Siri iliyofichika nyuma ya Sumaye na Lowassa kurudi tena CCM

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
🆕SIRI KIJASUSI ILIYOFICHIKA NYUMA YA SUMAYE NA LOWASA KURUDI TENA CCM

🔵Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba (CRM)

Watu wengi kwa kutokuelewa kilichopo nyuma haya hayo yote wanaweza kutoa sababu zao ambazo kwa juu juu zinaakisi ukweli kutokana na hali ya nchi inavyoendeshwa sasa kutokana na utawala wa ccm ya Magufuli

Watu wengi ukiwauliza watakwambia Lowasa na Sumaye wametoka kutokana na uchu wa madaraka baada ya kukosa walichokuwa wakitaka ikiwa ni nafasi ya urais kwa Lowasa na nafasi uongozi kwa sumaye Wengine watasema ni wanafki na wengi watasema wamekwepa mateso na manyanyaso waliyokuwa wanayapata kwa kuwa upinzani ikiwa pamoja na kufilisiwa mali zao na kutishiwa kuuwawa kwa kuwepo upinzani yaani CHADEMA

Lakini leo nataka niwaambie hayo yote hakuna hata moja lililo na ukweli ndani yake, ni sababu za kujihami tu zinazotolewa ili kulinda chama.Ila mpango wa Lowasa na Sumaye Kujitoa CCM na Kuonekana Kujiunga na CHADEMA na , pia hao hao kurudi tena CCM ni mpango uliopangwa kamili tangu Mwanzo na KAMATI MAALUM YA KIJASUSI (KIINTELIGENSIA) Ndani ya CCM au Serikali ya Tz

Wengi wasioyajua haya wanaweza kupinga kishabiki kama ambavyo wangeweza kupinga ikiwa tungewaeleza mapema juu ya mpango huu Ulioratibiwa na watu wachache sana ndani CCM ambao hata CCM wengi hawalijui hilo kwani ilikuwa ni mkakati wa kiinteligensia na kiusalama zaidi ili kuepusha jahazi la CCM ambalo lilikuwa linaenda kufa mikononi mwa Rais J Kikwete

Kutokana na vuguvugu kubwa walilokuwa nao wananchi wa Tz la kutaka mabadiliko kupitia UKAWA katika Mwaka 2015 ambalo lilionyesha dalili ya kuwepo kwa uwezekano wa CCM kutolewa madarakani ikiwa hakutakuwa haitakuwa na tahadhari ndipo wakubwa wachache walipouandaa mpango huu wa kiusalama

Kama nilivyotangulia kusema mpango huu ulifanywa na kujulikana na wakubwa wachache sana ndani ya CCM na Majususi wa mambo ya kisiasa, Ndipo walipopanga kuwatoa sadaka Waliokuwa Mawaziri Wakuu wakubwa wawili yaani Lowasa na Sumaye ambaye mmoja wao(Lowasa) alikuwa na mvuto mkubwa sana wa kisiasa na mtaji wa watu wengi

Mpango wa kumtoa Lowasa ulipangwa mapema kabisa ndio maana Uliaanza kuona LOWASA AMEKATWA KTK WAGOMBEA URAIS WA 2015 . Lakini huo ulikuwa ni mpango kamili uliokuwa ukilenga kuwavuta Wapinzani Kufurahia anguko hilo la lowasa kukatwa kwa faida yao

Mpango huo ulikuwa kuwa Kwanza Kumtafuta Mgombea na mwanasiasa ambaye alikuwa na ana mvuto mkubwa kwa CCM na Upinzani ambaye Ikiwa wangemkataa huyo basi Upinzani wangetamani kumchukua na kumtumia kama mtaji wao ili Kupitia huyo ndio ingewaaminisha wananchi na upinzani Kuwa CCM inaenda kugawanyika kwa kuondokewa na Wakubwa wa chama wa muda mrefu

Mpango huu ulilenga Ikiwa Lowasa angetoka na kuhamia upinzani na kupewa dhamana ya urais , hata kama ingetokea ashinde bado ilikuwa wamekubaliana Nae kuisaliti upinzani kwa kuirudisha serikali mikononi mwa CCM.

Lakini hasaa ilikuwa ni mpango wa kupunguza nguvu za Upinzani kwani Kupitia hao ndio walikuwa Chachu ya kuiua upinzani kwani ndio waliokuwa wanavujisha siri za wapinzani.Kumbuka Lowasa na Sumaye mara baada ya Kujionyesha kuhama CCM waliaminiwa na CHADEMA hata kupewa uwakilishi kwenye Mabaraza makubwa ya maamuzi ya Chama.Hiyo ndio Ulikuwa Mpango wao kuwaingiza Sumaye na Lowasa huko ili kutaka kutafuta kuidhohofisha Nguvu ya upinzani na kutaka kujua ikiwa Upinzani walikuwa wapewa nguvu na mataifa ya nje au la?

Ndio maana mara baada ya Lowasa kuhama CCM na baadae Sumaye Alifuata , na kweli Upinzani wakaingia katika mtego ule ule kama ulivyopangwa na Kamati ya Kijasusi ya CCM.Viongozi hawa Lowasa na Sumaye waliletwa upinzani kwa makusudi ya kutaka kuwafanya wapenye na waaminiwe kabisa kupewa nafasi za juu zaidi ili kuiua kabisa Upinzani ndio maana Kwa muda mrefu wamekuwa na mawazo kinzani sana na yakuwavunja moyo viongozi wa juu wa upinzani ktk vikao vikubwa vya maamuzi

Kumbuka hata Plan ya Kumchagua Rais JPM kama mgombea kwa tiketi ya CCM watu wengi wa ndani ya CCM na nje Ya CCM waliishangaa kwani hakutegemewa wala hakupangwa hivyo tangu mwanzo bali ilikuwa ni Plan B ya watu wachache ndani ya CCM wenye nguvu ya maamuzi waliokuwa Kwenye Kamati hiyo ya Kijasusi(Inteligensia) Kwa lengo la kukisaidia chama kisife ndio wakatumia mpango huo wa kumuinua Mtu mwingine asiyedhaniwa wala kufikiriwa kabla na ndio nguvu zote za Chama hawakuwa na jinsi ilibidi waende nae tu kama Maamuzi ya watu hao wachache yalivyopangwa katika Kamati hiyo ya Kijasusi

Hivyo niseme tu, haina haja kuanza kuumiza kichwa sasa na kutoa sababu zisizo na ukweli juu ya Kurudi kwa Sumaye na Lowasa CCM, huu ulikuwa ni Mpango kamili na wameshakamilisha Kazi waliyotumwa hivyo sio ajabu wakirudi kwao walipokuwa CCM.

Tatizo kubwa la Wapinzani wa tanzania na ikiwa hawatajirekebisha bado wataendelea kuitwa wapinzani yaani hawatakuja kuwa watawala wa Nchi hii ni kwasababu Wanadhani Swala la kutawala nchi ni swala la tu la kuweza kuongea jukwaani na wananchi na kuwapa ahadi nzuri ndio maana nguvu kubwa wameielekeza katika KUTAFUTA UHURU WA MAONI. Hata ikitokea CCM imewapa Uhuru wa maoni bado mnaweza msishike dola na hata mkishika bado mnaweza msiongoze nchi vizuri

Huwezi kutamani Kutaka kushika nchi na kutawala kisiasa ikiwa HAUJUI KUFANYA UJASUSI WA KISIASA au Ikiwa hauna Majasusi ndani ya Chama chenu wanaoweza kuchunguza, kusambaza propaganda na hata Kutengeneza matukio yatakayoweza kuhamisha uelekeo wa Mshindani wako katika Siasa

Moja ya Trick ambayo CCM wamefanikiwa kuitawala nchi hii na kuwashinda Wapinzani sio kwasababu ya Nguvu kubwa tu wanayotumia CCM bali ni Kuwa Wapinzani hawana MAJASUSI NDANI YA CHAMA watakaoweza kufanya Ujasusi wa chini chini utakaoweza kuibua matatizo na kuyashuguulikia

Na Kwa hili Swala la Lowasa na Sumaye Kutumwa Upinzani na Kurudi tena CCM baada ya kumaliza kazi waliyotumwa ni moja ya Matukio ya kiinteligensia ya CCM waliyofanikiwa kuwaweza wapinzani wao ambalo lilipelekea wengi wanaofuata upepo wa wanasiasa kuchukuliwa na wimbi waliloliona kama ni wimbi la mapinduzi kumbe Ulikuwa ni mpango uliosukwa na watu wachache Akiwamo JK na Kamati hiyo ya Kijasusi.

Kwa kukosa umakini na tahadhari kwa Vyama vya upinzani na kwa kutokuwa na Kamati za Kijasusi ndani ya Chama ndio kimepelekea hata Upinzani kufifia nguvu yake kwa watu hasa tunapoelekea Uchaguzi mkuu 2020.

Hata kama Mikutano imezuiwa kinyume cha katiba, uhuru wa vyombo vya habari umeminywa,Uhuru wa maoni umeondolewa kinyume cha katiba bado Haimaanishi Akili hamna. Ushindi sio Vita ya maneno bali ni Vita ya Akili.

Ikiwa Chama cha Upinzani kimekosa Akili au Plan B ya kufanya hata kuwafanya wanachama wao nao kukosa direction ya kujua lipi la kufanya katika mazingira magumu haya wanayopitia basi Chama hicho kitakosa Akili ya kufanya hata pale watakapopewa nchi kutawala kwani kuna mashambulizi mengi na vita nyingi za kisiasa na kiuchumi za ndani na nje ya nchi ambazo zitahitaji akili nyinyi sio maneno mengi, ambazo ushindi wake utategemeana na Uwezo wa chama tawala katika njia za kijasusi
 
Niwahi sema kuwa huyu bwana lowasa hela yake yote aliofanyia kampeni alirudishiwa je hii ilikuwa njama anyamazishwe au ni mipango ilikuwa
 
MWAISEMBA CR,
Upumbavu tu. Unasema vyama viwekeze kwenye ujasusi, next time utasema upinzani au vyama uwekeze kwenye majeshi yake.

Hakuna aliyewatuma lowasa na sumaye upinzani, acha story za kijiweni, wala hakuna kazi wameifanya,

Ccm hawataki siasa za kidemokrasia, hivyo hawahitaji inteligensia, wanahitaji polisi tu kukaa madarakani
 
MWAISEMBA CR,
Hili jambo liko wazi tangia zamani labda kwa yule mwenyewe uelewa mdogo wa kushabikia bila reasoning!

Chakuongezeana kukumbusha watu ni kwamba, vyama Vinci hapa Tanzania vilikuja ili kuokoa jahazi la uchumi wa nchi, so vyama vyote viko chini ya CCM kwa mfano Mbowe ni mtu wa serikali (under cover) agent!
 
Ni maoni yako yanapaswa kuheshimiwa. Na wewe mwenye mawazo usilazimishe mawazo yako kila mtu aya kubali.

Na Yataongelewa mengi sana.
 
Back
Top Bottom