Wenye watoto njooni huku

Wenye watoto njooni huku

ney1

Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
25
Reaction score
6
Habari za jioni wapendwa.

Naombeni uzoefu kwa mliopitia hii hali hasa single mom.

Mchumba wangu alifariki nikiwa na mimba ya miez 2 tayari tulikuwa tumekamilisha taratibu zote ilibaki ndoa tu alipata ajali na kufariki ( mungu amlaze pepa)
baadhi ya dada zangu walinishauri nitoe lakini sikuona haja niliamini mungu anamakusudi yake,, mama angu alinitia moyo sana.

Sasa mtoto anamiezi 4 wazazi wameamua niende chuo nikasome! nawauliza wazoefu wa kulea je! nitaweza kusoma na mtoto mdogo?? nafasi imepatikana ya nurse( medical attendat) na nimeambiwa kuna day.... je? nikipata bint wa kunisaidia kukaa na mtoto nitaweza? wazoefu naomben msaada wa ushauri na mawazo pia.

Asanteni
 
kwani wazazi wako wapi......? ni bora kama mama yako ana nafasi akamlea mjukuu......miezi minne kwa upande wangu bado mdogo....na wadada wa kazi walivyo sasa ......inabidi sijui umfanyeje ili amlee mtoto vizuri.......
 
Utaweza tena wala haisumbui kbs cha muhimu upate dada mzuri anaependa watoto na pia kumbuka kuishi vzr na dada,atakulelea mtoto wako hd utapenda.
 
Unaweza kabisa!!Mimi nimesoma tangia mtoto wangu ana miezi 7 na nimemlea mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote na elimu yangu nimehitimisha na nafanya kazi ya maana.Muhimu ni uwe na nia na focus na usikate tamaa kwasababu si rahisi ni ngumu na kuna changamoto nyingi mno!!Lkn nashukuru alhamdulillah nimemaliza salama na sasa mtoto wangu ana miaka 6!Nilipohitimisha mm elimu yangu na yeye kaanza yake!
 
......pole sana kwa kufiwa na mpenzio, sasa wewe ndio mama na baba wa mtoto,kama huna kazi ya kueleweka kwa sasa......nakushauri nenda shule. Utaweza tu kusoma, as long as unamtu wa kukulelea mtoto.
Mtoto unaweza kumuacha na mama yako, mtafutie mdada awe anamsaidia kulea.
 
Usimwamini msichana wa kazi ht kwa saa1, km mama yupo na amekuruhusu ukasome mpe jukumu la kulea mjukuu wake
 
nikiwaza kuhusu msichana wa kaz ni changamoto
 
gorgeousmimi mwambie sasa how you did it.

ney1 hongera mwaya kwa kufanya maamuzi mema, na pole sana kwa kumpoteza mchumba wako. Huyo mtoto atakubariki sana. Itafika mahali utashindwa kuelewa usingekuwa na huyo mtoto ungeishije.

Anyway tukirudi kwenye swali lako. Mimi kama mimi nakushauri kama hiyo nafasi ya kusoma haina masharti sana (kwamba hata baadae bado hiyo opportunity utakuwa nayo) subiri. Mlee mwanao mwenyewe mpaka afikishe mwaka mmoja.

Mimi nimejitahidi miaka 2 mtoto wangu nimemlea mwenyewe na nnajua ni jinsi gani hicho kitu kimemfanya mtoto wangu awe alivyo. Yani hata mtu akikupa guarantee sasa hivi mwanao atakuwa hivyo utatumia kila dakika unayoweza na yeye maana ni zaidi ya raha kumuona mwanao akikushangaza kila siku itokayo kwa Mungu na watu watakavyomu-admire jinsi atakavyokuwa kama mashine.

Kwanza kukaa nae kutakupa fursa ya kumnyonyesha exclusively mpaka afikishe miezi 6, usiwe kama wadada wa mjini wanaojidai sijui hawana maziwa au muda. Maziwa ya mama yana faida nyingi (bond kati yako na mtoto, kitendo cha kumyonyesha tu kinamfanya ajisikie anapendwa, atajisikia amani kwasababu kuwa kwenye mikono yako kunamfanya aone kwamba yuko safe, ukuaji wake utakuwa mzuri kiakili na kimwili, ndo ile mtoto anatembea mapema watu wanashangaa bila kusahau kumkinga na magonjwa and so on). Yani mtoto atapata faida kiakili, kimwili na kihisia. Mpe hiyo nafasi bana. Hatopata mapenzi ya baba yake, basi wewe mpe all that you can give her/him.
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kabisa!!Mimi nimesoma tangia mtoto wangu ana miezi 7 na nimemlea mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote na elimu yangu nimehitimisha na nafanya kazi ya maana.Muhimu ni uwe na nia na focus na usikate tamaa kwasababu si rahisi ni ngumu na kuna changamoto nyingi mno!!Lkn nashukuru alhamdulillah nimemaliza salama na sasa mtoto wangu ana miaka 6!Nilipohitimisha mm elimu yangu na yeye kaanza yake!

na wewe ulifiwa na mchumba au ulionja utamu tu? Du una mtoto wa miaka 6? Shikamoo mama mdogo.
 
nikiwaza kuhusu msichana wa kaz ni changamoto
Kama uyasemayo ni yote ni KWELI basi pole.Ushauri mpe mama yako mzazi mtoto akulelee cha muhimu kuwepo na uwezo wa kumlisha maziwa na vimiminika vingine vyenye ubora kama unga safi wa dona na maji ya matunda yaliokamuliwa.Kama uko dar na huna uwezo wa kununua maziwa naomba uwasiliane na mimi ila tu endapo yote ulioyasema hapa yote ni kweli.
 
Mkuu hongera kwa kuchukua uamuzi mzuri wa kulea ujauzito na leo una mtoto . Mungu akubariki kwa hilo kwani wengi walishindwa na hawakufiwa bali ujana na sababu zingine ambazo hatuzijui.

Nafikiri uamuzi wa kusoma nao mzuri lkn hiyo shule/chuo ni boarding au day. Kama unaweza kwenda na kurudi basi mzazi wako anafaa kukaa na mwanao ukiwa chuo , siamini sana wasichana wakazi peke yao manake huyo mtoto bado mdogo sana . Endelea kusoma michango ya wadau utapata kitu.
 
habar za jion wapendwa
naomben ozoefu kwa mliopitia hii hali hasa single mom
mchumba wangu alifariki nikiwa na mimba ya miez 2 tayari tulikua tumekamilisha taratibu zote ilibaki ndoa tu alipata ajal na kufariki ( mungu amlaze pepa) .
baadhi ya dada zangu walinishauri nitoe lakini sikuona haja niliamini mungu anamakusudi yake,, mama angu alinitia moyo sana

sasa mtoto anamiez 4 wazazi wameamua niende chuo nikasome!! nawauliza wazoefu wa kulea je! nitaweza kusoma na mtoto mdogo?? nafasi imepatikana ya nurse( medical attendat) na nimeambiwa kuna day.... je? nikipata bint wa kunisaidia kukaa na mtoto nitaweza? wazoefu naomben msaada wa ushauri na mawazo pia.
asanten

Hao waliokushauri utoe mimba bado una undugu nao?
 
You are a strong woman. You went through the pain of losing your fiancee and carried your pregnancy to term.

You have taken care of your little baby too.

You sure as hell can go back to school.

You go back and study hard for your sake as well as the baby's.

Good Luck.
 
utaweza ila tafuta ndugu yeyote wa kikeni au kiumeni ukae nae amlee
 
Kwanini mzazi wako asije kukaa hapo na wewe na huyo H/G? Ili ukienda utaweza kusoma Kwa amani..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom