Western union- msaada kuhusu hili la kitambulisho

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
667
957
Wakuu nipo Mkoani Mwanza kwa safari ya ghafla. Bahati mbaya nimesahau Leseni na Kitambulisho cha Kura Dar es salaam.

Sasa nimetumiwa pesa kupitia Western Union, nimekwenda Bank na kujaza fomu ila wamegoma kabisa wanadai Leseni na Kitambulisho.

Msaada kwa aliyewahi kutana na hii kadhia kama mimi,na wenye uelewa kwa hii kadhia.
 
Sharti la kutoa pesa ni kuwa na kitambulisho.Kusahau sio sababu inayokubalika. Chukulia mfano upo Airport unataka kusafiri nje ya nchi halafu kwenye passport control useme nimesahau passport.Je safari itakuwepo?Mkuu wapigie jamaa zako wakutumie kwa basi za abiria. Hamna shortcut.
 
Back
Top Bottom