Wenye uchungu na nchi...

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
KWA wote wenye uchungu, nenda mkajifungue,
Mbunge katupa uvungu, hili tukalitambue,
Wao hawana uchungu, acheni watu waliwe,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Wagoma madaktari, nendeni kujifungua,
Uchugnu ukishamiri, hio mnashautiwa,
Angalia yaso kheri, kwao mnaowachagua,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Tumezidisha sanaa, kinamama kutania,
Kwa kwua wateuliwa, hili wanaliridhia,
Wengine wangelikua, wasingelivumilia,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Nchi hii ya wakubwa, wadogo kazi kuliwa,
Na uchungu si ubwabwa, hauwezi ukaliwa,
Mnyonge budi kukabwa, nchi hatutomwachia,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Mabavu tunatumia, vikaoni tukikaa,
Wengine tunakataa, na sheria kutumia,
Nchi hivyo haijawa, wala tena haijawa,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Kikao twakitumia, kampeni kupigia,
Kwa uchama tunapaa, wetu viti wametwaa,
Nani atawasikia, sauti wasiokuwa ?
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchungu mkijaliwa, huruma kuionea,
Taifa mkalilia, kuwa yasiyotakiwa,
Basi mmeshaambiwa, mwatakiwa kujifungua,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Mwatakiwa kujifungua, ushauri nautoa,
Upinzani mlokuwa, bado hivi mwatulia,
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wao mkawaachia, na uchungu wasokuwa,
Nia yao kutimia, wananchi wakajionea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Hivi bado mwachelewa, bado hamjajifungua ?
Au mnayangojea, operesheni kufanziwa,
Sezariani ikawa, na machungu kuzidia ?
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchungu 'naojua, tabu zetu kupungua,
Hao wakifurahia, mimi nashindwa elewa,
Hivi mema watutakia, au yepi wamenuia ?
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchungu ninaojua, rushwa ipate pungua,
Maofisi nazo njia, salama tukabakia,
Na sio kukamuliwa, kila unakopitia,
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchungu ninaojua, mfumuko kufumua,
Hadi chini kufikia, na bei zikapungua,
Fukara tukanunua, tushidnwavyo kununua,
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchungu ninaojua, posho zao kuachia,
Wenye dhiki kuzidia, ziende kuwafaa,
Mzaha mwatufanyia, hivi kweli mwajijua ?
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Uchama ukizidia, uoza unaingia,
Ikawa nchi balaa, kwa vyote kujiozea,
Pasiwe cha kunukia, ila kunuka usahaa,
Wote sasa kujizoa, 'spitali kwelrkea,
Wenye uchungu na nchi, tokeni mjifungue !

Mwaemanje Watanzania wenye akili huru ????
 
Rejoinder:

Nafasi za juu jama, zataka fikra na hadhi,
Wengine katika vyama, viwango bado hamkidhi,
Na kunena si hekima, hekima kitu waachi,
Wachache wanaosema, yawe bora si upuuuzi!!
 
Back
Top Bottom