wenzangu m'meiona hii toka itv??nimestushwa sana!!

Yap hata mimi nilimuona siju kama afya yake itakuwaje miaka mitano ijayo, twaweza chagua mwingine kama nigeria.
 
Mweledi Balantanda. Umesema hapo ktk bold kuwa Bill na Chelsea walimkampeinia Hilary kuomba ridhaa ya kupitishwa kugombea. Huwa inaishia hapo. Likifika suala la uraisi wa nchi ni CHAMA kuhusika kwa mtiririko muktadha. Huwezi kuniambia kwamba RIZ1 na SALMA ni vinara wa kumnadi mgombea wa CCM. ina maana chama hakina mechanism yeyote zaidi ya hao wawili? Kama si maslahi kwa famili ni nini basi? inaonesha mgombea na familia yake hawakiamini chama kwamba kinaweza kusimama naye mpaka ashinde? Kuna methali inasema whats goes around comes around just as to say mwenda tezi na OMO marejeo NGAMANI.

Wanachikifanya akina kikwete family ni ufuska wa kisiasa yaani wanabaka mchakato rasmi wa kampeni kwa kutumia funds za umma kujiimarisha madarakani. Najua wanatamani katiba ingekuwa upande wao lakini SISI wananchi tunasema Tanzania ilikuwepo na itaendelea kuwepo bila wao. Nimependa responce yako ya kumshambulia mtoa hoja kuwa kwa nini aseme KIKWETE hatashinda. Sidhani kama ungesema hivyo kwa slaa ama lipumba.

Ila rais wangu yupo kwenye hali mbaya. anapaswa kumsikiliza daktari wake sasa kuliko kipindi kingine chochote.

Well said.
 
Chelsie hakuwahi ku campaign kwa Hillary hata siku moja, japo alikuwa anaongozana naye. Bill Clinton alikuwa ana campaign kama raisi msataafu akiwa kwenye chama cha Democrats.

Mkuu afandhali umeliweka hili katika mrengo wa kueleweka. Watz tunashindwa kuelewa Tz si US na tumeshindwa kufikia maendeleo tuliyojipangia kwa miaka 50. Sasa umaskini wa US na Tz ni sawa mpaka Riz na Salma wawe na uwiano wa Chels na Clinton? Kwani CCM ni Democrats siku hizi? I'll continue to wonder!
 
Hi wana JF,

Mimi nimeangalia TBC jana kwenye taarifa ya saa 2.00 usiku.
Ni kweli JK anaonekana yuko hoi. Sina uhakika kama atazimaliza mbio hizi za Kampeni. Nilimwangalia nika-note hiyo hali kuwa JK hayuko kwenye hali yake kama alivoanza pale Jangwani yaani Kasi zaidi,Nguvu zaidi na Ari zaidi. Ukweli ni kwamba JK AMECHOOOOKA!!!!

KWAMBA ANAONEKANA USO UMEFUBAA(Dalili ya mtu mgonjwa) NA SAUTI YAKE INASIKIKA NA MIKWARUZO(hoarse)AU KAMA ANAMFUA MAKALI!!!

Kitu ambacho nilijiuliza baada ya kumwona JK katika hali hiyo ni Je,ni ugonjwa uliomwangusha Jangwani au ni uchovu wa safari za Kampeni???Bado sijapata majibu ila mimi nafikiria haya yafuatayo:

  • Kwamba the President is very sick. Anachofanya sasa ni kujikaza tu ili kuondoa hofu kwa Watanzania kuwa yeye si mgonjwa ili kufuta ile hali iliyotokea pale Jangwani.
  • Kwamba Daktari wake ameshindwa au anaona aibu kumshauri JK apumzike.
  • Kwamba JK ana hofu kama atakubali kupumzika kwasababu za kiafya basi Dr. Wilbroad Slaa atampiku na kuichukua Ikulu.
  • Kwamba JK anategemea ushauri wa Kigagula Sheikh Yahya Hussein kuwa amemwekea kinga isiyoonekana kwa maana ya JINI.
Sasa hofu yangu kuu ni hii hapa:

  1. Nahofia kuwa yasije yakatokea yale yaliyomkuta marehemu Rais Yar'dua wa Nigeria aliyefia nje ya nchi akipata matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
  2. Sheikh Yahya alitoa utabiri wake wa kima-jini akasema UCHAGUZI wa mwaka huu hautakuwepo au uta ahirishwa kutokana na kifo cha mmoja wa wagombea wa kiti cha Urais!!!GOD FORBID.
  3. Sheikh Yahya pengine kwa mapepo yake ya ki-majini anajua kabisa kinachoendelea na mwisho wake. Na ili utabiri wake utimie ameamua kumdanganya JK kuwa amemwekea ulinzi usioonekana kumbe ndiyo ana-mmaliza!!!!
Mimi simo najitoa kabisa. Kama litatokea la kutokea kabla ya Oktoba 31 basi CCM,Familia ya JK,Daktari wake na Sheikh Yahya watasitahili kubeba lawama kwa uzembe,uongo na unafiki ambao wameuonyesha kuhusu kusimamia AFYA YA JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!!

USHAURI WA BURE KWA JK,FAMILIA YAKE NA CCM: JK apumzike kabisa na kazi ya Kampeni amwachie mgombea mwenza Gharib Bilal ili apambane na Dr. Slaa,Prof. Lipumba,Rungwe, Mugahwa n.k.

Kama Bilal atashindwa kuuza sera za CCM za BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA basi CCM wapishe ikulu ili CHADEMA waweze kuingia mjengoni na kuleta mabadiliko tunayoyasubiri kwa hamu.

Wasalaam.
 
nimemuona JK leo kwenye taarifa ya habari akihutubia sehemu flani..yaani kachoooka, sauti yake as if kabanwa na mafua kwa wiki ka 7 hivi, isitoshe ile smile yake ilipotea kabisa, nadhani ingekuwa ridhaa yake wiki kampeni zingekuwa zinaisha, nahisi huyu mmzee atakuwa na msongo sana wa mawazo, ila wasi wangu ni kwamba sijajua bado kwamba huyu JK ATAZIMALIZA KWELI HIZI MBIO ZA KAMPENI,? nauuliza ni kipi hasa kinamtatiza? au ni hii ripoti ya synovate? AAGH DK MABUNDUKI WE LIENDELEZE TU KUSONGESHA...HUYU JK MUDA SI MREFU ATAKUWA CHALIIIIIIII..WE SUBIRIA TU

Samahani, inaonekana lile funzo kutoka kwa wazazi kwamba usicheke wagonjwa au walemavu hujalipata wewe. Au hujasikia hii, "Hujafa hujaumbika"?
 
Hiyo nyekundu ndo ilani MPYA ya CHAMA CHA....:confused2:
 
Qulfayaqul na redSilverDog naona mmeni'kot' vibaya! sijamanisha hiyo ''CHALIIIIII' kwamba atakufa,lah/hapana ni kwamba uchovu wa mwili alionao unaweza kumletea matatizo zaidi na kiutu tu ni kwamba inambidi atake rest for sometime....hembu cheki hiyo reply HAPO JUU na maono ya ''MAKOYE2009'' kachambua vizuri mno,comment yake ni awesome na outstanding, hii hali sie tunaoona kwa jcho la tatu mbeleni huenda kukawa na matatizo(simaanishi kifo) kwa huyu JK utake usitake. WELDONE MAKOYE:mad2::playball::confused2::becky:
 
Wana JF, bila kupoteza maana ya ujumbe wa Dingiswayo, nafikiri methali hizi mbili zimetumika isivyo, " whats goes around comes around " na "mwenda tezi na OMO marejeo NGAMANI." Am standing to be collected, lakini siamini kabisa kwa msemo wa "whats goes around comes around" ni sawa na mwenda tezi na OMO marejeo NGAMANI. Methali au misemo hii miwili ina maudhui ya aina mbili tofauti hasa tukiutafsiri ule wa kiingereza kwa kiswahili. Maudhui ya msemo wa kwanza " what goes around comes around - utendayo mwenzio ndiyo yatakayokuja kukupata ( tafsiri isiyo rasmi), ni kuwa kwa lolote umtendalo mwenzie basi utegmee kutendwa vivyo hivyo hata kama sio na uliyemtenda, msemo huu ni sawa na ule " To give someone the test of his/her own medicine (hii ni mtazamo wangu), na maudhui ya msemo wa pili yaani " mwenda tezi na omo marejeo ngamani-ni kuwa pamoja na kukuru kakara zote mtu azifanyazo basi ipo siku atarejea tu katika shina lake, ni sawa na kusema ng'ombe avunjikapo mguu hurejea zizini!
 
Kwa kweli namsikitikitikia Rais wangu wa awamu ya nne JK. Nilitamani sana aachie ngazi kwa heshima, hasa afya yake ilipoingia mgogoro, lakini naona ana kiburi. Ni ujinga kupingana na afya, hakuna spea hata kama ana hela kiasi gani.

Inafaa apunguze mizunguko kwani atajimaliza tu kabla ya Oktoba. Mbaya zaidi ni hatashinda, angeshinda walau ingemfariji. Hawezi kushinda kwa sababu hana sifa ya kushinda baada ya kutanguliza familia yake na ubinafsi.

CCM sio NGO ya familia yake. Kwa vile yeye, Salma na Ridhi wamelivalia njuga hili suala la kumrudisha ikulu, ameonesha madaraka haya ni kwa faida ya familia. Hatukatai familia yake na ndugu zake kumuunga mkono kwa namna yoyote, ila sio kwa kutumia rasilimali ya nchi. Hata kama wakisema ni fedha ya chama, chama hicho kinachangiwa na wananchi. Huyo hafai kuendelea kuongoza nchi yetu.

Haitapendeza afie kwenye kampeni, itapendeza kama wenzake kina Mkapa na Mwinyi akitulia na kutoa ushauri. Kwa vile ameshaanza kampeni, nashauri asitumie nguvu nyingi, atajimaliza kabla ya uchaguzi. Ajiandae tu kupunzika baada ya uchaguzi, hatarudi Ikulu.

Usiwe na shaka atamaliza tu hiyo kampeni kwani hivi sasa tayari ana walinzi wasioonekana kwa macho ya kawaida waliotayarishwa na Sheikh Yahya Hussein.
 
nimemuona JK leo kwenye taarifa ya habari akihutubia sehemu flani..yaani kachoooka, sauti yake as if kabanwa na mafua kwa wiki ka 7 hivi, isitoshe ile smile yake ilipotea kabisa, nadhani ingekuwa ridhaa yake wiki kampeni zingekuwa zinaisha, nahisi huyu mmzee atakuwa na msongo sana wa mawazo, ila wasi wangu ni kwamba sijajua bado kwamba huyu JK ATAZIMALIZA KWELI HIZI MBIO ZA KAMPENI,? nauuliza ni kipi hasa kinamtatiza? au ni hii ripoti ya synovate? AAGH DK MABUNDUKI WE LIENDELEZE TU KUSONGESHA...HUYU JK MUDA SI MREFU ATAKUWA CHALIIIIIIII..WE SUBIRIA TU

Ajuaye Bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama.
Leta hoja ya kisiasa kama unayo, vinginevyo mambo ya kuchoka au la hayo ni ya kibinadamu, hakuna asiyefikwa na uchovu. Wewe huwa huchoki?
 
Nachukia muongozo/itikadi/sera anazoutima Jakaya Kikwete kuongoza nchi lakini sijafikia hatua ya kumchukia yeye binafsi.

Kwakweli nimesikitika sana kwa hali niliyomuona nayo jana wakati naangalia TBC1 taarifa ya habari. Our President is sick, na nnamuombea arudi katika afya yake ya kawaida na kuendelea na kampeni.
Kwasasa nashauri asitishe kampeni hata kwa wiki 2 ili apate matibabu sahihi.

Raha ya kampeni ni ushindani. Akibaki Dr. Slaa, au JK pekeyake, raha ya kampeni itapotea...
Namuombea JK arudi katika hali yake ili aendelee na kampeni zake. Ila sipendi itikadi za chama chake za kulindana.
 
..JK safari za ndani haziwezi. zinamikiki mingi hivyo zinamchosha.

..safari za nje ndiyo zinamfaa zaidi. subirini akishinda, na kuanze safari za nje, muone atakavyonawiri.

..Waswahili wana msemo wao "mchumia juani hula kivulini."
 
Du hata mimi nilimuona jamani jana hiyo alikuwa nadhani kondoa mpaka nikawauliza wenzangu hiome jamaa vipi huyu? anaumwa sauti ya chini.
 
Yawezekana labda kuna msuguano mkali katika matawi ya juu ya vigogo wa CCM,lakini ni vigumu sasa hivi kujua undani wa tatizo mpaka baada ya uchaguzi mkuu.Ila sioni dalili nzuri kwenye kambi ya Kikwete sivyo walikuwa wanategemea kambi ya Chadema.Nguvu za Mama Salma na mwanae hazitoshi kumsaidia ilitakiwa strong CCM mechanism.
 
Back
Top Bottom