Utakuta umeenda hospitali umepanga foleni na pengine mnaingia kwa namba kumuona daktari, unakaa zaidi ya masaa hata 3 unasogea tu kwenye foleni yako, ghafla anakuja mtu hapangi foleni, wala namba hana wala appointment na daktari hana, anaingia kwa daktari wanapiga stooooori kama saa moja hivi au zaidi nyie mmekaa tu kusubiri,mnabaki kusikia vicheko tu nje jamani hii inakuwaje, mimi sioni kama huu ni ustaarabu, hospitali huenda wagonjwa, hatuendi kupiga stori, kama una stori na daktari sikatai ila subiri muda wa lunch au hata baada ya kazi, watu wengine wanazidiwa na kupata madhara makubwa kwa kuchelewa kuhudumiwa na daktari.
Nawaomba sana watu wenye tabia hiyo muache, sio ustaarabu kabisa, mjue watu wakienda hospitali wanaumwa hawaendi kucheza au kujionyesha.
Pia viongozi wa hospitali mliangalie hili.
Nawaomba sana watu wenye tabia hiyo muache, sio ustaarabu kabisa, mjue watu wakienda hospitali wanaumwa hawaendi kucheza au kujionyesha.
Pia viongozi wa hospitali mliangalie hili.