Wenyeviti 11 wa Mikoa CHADEMA wampinga Dr Slaa

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Wenyeviti 11 wa mikoa wa CHADEMA wamepinga uamuzi wa Dr Slaa wa kutengua uteuzi wa David Kafulila. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo tarehe 14 Novemba, ambalo halijataza majina wala mikoa ya wenyeviti hao, wenyeviti hao wanaelezwa kuutafsiri uamuzi huo kuwa ni kuendeleza kambi za uchaguzi wa chama hicho wa septemba 2009.

Habari hiyo inaeleza kuwa wenyeviti hao wanaamini kwamba David Kafulila alikuwa ndiye kinara wa kambi ya Zitto Kabwe. Habari inaeleza kwamba wenyeviti hao wanamsubiri Dr Slaa kwenye kikao cha Kamati kuu ya chama hicho kilichopangwa kufanyika Nov 27 na 28 waweze kumpinga.

Habari hiyo imemnukuu Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kigoma akieleza kwamba wao bado wanamtambua David Kafulila kuwa ni Afisa wa chama kwa kuwa hajapewa barua rasmi na makao makuu kuelezwa kwamba uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha katibu huyo, anayefahamika kwa jina la Msafiri Wamalwa amemueleza Kafulila kuwa ni Afisa anayetoka katika Mkoa wake Jimbo la Kigoma Kusini ambapo ni kati ya maeneo ambayo chama hicho kimefanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake David Kafulila ameeleza kuwa alipokea mwaliko wa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mo Ibrahim hapa Tanzania chini ya Katibu wa zamani wa UN Koffi Annan

......ndiyohiyo
 
Huu uzushi wa Mwananchi, si watupe basi majina ya hao wenyeviti wa mikoa na kauli zao? Halafu hivi afisa akitenguliwa ajira yake ni lazima mkoa wake wa asili ujulishwe kwa barua? Halafu wenyeviti wa mikoa watasubirije kamati kuu wakati wao kikatiba sio wajumbe wa kamati kuu kwa mujibu wa katiba mpya wao ni wajumbe wa baraza kuu?

Asha
 
CHADEMA as a political party kimeanza kukua, na katika mchakato wa ukuaji kinavutia wengi. Sasa inakuwa kama kokoro la wavuvi. Wakati walengwa kwenye kokoro huwa ni samaki wanaoliwa, humo utakuta konokono na takataka nyingine za majini. Takataka hizi zisizotakiwa hujulikana pale kokoro linapokuwa limevutwa na kufikishwa nchikavu.
 
Hakika CHADEMA pamoja na kuwa ni chama cha UKABILA NA UKATOLIKI lakini Dr Slaa ndie atakae imaliza Chadema.

Ningekuwa Mkatoliki au Mtu ninayetokea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ningeshauri huyu wamuondoe maana yake ana chuki sana na mnafiki mkubwa sana huyu .
 
Huu uzushi wa Mwananchi, si watupe basi majina ya hao wenyeviti wa mikoa na kauli zao? Halafu hivi afisa akitenguliwa ajira yake ni lazima mkoa wake wa asili ujulishwe kwa barua? Halafu wenyeviti wa mikoa watasubirije kamati kuu wakati wao kikatiba sio wajumbe wa kamati kuu kwa mujibu wa katiba mpya wao ni wajumbe wa baraza kuu?

Asha

Kila mara mimi nimekuwa nikimtilia mashaka sana (maandishi yake) huyu kijana anayejiita mwanamapinduzi wa gazeti la mwananchi, yaani Ramadhani Semtawa. Ukisoma kwa makini(kati ya mistari) maandishi yake, anaelekea kuwa mkosoaji mkubwa wa Chadema, na Mbowe. Tena wakati mwingine inaonekana wazi ni hisia tu zinamsukuma.

Yeye na Makwaia wa Kuhenga tofauti yao ni katika majina tu na vyombo wanavyoviandikia. Lakini wote wamevaa magwanda waliyonunuliwa na Rostam Aziz. Pumbaf!
 
Du!
 
Ni mduara wa mshughulikia Mbowe lakini mlengwa halisi ni Dr Slaa. Na ukichambua sana kwa kweli mlengwa ni CHADEMA. Lakini wao ukiwauliza huwa wanajibu wako kumtetea Zitto dhidi ya viongozi wenzake wanaomtenga na kukigeuza chama kuwa cha kikabila. Mduara huu uko kwenye vyombo vitatu vya habari. Pale Mwananchi mduara huu kinara wake ni Denis Msacky, ukimundoa Semtawa, mwandishi mwingine ni Fidelis Butahe. Wenyewe huwaita wanaotofatiana na Zitto kuwa ni enemies of truth. Pale habari Corporation Kinara ni Muhingo akisaidiwa na Ballille, mwandishi wanayemtumia ni Dada Sarah Mossi. Kwa bahati mbaya, ajenda zao zinafanana sana na za Rostam Aziz dhidi ya CHADEMA. Mwenye kujua undani wa mduara huu atuanikie zaidi

serayamajimbo
 
Habari hii leo imezua mambo kwetu, tulitaka nasi turuke nayo. Lakini kila mwenyekiti wa mkoa wa CHADEMA tuliyemhoji amekanusha kuwa hakuna kitu kama hicho. Kuna mtu ana namba ya simu ya Zitto alipo ujerumani? Tafadhali anitumie kwenye PM
 
Hakika CHADEMA pamoja na kuwa ni chama cha UKABILA NA UKATOLIKI lakini Dr Slaa ndie atakae imaliza Chadema.

Ningekuwa Mkatoliki au Mtu ninayetokea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ningeshauri huyu wamuondoe maana yake ana chuki sana na mnafiki mkubwa sana huyu .
Tumechoka na upuuzi huu kila siku, kama huna cha kuandika si usome tuu. Ajira ina kuonywa,kufukuzwa au kutenguliwa iwapo hukidhi matarajio ya mwajiri wako. Sasa laajabu ni nini kwa Slaa kusitisha ajira hizo? Mwacheni Dr afanye kazi yake bila kuogopa
 
Hahitaji uwe na degree kutambua kuwa habari ya gazeti hilo ni za kupikwa.

Ila Mungu ametujalia wengine tuna uwezo wa kupembua mchele na pumba.

Hivi ni wapi Zitto alipopinga kusimamishwa kwa Kafulila na mwenzake? nimejaribu kutafuta sijapata.

Naomba mnisaidie hiyo sehemu aliposema hayo. Hawa waandishi wanachadema msipokuwa makini watakivuruga chama chenu.

Isije ikawa kuwa Dr Slaa naye alitoa maamuzi yake kwa kusoma haya magazeti!!!
 
Tumechoka na upuuzi huu kila siku, kama huna cha kuandika si usome tuu. Ajira ina kuonywa,kufukuzwa au kutenguliwa iwapo hukidhi matarajio ya mwajiri wako. Sasa laajabu ni nini kwa Slaa kusitisha ajira hizo? Mwacheni Dr afanye kazi yake bila kuogopa
Kama kweli Dr Slaa ni muadilifu kwanza angeanza kumtimua Mwenyekiti wake anayetumia Chama kama taasisi au NGO yake binafsi na kuviacha hivi vidagaa.

jamaa angekuwa anatokea kaskazini basi yangemalizwa kilaini kabisa.

Dr Slaa hafanyi kazi kwa matakwa yake bali anasukumwa na watu nje ya mduara ili wapate manufaa baadae.

HAFAI KABISA KUWA KIONGOZI WA KITAIFA. MDINI NA MKABILA NO 1
 
Kila mara mimi nimekuwa nikimtilia mashaka sana (maandishi yake) huyu kijana anayejiita mwanamapinduzi wa gazeti la mwananchi, yaani Ramadhani Semtawa. Ukisoma kwa makini(kati ya mistari) maandishi yake, anaelekea kuwa mkosoaji mkubwa wa Chadema, na Mbowe. Tena wakati mwingine inaonekana wazi ni hisia tu zinamsukuma.

Yeye na Makwaia wa Kuhenga tofauti yao ni katika majina tu na vyombo wanavyoviandikia. Lakini wote wamevaa magwanda waliyonunuliwa na Rostam Aziz. Pumbaf!
Kuna tatizo gani kukosoa Chadema, chadema ni taasisi lazima ikosolewe agh!
 
Kifupi kwa mwenye kujua maana ukisoma hizi habari utaelewa kwamba ni ktk mlolongo wa kuimaliza Chadema na hakika wanaoimaliza ni wao wenyewe wanachama. Makundi haya, chuki na roho ya kwanini, hata imefikia watu kutozungumza wakati ni viongozi wa juu inatisha.. Uswahili mtupu na kila mmoja wao anatazama mnakalio ya mweziwe..

Msiwalalamikie waandishi wa habari, matatizo yapo ndani ya chama na kwa bahati mbaya ni viongozi wachafu wa midomo ndio utawasikia sana wakiandika..Mbona simksikii Dr. Slaa na Mbowe wakijjiunga na habri hizi za mipasho!.. Wahenga wanasema - When searching for truth look no further than yourself!
 
Chadema is yet another disapointment to majority of Tanzanians...lol...huyu Slaa updre ndio maana ulimshinda au laana ya wakatoliki inaendelea kumla!
 
Kila mara mimi nimekuwa nikimtilia mashaka sana (maandishi yake) huyu kijana anayejiita mwanamapinduzi wa gazeti la mwananchi, yaani Ramadhani Semtawa. Ukisoma kwa makini(kati ya mistari) maandishi yake, anaelekea kuwa mkosoaji mkubwa wa Chadema, na Mbowe. Tena wakati mwingine inaonekana wazi ni hisia tu zinamsukuma.

Yeye na Makwaia wa Kuhenga tofauti yao ni katika majina tu na vyombo wanavyoviandikia. Lakini wote wamevaa magwanda waliyonunuliwa na Rostam Aziz. Pumbaf!

Ndugu yangu Invicible, tatizo sasa sio huyu mwandishi tu
Tatizo ni hata Chadema , je haina kitengo cha uchunguzi kama huu?

Just imagine wewe na makazi yako umeona hicho Chadema pengine hawajaona hilo.Kama wameona wamechukua hatua gani

Jamani Chadema inabidi kuwa wakali kama kuna mtu kwa makusudi kabisa anapindisha habari, ukali huu ni ku-mface. ajue mnajua

Ila kuna uwezekano mkubwa pia akawa ana urafiki na mtu aliyemo Chadema, akawa anasema vitu ambavyo hata wengine ndani ya chama hawajui!

To solve this needs intelejinsia! mpelelezeni kila hatua mtampata tu mbaya wenu, believe me!
 
Chadema is yet another disapointment to majority of Tanzanians...lol...huyu Slaa updre ndio maana ulimshinda au laana ya wakatoliki inaendelea kumla!

na atazidi kulaaniwa duniani na hata mbinguni.
 
Kama kweli Dr Slaa ni muadilifu kwanza angeanza kumtimua Mwenyekiti wake anayetumia Chama kama taasisi au NGO yake binafsi na kuviacha hivi vidagaa.

jamaa angekuwa anatokea kaskazini basi yangemalizwa kilaini kabisa.

Dr Slaa hafanyi kazi kwa matakwa yake bali anasukumwa na watu nje ya mduara ili wapate manufaa baadae.

HAFAI KABISA KUWA KIONGOZI WA KITAIFA. MDINI NA MKABILA NO 1

No, nadhani huyu mwenyekiti amefund sana hiki chama, so bado anakidai
 
Back
Top Bottom