wenzangu m'meiona hii toka itv??nimestushwa sana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wenzangu m'meiona hii toka itv??nimestushwa sana!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Sep 20, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  nimemuona JK leo kwenye taarifa ya habari akihutubia sehemu flani..yaani kachoooka, sauti yake as if kabanwa na mafua kwa wiki ka 7 hivi, isitoshe ile smile yake ilipotea kabisa, nadhani ingekuwa ridhaa yake wiki kampeni zingekuwa zinaisha, nahisi huyu mmzee atakuwa na msongo sana wa mawazo, ila wasi wangu ni kwamba sijajua bado kwamba huyu JK ATAZIMALIZA KWELI HIZI MBIO ZA KAMPENI,? nauuliza ni kipi hasa kinamtatiza? au ni hii ripoti ya synovate? AAGH DK MABUNDUKI WE LIENDELEZE TU KUSONGESHA...HUYU JK MUDA SI MREFU ATAKUWA CHALIIIIIIII..WE SUBIRIA TU
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli namsikitikitikia Rais wangu wa awamu ya nne JK. Nilitamani sana aachie ngazi kwa heshima, hasa afya yake ilipoingia mgogoro, lakini naona ana kiburi. Ni ujinga kupingana na afya, hakuna spea hata kama ana hela kiasi gani.

  Inafaa apunguze mizunguko kwani atajimaliza tu kabla ya Oktoba. Mbaya zaidi ni hatashinda, angeshinda walau ingemfariji. Hawezi kushinda kwa sababu hana sifa ya kushinda baada ya kutanguliza familia yake na ubinafsi.

  CCM sio NGO ya familia yake. Kwa vile yeye, Salma na Ridhi wamelivalia njuga hili suala la kumrudisha ikulu, ameonesha madaraka haya ni kwa faida ya familia. Hatukatai familia yake na ndugu zake kumuunga mkono kwa namna yoyote, ila sio kwa kutumia rasilimali ya nchi. Hata kama wakisema ni fedha ya chama, chama hicho kinachangiwa na wananchi. Huyo hafai kuendelea kuongoza nchi yetu.

  Haitapendeza afie kwenye kampeni, itapendeza kama wenzake kina Mkapa na Mwinyi akitulia na kutoa ushauri. Kwa vile ameshaanza kampeni, nashauri asitumie nguvu nyingi, atajimaliza kabla ya uchaguzi. Ajiandae tu kupunzika baada ya uchaguzi, hatarudi Ikulu.
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Dopas, kwa bahati mbaya sana hangeweza kuachia ngazi hata kama angetaka kufanya hivyo. Kikwete kwa hivi sasa ni mateka wa mafisadi na kuendelea kubaki kwake madarakani ndiyo salama yao hao waliomwezesha kuukwaa Uraisi. Wako tayari kumsindikiza Ikulu hata kama ni ndani ya gari linalobeba wagonjwa na kwa kutumia njia zozote zile hata ikibidi kufa mtu. Ndio maana wanasema piga, ua, galagaza, CCM lazima washinde !

  Hata hivyo na wazalendo nao safari hii wameamua kula nao sahani moja na hakuna kulala tena hadi kieleweke. Wananchi tumenyanyaswa, tumepuuzwa, tumeonewa na tumeibiwa vya kutosha na sasa kwa sauti ya nguvu tunasema hapana imetosha, hatukubali. Hivi sasa bado siku 41 CCM inaketishwa benchi na mafisadi woote matumbo moto - angalia wanavyohangaika kuokoa jahazi lakini ukweli ni kuwa wamechelewa.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yah kampeni zinataka uwe fit kweli
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mhhh wewe.........Hebu tuondolee uchuro hapa ebo!!!!!!!!!!..........Ushakuwa Sheikh Yahya mara hii

  Sipendi sana kuchangia 'sredi' za aina hii(za kampeni/uchaguzi0 lakini kauli zako hizi nzio zimenifanya nichangie aisee....

  -Kikwete anatumia haki yake ya kikatiba kugombea uprezidaa bana,hayo mambo ya afya yake anayajua mwenyewe ndo maana akajitosa na kuendelea na kampeni za uchaguzi....Kwa nini unamuita ni mjinga na ana kburi..............kuwa na adabu bana,eti anapingana na afya yake!!!!!,suala la afya yake limeshaongelewa hapa na hata ugonjwa unaomsumbua(kwa mujibu wa madaktari wake na CCM) ni sukari kushuka unaweza ukampata yeyote na wakai wowote(hata wagombea wengine) subiri kampeni ziishe uchaguzi ufanyike ndo uanze kuyaongea haya.............KIKWETE yupo kwenye kampeni na anatumia muda mwingi sana katika safari na kuhutubia mikutano ya hadhara so si ajabu kumuona kabadilika wajihi..........Ni hali ya kawaida kaika kampeni

  -Suala la kushinda ama kutoshinda kwa mgombea yeyote tuwaachie wananchi hiyo tarehe 3 Oktoba(ni sawa na mpira wa miguu,mshindi wa taji hupatikana baada ya dk 90,au 120 au kwa penati,zamani hata kwa shilingi)....Hapo ndo tutajua mbivu ni zipi na mbichi ni zipi.............Ni kigezo kipi kimekufanya uamini kwamba KIKWETE hatashinda ei 'baada ya kutanguliza familia yake na ubinafsi'!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  -Mama Salma,Ridhwani ama mtu yeyote kutoka familia ya KIKWETE anao uhuru wa kumkampenia KIKWETE(kwa taratibu walizojiwekea wao CCM)...............Ni sawa na Bill Clinton na bintiye cHELSEA WALIVOKUWA WAKIZUNGUKA us nzima kumkampenia Hilary wakati akitaka ridhaa ya wana Democrats kumteua awe mgombea urais wa US...CCM tayari wameeleza kwamba hizi ni gharama zao kama chama na si hao tu kuna makada na ndugu kibao wamezunguka Tanzania nzima.....Huu ni mkakati wa ushindi wa CCM ambao ungeweza kubuniwa na kutumiwa na chama kingnie chochote kile......Ndo maana utaona vyama vya CUF na CCM wagombea urais na running mates wao hawazunguki pamoja,wanaenda sehemu tofauti kwa lengo la kuwafikia waTanzania wengi zaidi na kupata kura nyingi....

  -Nani kakwambia atafia kwenye kampeni aiseee...KIKWETE bado ana sifa ya kikatiba ya kugombea kipindi kimoja zaidi,hayo mengine ya utendaji kazi tuwaachie waTanzania waamue kupitia uchaguzi.......Mengine tumuchie Sheikh Yahya & Co......................................................Kwa heri ya kuonana
   
 6. MAWANI

  MAWANI Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shekhe yahaya Yuko wapi? Alipaswa kuongeza nguvu zaidi
   
 7. MAWANI

  MAWANI Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya hayo katiba yetu inaruhusu Mtanzania kugombea urais siyo zaidi ya mara mbili. Lakini haisemi kuwa lazima vipindi vifuatane. Ok? Kwa hiyo Kikwete angeenda Londan, St. Thomas akatibiwa kwa utulivu akiishapona, arejee by then itakuwa ni 2015. Hapo atagombea tena. Kama wa Tz wataona kuwa anafaa, watampa kama wataona hafai, angalau amekaa ikulu kwa 5 yrs. Au siyo?
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nakuunga mkono hebu angalia picha yeke ya jana wakati wa mazishi ya mtoto wa Msekwa kapoteza uzito huu mwili si wake.

  [​IMG]
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Msekwa kafiwa na mwanawe? Huyu ndiye mkemwenzake na Anna abdala? Mbona bi anna haonekani hapa?
  Bila shaka wataarisha uchaguzi kwa kuwa msekwa kafiwa.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Balantanda, kila mtu ana haki ya kugombea lakini katiba hiyo hiyo inataja sifa za mgombea kwa hiyo inaweza kutoa kwa mkono huu na kunyima kwa mkono mwingine. Mfano asiyejua kusoma na kuandika kanyimwa haki hiyo, naweza kusema katiba haimpi haki mtu yeyoye kugombea akiwepo kichaa labda katiba ituambie kichaa siyo mtu.

  Kwani katiba inasemaje juu ya rais mgonjwa hadi rais azimie ashindwe kuamuka ndipo tujue afya siyo nzuri, kama rais anashindwa kuhutubia wananchi wake na kuanguka anguka ovyo ovyo tena hadharani huoni hilo ni tatizo. Halafu elewa katiba haisemi lazima amalize vipindi viwili hata kama ni mgonjwa. Hebu mwangalie tena mtu unayemtetea kama afya yake bado inaruhusu kuongoza nchi yenye watu zaidi ya mil.40,

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  choka mbaya pamoja na kula bata lakini wapi
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  naona kwenye gazeti la mwananchi wanasema kwamba alifika dodoma, lakini baadae alielekea darisalama, kwa sababu hawezi kuhutubia watu walio kwenye mfarakano "yaani madhara ya kura za Maoni ndani ya ccm"
   
 13. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaumwa huyu ndiyo maana badala ya kukampeni Dodoma ameamua kwenda mapumzikoni kwa muda, sijui ni kwa muda gani.
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  story za vijiweni
   
 15. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwani anawahutubia wana CCM peke yao au watanzania wote?
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Habari za CHADEMA kutangulia mbele kidogo kwa kura za maoni hazingempa JK uchovu mkubwa. Kama kachoka mnavyosema, basi naamini walipompa briefing Usalama Wa Taifa walimwambia kipindi hiki "hawataweza kunyosha mambo".

  Kuna watu wengi wanaoipenda nchi huko UWT. Wako wakubwa wachache wa ngazi za juu ambao hula na mafisadi wa CCM, lakini hawawezi wenyewe "kunyosha uchaguzi" na kumhakikishia JK ushindi.
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Haueleweki mkuu wangu Luteni......Sidhasni kama ingekuwa ni tatizo KIKWETE angeruhusiwa kikatiba kugombea urais mwaka huu.....Nilichotaka kusema hapo juu ni kwamba tuwaache wananchi/WaTanzania ndo watoe uamuzi wa kama anafaa kuwaongoza ama la......eti kwa kusema kwamba anaonekana kachoka mnooooooo....

  Ishu hapa si kumteteea Kikwete bali mimi hapa nimeamua kuchangia kutokana na bandiko la pili katika'sredi' hii ambalo ukilisoma vizuri utaona limekaa kipropaganda na kiushabiki bin kiuzushi mnoo....Tuwaache wagombea wote wanadi sera zao kwa wananchi na tuangalie matokeo ya uchaguzi huo baada ya hiyo tarehe 31 Oct
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kamanda nimeiona hiyo.nimekubali mzee amechoka...niko canada sikupata kuiona hiyo live.asante sana
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  MF hata wewe???......hahaaaaaaaaaaa.....Ningekuwa mimi ningeuliza japo kwa PM badala ya kueka bandiko la dizaini hii hadharani....Yaani unauliza Anna Abdallah ni mke mwenzie wa Anna Abdallah......lol....hebu tuacheni basi ushabiki wa dizaini hii ambao si mzuri asilani

  Msekwa ni nani mpaka uchaguzi uahirishwe kwa yeye kufiwa na mwanawe????.......Tuachane na ushabiki ba upotoshaji wa makusudi usio na maana jama............Tuwe makini japo katika siku hizi 40 zilizobaki.....
   
 20. S

  Safre JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Da tumwombee ili Slaa akiingia aone mambo yanavyoendeshwa
   
Loading...