Wenyeviti na meza bado hamjaelewa tu? Waheshimiwa mnangoja nini, eti mnasubiri nini, CCM mtashinda wapi?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Tayari Nchi nzima wananchi WALIO wengi wameshaonyesha muelekeo kuwa wanahitaji Chama na kuondoa UTAWALA kuweka uongozi, CCM ni watawala hawana tofauti na Utawala wa KIFALME au kikoloni,msipoondoka kwa hiari zenu mtabakia kufukuzwa kwenye majukwaa.

Ni wakati muafaka CCM mjirekebishe na kuondoa kiburi chenu kwamba nyinyi ndio nyinyi, hilo limeshapitwa na wakati na halina nafasi, rudini chini jipangeni na kuona wakati sio rafiki tena kwenu, msiilazimishe Tume kuwapa ushindi wa chee, mtawatia kwenye matatizo na wao wakiwasikiliza ni kujitafutia balaa.

CCM kuweni makini sana na kubalini kushindwa ,itakuwa mmesahau ule msemo wa mshindani hushindwa. Nchi nzima upepo unaovuma si wa Chadema wala ACT wala wenginetele, Upepo huu ni wa Tundu Lissu ambae haionyeshi kabisa kuwa na mbadala,wananchi wanaonekana na furaha kutoka moyoni kabisa, jamaa anakubalika vibaya mno,kila anapopita wananchi ni tabasamu tu,hamna bendi wala msanii wala waliovaa sare za vyama ni wananchi katika uasilia wao.

Hongera Tundu Lissu Nchi inahitaji uongozi wako na wanausubiri kw hamu kubwa,usiwasahau mashehe zetu na mapadri wetu waliowekwa kizuini kwa sababu zisizojulikana ambazo CCM na wachunguzi wao wameshindwa kuzifikisha mahakamani.

Wananchi wako pamoja nawe,endelea kuwajenga wazidi kuwa na msimamo usiotetereka wala kuogopa makapi ya nguvu za mtawala CCM.
 
Rais wabunge madiwani wa CCM tamaa zao na ushindi wao unategemea huruma za Tume hawajui mwaka huu ni mwaka wa wananchi kuchagua kiongozi sio tume kuweka mtawala.
 
Lissu azidi kuikanyaga CCM,yaani CCM wanabaki kuchungulia madirishani,safari hii ni mapambano tu,imeshatolewa ilani na mbiu ya mgambo CCM akijitia umbelembele kitakachomkuta asiwalilie polisi.
 
Back
Top Bottom