Wenyeji wa iramba-singida

mtamanyali

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,161
613
Wanajamvi poleni na mihangaiko ya kila siku. Mimi ni mwalimu wa shahada ya kwanza na hivi karibuni wizara imenipangia iramba mkoani singida kama kituo changu cha kazi. Tatizo siifahamu hata kidogo wilaya hiyo naomba wanajamvi mnisaidie ili walau nipate picha ya sehemu ninayoenda au kama kuna mtu anapenda kwenda huko tunaweza kubadilishana. Naomba kuwasilisha.
 
Usiwe na haraka mkuu.
Ulitaka kazi na sasa umepata.
Kafanye kazi acha kutafuta mtu wa kubadilishana nae.
Ukitoka huko upo fluent kinyiramba,hahahahaaaaa.
OTIS
 
Sina uoga wa kazi wakuu ila napenda niyafahamu mazingira niendayo kwani sikuwahi hata sikumoja kufikiri kama nitaishi kule.
 
Congratulation kwa kupangiwa Iramba! mimi ni mwenyeji wa Iramba mkoani Singida. Kusema kweli wilaya hii ni kubwa sana na watu wake ni wakarimu sana. Kuna Wanyiramba na Wanyisanzu[ mimi pia ni Mnyisanzu] ambayo ndio makabila yanayopatikana ktk hii wilaya.Miundombinu ya wilaya hii kama barabara siyo ya kuridhisha sana ila huduma zingine za kijamii kama hospital,maji na umeme they are satisfactory available depending on the specific area.Mkuu nipigie kupitia 0755 095221 / 0657 218805 nikujuze zaidi.
 
sina uoga wa kazi wakuu ila napenda niyafahamu mazingira niendayo kwani sikuwahi hata sikumoja kufikiri kama nitaishi kule.

kwanza hongera kupata kazi huko......napenda kukutoa uoga kabisa....iramba hakuna shida kabisa maana ukisafiri mathalani toka dar mpaka huko unafika siku hiyo hiyo
pili siku hizi kuna lami toka dar mpaka huko lami hii ya kwenda mwanza
nakumbuka kipindi cha nyuma ilikuwa shida kidogo...kwa mfano mimi naishi kahama ilibidi wakati mwingine tulale singida asubuhi twende...lakini sasa ni safiiiiii hakuna shaka....
Tatu iramba ni wakulima wazuri wa karanga,wafugaji wa kuku,pia wanalima mahindi kidogo na mtama na uwele, japo si kubichi sana lakini pia si kubaya sana!
Mwisho nakutoa hofu nenda kafanye kazi...kama mimi nilivyo amua kufanya kazi kahama
 
Congratulation kwa kupangiwa Iramba! mimi ni mwenyeji wa Iramba mkoani Singida. Kusema kweli wilaya hii ni kubwa sana na watu wake ni wakarimu sana. Kuna Wanyiramba na Wanyisanzu[ mimi pia ni Mnyisanzu] ambayo ndio makabila yanayopatikana ktk hii wilaya.Miundombinu ya wilaya hii kama barabara siyo ya kuridhisha sana ila huduma zingine za kijamii kama hospital,maji na umeme they are satisfactory available depending on the specific area.Mkuu nipigie kupitia 0755 095221 / 0657 218805 nikujuze zaidi.

nashukuru sana ndugu kwa maelezo yako ama kweli wewe ni muungwana. Nategemea mengi kutoka kwako. Nitakupigia badae mana kwa sasa nipo kazini.
 
kapaone kwa macho usiporidhika unaondoka... Mimi mwenyewe nlipangiwa singida mjini mwaka jana nliumwa kwa uoga.. Lakini nkakaza nikaja ona mwenyewe.. Nna mwaka sasa huku.. Jikaze jembe
 
kwanza hongera kupata kazi huko......napenda kukutoa uoga kabisa....iramba hakuna shida kabisa maana ukisafiri mathalani toka dar mpaka huko unafika siku hiyo hiyo
pili siku hizi kuna lami toka dar mpaka huko lami hii ya kwenda mwanza
nakumbuka kipindi cha nyuma ilikuwa shida kidogo...kwa mfano mimi naishi kahama ilibidi wakati mwingine tulale singida asubuhi twende...lakini sasa ni safiiiiii hakuna shaka....
Tatu iramba ni wakulima wazuri wa karanga,wafugaji wa kuku,pia wanalima mahindi kidogo na mtama na uwele, japo si kubichi sana lakini pia si kubaya sana!
Mwisho nakutoa hofu nenda kafanye kazi...kama mimi nilivyo amua kufanya kazi kahama

nashukuru kaka kwa kunipa moyo.
 
kapaone kwa macho usiporidhika unaondoka... Mimi mwenyewe nlipangiwa singida mjini mwaka jana nliumwa kwa uoga.. Lakini nkakaza nikaja ona mwenyewe.. Nna mwaka sasa huku.. Jikaze jembe

thanks ndugu
 
nashukuru sana ndugu kwa maelezo yako ama kweli wewe ni muungwana. Nategemea mengi kutoka kwako. Nitakupigia badae mana kwa sasa nipo kazini.

do upo kazini na iramba unaenda kufanya nini? unaacha computer unaenda kushika chaki, kujisaidia vichakani, kutembea kwa mguu umbali mrefu du fikiri mara mbili
 
nani kama singida,nani tena kama iramba.....................samaki wa kiteka,nyama ya kuku wa kienyeji,mayai............daaah!nani kama singida.
watu wake wakarimu,wasichana warembo,wenye asili ya bara la arabu na asia,hawana kinyongo na wageni waingiao na watokao............................nani kama singida.
mafuta ya alizeti,asali kweli singida kiboko.
karibu sana singida ujusikie upo nyumbani,karibu sana mwalim.sikupi namba yangu kwa kuwa tayari umeshapata hapo juu.
 
kaka nipo kazini bado najifikilia ndio maana naulizia mazingira nisije nikajilaumu badae
 
asante sana mwenyeji wangu
 
kaka nipo kazini bado najifikilia ndio maana naulizia mazingira nisije nikajilaumu badae

Kama uko kazini jaribu kuangalia wapi utapata faida na kujipanga kimaisha vizuri zaidi.. Mfano
1.compare mshahara.. Kama una bachelor huku uatakula 469,200 gross take home kama 402,000..
2.job security its almost impossible kuskia serikali imemtimua mfanyakazi wake especially mwl
3. Fursa za kwenda kusoma after two yrs huku ukiendelea kula mshahara.. Private firms nyingi ukienda soma imekula kwako
4.vijiziada.. Kusimamia na kusahihisha mitihani kuanzia mock hadi necta form2,4 na 6..kumbuka kjjn walimu sio wengi saana so no competition/haka kamchakato kana bonge ya hela
4.seminers
5. Kula vijicheo ni kawaida na utakuwa unazitauna kimtindo
6. Singida fursa zipo kununuavitunguu na alizeti kwa farmers kuziuza kwa hela ya kutakata zikianza kuadimika .... Hakunaga kuku wala mayai ya kizungu huku... Kuku waukweeeli umeuziwa hela kubwa sana buku6.. Achilia mbali nyama ya ng'ombe na mbuzi+maziwa/wafugaji hawa
jIONGEZE JEMBE....CHANGANYA NA ZAKO
 
thanks great thinker!
 
Mwalimu inategemea umepangwa tarafa ipi,maana iramba kulu kuliko TZ,wenyeji hutumia kamsemo hako.Usinisjangae ninacho kuambia ukweli Iramba nikumbwa.
 
Kafanye kazi bana!Iramba kupo bomba tu.,,,ukifika kule utasikia wanasalimiana "mbi!""iiiiiza mbwanewe!
 
Back
Top Bottom