Wenye watoto wa kike wafundisheni binti zenu kujitegemea, wasitegemee pesa ya mwanaume

Yes Boss, I agree with you
Your words are 100% true.

Ni vizuri kuridhika, kuishi maisha halisi na kukubaliana na hali iliyopo katika maisha yenu/yako. Baada ya hapo mnaongeza juhudi za kutimiza ndoto zenu.

Pesa itumike kulingana na kipato (gharama zisiwe kubwa), akiba ipatikane na pesa ya dharura pia iwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja
 
Mwanamke kaumbwa kwa hisia ya kusaidiwa ukiona mwanamke asie penda kuhongwa huyo ni Jike dume jiepushe nae ukimzoea atakunyonya damu
 
brother tafuta pesa aisee on top of your personality, kama vitu vidogo kama pesa vinakuvimbisha bandama namna hii, tafuta mwanamke mmoja asiyependa hela oa kisha muhudumie, ukihangaika na michepuko at your own risk, kwa maana hata hao financially stable women asilimia kubwa wanapima kama utatoboa ama vipi na hawawezi kukukubali wewe zaidi ya mtu mwenye pesa zaidi yako ipo hivyo karne na karne, mtoto wa kike anaozeshwa kwa familia tajiri all for her welfare and family stability

Kwa sasa mambo mengi yamebadilika kwa namna jamii inavyoishi, wote tuna push watoto wetu wa kike wajitegemee, wajenge nyumba na wanunue magari yao, waishi namna wanavyotaka wao na kuacha kumtegemea mume, hilo ni kosa kubwa kwa upande wangu, unampa pressure mtoto ya kutafuta kwa means yoyote ile ikiwemo hiyo ya kuingia katika mahusiano kwa ajili ya kutafuta pesa.

Tunasisitiza kwenye uchumi lakini siyo maadili. Hata awe na pesa vipi akikosa maadili ni kazi bure.

Wazazi na jamii msiwape pressure watoto wa kike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndiyo maana kuna kundi kubwa la wadada wanaoliwa 'tigo' ila tukiongea ukweli, wadada wengi wanajiuza indirect, wana msemo wao eti 'mwanaume anamuweka mjini'
 
Naungana na mtoa mada...wanaume wengi ndo tunaowalemaza akili wanawake kwanzia wakiwa watoto(mtoto wa kike anahitaji kua karibu zaidi na baba) mpaka wakiwa wakubwa kuwafanya wategemee akili za wanaume moja kwa moja utadhani Mungu alitupendelea akili wakati alitupa wote sawa.

Hiyo imepelekea wanawake wengi mno(japo sio wote)kua vilema wakutumia akili zao ipasavyo,akili na fikra zao zimeshajengeka kupewa,kutegemea fikra za wanaume,wao ni kuwaza kuvaa,kula,vitu vizuri tu!

Katika kutumia fikra zetu huhitaji kua na uume na pum** bali ni akili akili ambayo kila mwanadamu amepewa bila upendeleo wowote ule.

Siku mumeo akifa,akifukuzwa kazi,akifilisika,akiumwa hoi kitandani au chanzo unachokitegemea utafanyaje kama sio kutoa mwili wako kwa wanaume wengine ili ujikimu kimaisha!?

Nyie wanaume wenzangu mnaosema wanawake eti ni maua,mnawalemaza mno aisee.mwanaume ni jukumu lake kuitunza familia yake kwa kila kitu asilimia 100 ila usimuache mkeo alemae akili zake bila kua na kitu chakufanya kumuingizia kipato kabisa.siku ukikwama je?ukiumwa hoi kitandani?ushafikiria siku ukifa je watoto wenu watakula nini?watasoma?watakua na maisha gani?
Au mnategemea watatunzwa na ndugu zenu au kanisa na misikiti!?

Huu hapa chini ni mfano uliopo kwenye biblia juu ya mwanamke mjane mmoja ambae mumewe alikua mchungaji amekufa amemuacha mkewe na hali mbaya ya kiuchumi,madeni mengi ambayo aliingia mkataba watoto wakawe watumwa endapo atashindwa kuyalipa.so akamfwata nabii Elisha amsaidie juu ya hali yake kisa tu mumewe alikua mtumishi wake.
Ambapo alipewa ushauri wakujikomboa kwenye hali ngumu kwa vitu ambavyo alikua navyo nyumbani kwake ila hakuviona thamani yake au kuviangalia kwa jicho jingine sababu ya kulemaa fikra zake kutegemea kila kitu toka kwa marehemu mumewe.

Kwa dunia ya sasa nawaambieni wake zenu wataliwa mno ili kuwalea wanao!



2 Wafalme 4:1-7
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache.

Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Nenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom