima..then nakaa juani nakauka na ki.c.h.u.p.I changu narudi tena kuogelea..
10.kupanda kwenye miti ya miembe na mizambarau kama nyani
11.nikipigwa na kakaangu sinyamazi kama bi mkubwa yupo karibu mpaka aje akute nalia na kama yupi mbali sifuti machoz mpaka yanakaukia mashavuni ili bi mkubwa ajue nlipewa kipondo.
12.kubana sadaka kila jpili kwa ajili ya maandaz shule
13.kusingizia naumwa tumbo la period nisifanye mazoez asubuh boarding.
 
kufuta stamp za Posta kwa kutumia sabuni na ka kipande cha godoro ili kutuma barua bure from boarding school to home.. Halafu barua yenyewe inaomba TMO or EMO
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…