Wenye vyeti vyenye utata hawa hapa

Hi wanajamvi Cheti kua na utata inamaanisha nini?
Halafu kama mfanyakazi alihama kituo ccha kazi bahati mbaya kule alipotoka akawa hawaku mfungia data sheet haiwezi kusababsha mgongano wa majina na kuonekana kunautata?
 
Hizo dimension ambazo zimetumika kuangalia mfanano wa cheti. hakuna asiyefahamu majina ya kibantu yanafanana. hata kama hukusoma shule ukipewa kazi huwezi kuangalia majina tu
Ni kweli kabisa......Mimi mwenyewe mdogo wangu majina yote matatu anafanana na mwanafunzi mwenzake ila haikuwa shida kwani kila mtu ana namba yake ya mtihani.
 
Aaaaaaaaaah,Nani akubali ujinga huo....nakana na kwamba sikutambui mita 1million..
 
Naomba msaada orodha ya watumishi WENYE vyeti vinavyotumiwa na MTU zaidi ya mmoja yaani vyeti vya ' incomplete'
 
Hii hapa mkuu
 

Attachments

  • Taasisi_INCOMPLETE.pdf
    555.4 KB · Views: 87
Incomplete ni tofauti na cheti kimoja kutumiwa na mtu zaidi ya mmoja.

Incomplete maana yake taarifa zilizowasilishwa hazijakamilika
 
Nasikia hata yule Prof wanayesema ndio kiboko ya Tundu Lissu naye vyeti ni incomplete?
 
Kwa hiyo kuna vyeti vyenye utata, vyeti feki, watu wanaotumia majina yasiyokuwa yao (ingawa vyeti ni halali), wale wenye degree hewa (Vyeti halisi) n.k. Nilisikia wakisema mtu fulani hakutaka kufukua makaburi. Kumbe ameamua kuyafukua?? kama kaamua kufukua, basi afukue vizuri na afukue yote/kwa wote (Watumishi wote wa umma na taasisi zake, bila kujali unyeti wa taasisi hizo). Si mnataka kutenda haki na mna uchungu na jinsi nchi inavyopoteza fedha nyingi kutokana na watumishi hewa??
 
Kuna Majina Mengine si Rahisi kukuta watu wawili kama

Grace R. Turuka na Grace R. Turuka

Marry Abel Mntambo na Marry Abel Mntambo

Mhhh! Hizo ni Forgery za Kufa mtu hapo unakuta kuna Wakili Msomi anaenda Kuwatetea.
 
Back
Top Bottom